Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,111
- 2,741
Nikiwa katika moja ya Airport zetu nikisubiri kupanda ndege ya Qatar kwenda Uarabuni, nilikutana na kundi la Watalii kama 9 waliokuwa wanarudi kwao Marekani wakiwa na malalamiko mazito sana.
Hawa Watalii walikuwa na hasira isiyo ya kawaida wakilalamikia utendaji kazi wa Serikali ya Tanzania na gharama za kupima Corona. Licha ya kuwa hawa wote walikuwa na change (vaccination) kutoka nchini kwao Marekani, na kadi ya kuonyesha walipewa chanjo walikuwa nazo.
Walipoingia nchini, Walilazimishwa kulipa $100 kila mmoja kwa jailli ya kupima Corona na wala majibu hawakuyaona. Walipokuwa wanarejea makwao, walilazimishwa kukaa siku tatu zaidi Hotelini kusubiria majibu ya Corona nje ya kulipishwa $175 nyingine kila mmoja kwa jailli ya vipimo ili waweze kusafiri.
Mbaya Zaidi, wanne kati yao majibu yao ya kwanza yalirudi wana Corona Virus. Walipo rudi kupima mara ya pili, majibu yakarudi Negative.
Kwa kifupi hawa wageni walikuwa wanajuta kuja kutalii Tanzania, kwa maana usumbufu na gharama kuja Tanzania ni kubwa mno. Nchi nyingi za Magharibi unapokuwa na cheti cha kuonyesha umechanjwa, hakuna usumbufu mwingine. Walichoniuliza, ni kwamba, wanaporudi kwao, wanaenda kuonyesha karatasi la kupimwa kutoka Tanzania, au Chanjo waliyopewa Marekani?
Nadhani ni muda serikali ikaangalia hili swala kwa undani kwa sababu tunachafuka mno. Wale watalii kamwe hawatarudi Tanzania, na hatujui hiyo sumu wataisambaza wapi na kwa nani. Hatuwezi kutajirika kwa hizi vijihela vya $100.
Gharama ya kurekebisha hii uharibifu ni mkubwa mno.