Bando la wiki
JF-Expert Member
- May 23, 2023
- 337
- 914
Yaani kuishi nchi hii ya Tanzania imekuwa nongwa sana, kila eneo wafanyabishara wanajiamlia kufanya yao.
Waendesha daladala wanapakia abilia hadi mlangoni, watu wanasimamiahwa na kupangwa kama magunia ya mikaa.
Kwani serikali hatuwezi kufanya hata hili la usafiri kwa kuzingatia level seat nchi zingine zikaja kujifunza hapa kwetu Tanzania?
Cha kufanya serikali toa tamko kwa nchi nzima hakuna abiria kusimama kwenye chombo cha usafiri hasa daladala maana najua angalau kwenye vyombo vingine vya usafiri wa masafa marefu wanazingatia level seat.
Yaani mimi huwa nashangaa Trafiki wa Tanzania anasimamisha gari ndogo mfano Harrier au Juke nakuanza kuizunguka zunguka kukagua huku akiiacha daladala inampita mbele yake ikiwa imejaza abiria hadi mlangoni na ilhali wakijua hiki ni kichume na sheria za usafirishaji.
Serikali toa tamko kwamba Trafiki ashushe abiria yoyote aliyepanda daladala kwa kusimama, hiyo ndiyo iwe adhabu yake huku konda na dereva walioruhusu abiria kusimamia kwenye gari yao wakipigwa faini ya Tshs 30000.
Hii itasababisha abiria, konda na madereva kuheshimu sheria na usalama barabarani.
Hivi kwa ujazaji wa abiria wakiwa wamesimama hadi milangoni, tulishajiuliza endapo daladala hiyo inapata ajali hivi hao abiria walio simama watakuwa na hali gani? Au ndo kusema serikali itakuja na salam za pole kwa wananchi walioondokewa na wao.
Lakini pia serikali kupitia mkurugenzi wa halmashauri waone umuhimu wa kuwapunguzia tozo haya magari yanatoa huduma za daladala kwa wananchi wa Tanzania kwa sababu inawezekana wanajaza ivyo abiria ili wapate pesa za kulipa kodi za TRA na Tozo za halmashauri.
Lakini pia serikali ione umuhimu wa kupunguza kodi za forodha za uingizaji magari ya abiria ili wawekezaji waingize magari mengi ya abiria kwa ajili ya ku_accomodate the excess supply ya abiria inayochangiwa sana na ukuaji wa miji yetu na uzalianaji mkubwa kunakopelekea uongezekaji mkubwa wa idadi ya watu Tanzania.