Serikali, tumieni watu wenye vipawa vya ushawishi kutoa elimu kwa watu kabla ya kuchukua maeneo yao

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Ili kuepusha sintofahamu,tafrani na migogoro ya Ardhi isiyokuwa na Tija, Serikali tumieni watu wenye vipawa vya Ushawishi na kuongea Ili watoe Elimu na kujenga ushawishi Kwa watu na kuepusha tafrani.

Ukimsikiliza huyu Jamaa hapa chini anaongea huko Songea mbele ya Wananchi waliochukuliwa maeneo Yao ni wazi Wananchi wameelewa na wameshawishika ndio maana anapigiwa makofi.

Inafaa taasisi zote zijitahidi ku recruit watu wa namna hii Ili wasaidie kuepusha sintofahamu.

Hongera sana mwamba kutoka Songea.

======


JE, WAJUA SONGEA NDIYO BARABARA YA MKATO KWENDA AFRIKA YA KUSINI

Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile Mji wa Songea ni njia ya mkato ya kwenda nchini Afrika ya Kusini hivyo kujengwa kwa barabara ya lami kutoka Songea hadi Mkenda mpakani na Msumbiji kunakwenda kuufungua Mkoa wa Ruvuma kimataifa.

Mheshimiwa Ndile alikuwa anazungumza na wananchi wa Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea ambao wametoa hekari 5000 kwa ajili ya kujenga viwanda vya kisasa hivyo kuwezesha bidhaa zitakazozalishwa kwenye viwanda hivyo kuuzwa nchi za Malawi,Msumbiji na Afrika ya Kusini.
 
Back
Top Bottom