Serikali tusimamie wananchi makampuni ya simu yanatuibia kwenye Internet

Serikali tusimamie wananchi makampuni ya simu yanatuibia kwenye Internet

Wa JF.

Watanzania kila kukicha wanazidi kukamaliwa na hawa wawekezaje huku serikali ikiwa upande wa wawekezaji.

Mabenki yanajipangia riba kubwa wanavyotaka wao lakini serikali wala haina tatizo kwenye hilo.

Sasa hivi haya makampuni ya simu yanafanya wizi mkubwa kwa wateja wake kwenye kuuza vifurushi vya Internet sasa hivi Airtel na Vodacom wanafanya wizi wa wazi 1GB unanunua Sh 5000 ya wiki lakini ndani ya siku 3 unaambiwa zimeisha.

Vodacom wao 1GB Sh 8000 ndani ya siku 3 hamna kitu.

Zamani walikuwa wanauza 1GB Sh2500 ikapanda mpaka Sh 3000 kwa wiki.

Serikali tusimamieni Watanzania tunaibiwa na haya makampuni ya simu.

Na hizo MB wanazouza hamna maelekezo ya kodi wanalipa kiasi gani TRA.

baada ya kuwaaaazibu wanaukuta/ukawa/chadema tutaongea na wamiliki wa hio mitando tuwaombe waache kuwaibia.

kuwa mzalendo mambo yatatulia tu.
 
wamebaki kuzima mawasiliano ya wapinzani huku wananchi wanaumia na bei za mawasiliano kila kukicha,sasa sio voda,Airtel wala Tigo wa Halotel wameunda cartel moja hatari ya kutuangamza kweli tunaisoma namba
 
Voda sasaivi hakuna kifurushi cha 1500 ni mwendo wa 2000. Zamani 1000 ulikua unapata atleast 1GB now ni 350MB.Dabo bando enyewe washatugeuka Kile cha wiki cha 8000 GB zimepunguzwa toka 3 hadi 2 per week wtf!!!!
 
Wameiua TTCL Makusudi na wanaiwekea mizengwe kufufuka ili Mabaka Uchumi waendelee kutuibia.
 
Haaa TTCL tokea lini akawa na huruma,tena yule ndio mbaya kuliko hao wengine.
Kaambiwa mwamzo miaka ya 90 mabadiliko ya matumizi ya simu,yeye tena kama mkongwe wa mawasiliano nchini akajifanya mobile haimtishi,huku akitubambikia madeni yasio yetu na landline zake zilizokuwa hadimu na poor service.
Hata alipojaribu kuingiza mobile alianguka chini kama mende sababu ya kufanya kazi kimazoe na kubebwa bebwa.
Kama haitoshi kapewa mkonga wa Taifa kuusimamia lakini hadi leo kashindwa kuusambaza.
Yule dawa yake ni kumpiga chini shirika likasukwa upya,wananchi wauziwe hisa hapo kitaeleweka.
 
Yaani Toka nimehamia halotel Niko pouwaaaa 2500 nafanya Nitakalo napiga cm full kujiachia kimbieni ili wajifunze

Halotel kwa sasa wako vizuri sana.

Ila sina hakika kama wataendelea kuwa wazuri huko mbeleni.
 
Hawa jamaa kila siku wanakuja na bei mpya za hizo bando zao.
Endelea kuisoma Mkuu Ritz mda kidogo mtaniona na mda kidogo hamtaniona tena maana nitapaa kwenda kwa baba
 
Yaani jamaa wana Uhuru sana wa kujipangia bei.. kila siku wanaweka viwango vipya, mtetezi wetu ni nani kwa hili.!?
Serikali inatoa bei elekezi kwenye sukari badala ya services kama hizi!!
 
hii wizara husika haisikilizi malalamiko ya wananchi. watumiaji wa ving'amuzi wamelalamika muda mrefu sana kuhusu kutoonekana chaneli za nyumbani kwenye tv lakini hawajapata msaada hadi sasa.
 
