Serikali tusimamie wananchi makampuni ya simu yanatuibia kwenye Internet

Serikali tusimamie wananchi makampuni ya simu yanatuibia kwenye Internet

Wa JF.

Watanzania kila kukicha wanazidi kukamaliwa na hawa wawekezaje huku serikali ikiwa upande wa wawekezaji.

Mabenki yanajipangia riba kubwa wanavyotaka wao lakini serikali wala haina tatizo kwenye hilo.

Sasa hivi haya makampuni ya simu yanafanya wizi mkubwa kwa wateja wake kwenye kuuza vifurushi vya Internet sasa hivi Airtel na Vodacom wanafanya wizi wa wazi 1GB unanunua Sh 5000 ya wiki lakini ndani ya siku 3 unaambiwa zimeisha.

Vodacom wao 1GB Sh 8000 ndani ya siku 3 hamna kitu.

Zamani walikuwa wanauza 1GB Sh2500 ikapanda mpaka Sh 3000 kwa wiki.

Serikali tusimamieni Watanzania tunaibiwa na haya makampuni ya simu.

Na hizo MB wanazouza hamna maelekezo ya kodi wanalipa kiasi gani TRA.
Kampuni hizo ni shiida hususani Airtel wamekuwa Wezi hatari
 
Kuna Wizi mkubwa hata wa mda wa maongezi pia serikali inabidi iwambie TCRA wamulike Hilo janga .
 
KWAKWELI HUU NI WIZI MTUPU!
Vodacom kila siku wanakuja na bei kandamizi za vifurushi na natumaini ukihamia 4G yao huto tuvifurushi tutakuwa tunayeyuka kisaniisanii ili mradi kudanganywa 'spidi'!
Kuna haja ya kufufua TTCL itukomboe upande wa internet!
 
Tigo walikuwa heri lkn sasa ndio wezi wakubwa wamewapita hata Voda
 
HIVI KWANINI TTCL IMEPWAYAAA!INASUASUA

OVA
 
Mkuu Kwani unadhani serikali hawajui kuwa makampuni ya simu yanawaibia wananchi?
 
Yaani jamaa wana Uhuru sana wa kujipangia bei.. kila siku wanaweka viwango vipya, mtetezi wetu ni nani kwa hili.!?
Hatuna mtetezi kwa hili maana halijaanza leo,tangy kitambo tumekuwa tukilalamika wee lakini wapi
 
Kila siku nawaambia hamieni halotel muone ilivyo nafuu na huduma bora hamtaki mnaidharau,sh 3999 MB 1536 wiki,sh 5000 MB 2560 wiki,sh 7000 MB 3580 wiki na wala huibiwi kwakua kila unapotumia wanakuletea msg umetumia MB ngapi na zimebaki ngapi,so make changes guys
Kumbe mambo iko huku wacha nihamie sasa
 
Najiuliza waziri wa hii tasnia hapendi kiki jamani achukue waandishi wa habari aende ofis zao
 
Huduma za internet za Tigo gharama zinabadilika badilika mpk kero.

Mwaka jana 2015 mpaka mwaka huu mwezi march 2016 mambo yalikuwa vizuri ila ghafla mambo yamebadilika nachukulia mfano kifurushi cha Tshs 1,000 ambacho mm ndo nanunua kila siku(mara) kimeanzia 1GB mpk sasa ni 350MB mwaka huu huu ndani ya miezi mitano tu.

Kuanzia march
1GB = Tsh 1,000
600MB = Tshs 1,000
600MB + 50mb BONAS = Tshs 1,000
350MB = Tshs 1,000 (sasa hivi)

Ukidownload video au audio MB zinakwisha spidi ya mwendokasi (mabadiliko haya zaidi wiki hizi mbili)

Kifurushi cha watsapp kutoka 1,000 mpk 2,000 kwa mwezi..kifurushi cha Tsh500 ilikuwa 150MB + 30Mb Bonus wiki iliyopita kimebadilika sasa 130MB
 
Hii mijitu ni majambazi ya nchi kavu. ..ife milele. ..
 
Back
Top Bottom