KWAKWELI HUU NI WIZI MTUPU!
Vodacom kila siku wanakuja na bei kandamizi za vifurushi na natumaini ukihamia 4G yao huto tuvifurushi tutakuwa tunayeyuka kisaniisanii ili mradi kudanganywa 'spidi'!
Kuna haja ya kufufua TTCL itukomboe upande wa internet!
Wameshafufuka Mkuu mda si mrefu wanaingia
 
Hawa jamaa kila siku wanakuja na bei mpya za hizo bando zao.

Mkuu nyie ndio mnaounga kila kitu mkono kwa sababu ya itikadi, wabunge wa chama chako ndio kabisa hakuna kitu wanahoji bali kuunga mkono, ukiwauliza kwanini mnaunga mkono bila kuangalia mwananchi aliyewachagua wanasema wao sio wapinzani kupinga kila kitu. Rais naye akifika kwenye hadhara anakula kick kwamba anawajali watu maskini, anashangiliwa ile mbaya, lakini akitoka hapo hakuna mtu anayeteleza anachosema!! Hujasikia sakata la makato ya VAT kwenye miamala ya benk na simu? Wamichinga unaona yanayowakuta hata baada ya yeye kuruhusu? Kinachotekelezwa kwa uhakika ni kutokujaribiwa. Tumepiga kelele hapa jukwaani kuhusu sheria inasemaje kwenye ving'amuzi kuhusu local channels lakini hakuna hatua yoyote inachukuliwa. Lakini viongozi wanapita hapa jukwaani kusaka eti walioshabikia polisi kuuwawa.
 
Wakati mwingine usiwe punguani kiasi hiki wewe kuwa mfuasi wa Mbowe ndiyo unajiona una haki ya kukosoa peke yako mapungufu ya serikali wapi nimeunga mkono kila kitu mimi JF nimekuja peke yangu sijaletwa na mtu na nitaondoka peke yengu tofuati na wewe umeletwa na Mbowe.
 
Kweli hata mimi mpaka Vodacom nimeweka mfukoni niko halote na tigo bora ingawa wote mchele mmoja mapishi mbalimbali
 
Wakati mwingine usiwe punguani kiasi hiki wewe kuwa mfuasi wa Mbowe ndiyo unajiona una haki ya kukosoa peke yako mapungufu ya serikali wapi nimeunga mkono kila kitu mimi JF nimekuja peke yangu sijaletwa na mtu na nitaondoka peke yengu tofuati na wewe umeletwa na Mbowe.

Samahani kama nimekuudhi, naona umepandisha jazba ya hatari mpaka umeendika sentensi ndefu bila koma wala nukta!! Na hilo linajidhihirisha maana hujajibu hoja zaidi ya jazba, na tatizo hilo sio wewe peke yako, huko ccm ni wote mko hivyo na ndio maana jeshi la polisi liko pembeni yenu kila siku kwa ajili ya udhaifu huu. Pole nisamehe kwa kukuudhi.
 
Hoja zipi ambazo unazo wewe zaidi ya viroja, sasa wewe mbona umendika gazeti lote hili hamna herufi ndogo zote.
 
Hoja zipi ambazo unazo wewe zaidi ya viroja, sasa wewe mbona umendika gazeti lote hili hamna herufi ndogo zote.

Naendelea kukuomba msamaha tena kwa kukuudhi. Kujenga hoja sio mchezo kama jeshi linasimama mara kwa mara kukulinda hata kama unachemsha. Kama ni hiyo post yangu ipitie tena uone kama kuna kosa hilo la kiuandishi unalosema. Samahani kaka sintorudia tena kukuudhi.
 
AIRTEL wamenikera sana sio siri, haswa kwenye bando ya wiki yaani wamepandisha sh. 2000 yote kwa 1GB?

Kesho nitanunua line ya HALOTEL japo kwa muda kwani najua ni mtandao mpya so una vibonuses.
 
Naendelea kukuomba msamaha tena kwa kukuudhi. Kujenga hoja sio mchezo kama jeshi linasimama mara kwa mara kukulinda hata kama unachemsha. Kama ni hiyo post yangu ipitie tena uone kama kuna kosa hilo la kiuandishi unalosema. Samahani kaka sintorudia tena kukuudhi.
Hahahahaha wala ujaniudhi kwa lolote kamanda.
 
Vodacom wamepandisha bei ya vifurushi vyao vya internet.... Nimehamia Halotel
 
Back
Top Bottom