Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Sawa Mkuu umeeleweka, but kuna kitu kinaitwa KARMA. Naona hapa juhudi ni kumfilisi Mbowe baada ya kumuona kwamba amekuwa tishio kubwa kwa MACCM kwa miaka mingi sasa pamoja na juhudi kubwa za propaganda chafu dhidi yake CHADEMA na UKAWA pia.
Kwa hiyo mbowe anadaiwa au hadaiwi?Na kama anadaiwa kwa nini halipi?
 
Ukwepaji kodi wa namna yoyote ile haukubaliki, lakini kwa awamu hii hivi wakwepa kodi ni watu wa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha tu? Mbona akina maganga wako wengi wakwepa kodi lakini wanapeta tu?
Kwa hiyo Bakhresa ni mchaga?
 
Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
Siasa mchezo mbaya sana katika nchi zetu za Africa [emoji288]
 
Mbowe anastahili kulipa kodi zote kama mfanyabiashara mwingine.

Huyu na jamaa zake wakipewa nchi ndo mjue nchi imeuzwa. Hizi si dalili njema.

Alipe tu kodi. Asilete mazoea kwenye sheria.
 
Atalipaje wakati mmemdhuluma . BILCANAS ilikuwa na hisa pande mbili upande wa serikali na familia ya Mbowe. Mahakama mmetia mfukoni kisa wanap[ata pesakutoka kwenu

AONYESHE MKATABA HADHARANI . HANA CHA MKATABA, ANGEKUWA NAO ASINGENYAMAZA. MBOWE ANA GAZETI MKATABA HUO TUNGEUONA, LAKINI HANA. WATU WENGI WAMENYAKUWA MAJUMBA YA SERIKALI KWA UJANJA WA KUTUMIA UBIA NA MIKATA UCHWARA AMBAYO HAWAWEZI KUIONYESHA KWASABABU IMEJAA DHURUMA KWA WATANZANIA WENGI, NA ATI HAWA NDIYO WANADAI NI VIONGOZI WETU MUNGU ATUSAIDIE. MIKATABA UCHWARA SIYO KWENYE SERIKALI YA LEO. ALIPE KODI NA TUNATAKA RISITI.
 
Umeona Serikali inawagusa mafisadi wa lugumi, escrow, iptl etc!? Jiulize hawa kwanini hawaguswi!? Wabunge wa MACCM wamepokea milioni 10 kila mmoja kama rushwa ili kupitisha muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini. Je, umesikia aliyetoa rushwa na hao Wabunge kufuatiliwa kama anavyofuatiliwa Mbowe!?

Kuna yule aliyekutwa na nyara za serikali ambaye ni mtoto wa Mbunge wa CCM sijui amefanywaje vile
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tunajenga CIA na pia tunalipia dream liner kama nne hivi in advance. Hivyo ndo vipaumbele vyetu. Mbowe lazima alipe hiyo pesa chap au tupige mnada mali zake. Kugumi, escrow na kadhalika ni makaburi ya zamani mno na hatutayafukua!

Hata zile bilioni nane ni MAKABURI ya zamani hamtayafukua,hili la kusikia kwamba hajalipa miaka mitano wakati hoteli yenyewe haina hata miaka minne ni ajabu na kweli
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Kwahiyo unataka sheria ipindishwe kidogo kumpa favor Mbowe, kama hao wengine ambao hawa lipi kodi?.Mimi nafikiri uwataje hao ambao hawalipi kodi, ili nao wabanwe walipe kodi.
 
Umeona Serikali inawagusa mafisadi wa lugumi, escrow, iptl etc!? Jiulize hawa kwanini hawaguswi!? Wabunge wa MACCM wamepokea milioni 10 kila mmoja kama rushwa ili kupitisha muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini. Je, umesikia aliyetoa rushwa na hao Wabunge kufuatiliwa kama anavyofuatiliwa Mbowe!?
Kwahiyo unataka na Mbowe wam - treat kama Lugumi na hao wengine?
 
Tatizo wanasiasa wengi wako kwenye siasa kama kichaka cha kujifichia, wakiguswa wanatafuta huruma ya wananchi kwamba wanaonewa kwa sababu wako upinzani ila ukweli wengi hawalipi kodi. Mbowe kila sehemu anadaiwa NSSF, NHC,TRA. Serikali iliyopita wapinzani waliinanga sana kwamba ni dhaifu na haikusanyi kodi leo hii inakusanya wanasema wanaonewa utafikiri wao wako juu ya sheria. Mbowe lazima alipe kodi mbona wafanyakazi wanakatwa kodi kila mwezi.
 
Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Wafichue hao wengine. Vinginevyo tutasema ni mbowe tu.
 
Mmh Hays bwana lakin wamemwandama mno

Unapomkosoa mwenzio nawe tegemea kukosolewa.

Ama kweli kikwete alikuwa muungwana. Enzi ya Soviet union, mao, NA hata Nyerere ilikua ikiwa unaikosoa siasa zao chipukizi hata kama wanao wanakushtaki viyuoni.
 
Polisi wamefuta kesi kwa sababu uchunguzi "utachukua muda mrefu" kakutwa na meno ya tembo 600 kama sikosei, kaangamiza Tembo 300![emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]

Kuna yule aliyekutwa na nyara za serikali ambaye ni mtoto wa Mbunge wa CCM sijui amefanywaje vile
 
JANGA JINGINE KWA MBOWE





Na OMARY MLEKWA-HAI

MIEZI takribani mitano tangu aondolewe Bilicanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, jana tena Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 13.5 ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame mkoani Kilimanjaro vinginevyo itafungwa.

Uamuzi huu mpya wa Serikali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analolimiliki Mbowe kutokana na kile alichosema kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.

Takribani miezi mitano iliyopita, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilivamia na kutoa vitu vyote katika jengo maarufu la Bilicanas lililopo Mtaa wa Mkwepu na Makunganya, Dar es Salaam.

Jengo hilo lililovunjwa wiki mbili zilizopita lilidaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Aikael Mbowe ambaye ni baba mzazi wa Freeman Mbowe.

Hata hivyo, NHC ilieleza kuchukua uamuzi huo kutokana na mteja wake (Mbowe) kushindwa kulipa kodi ya pango zaidi ya sh bilioni 1.172 ambayo ni malimbikizo tangu miaka ya 1990.

Ingawa Mbowe mwenyewe amepata kusema kuwa jambo hilo limefanywa kwa sababu za kisiasa, lakini alipolifikisha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, kesi yake ilifutwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.

Alisema hali hiyo imesababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.

Byakanwa alisema Serikali ya awamu ya tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbunge huyo ambaye ni mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo Kijiji cha Nshara, hajawahi kulipa kodi ya huduma licha ya kuandikiwa barua Januri 21, 2016 ya kumtaka kulipa kodi hiyo ambayo hakuijibu.

“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi.

“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.

Alisema deni hilo lilipwe ndani ya siku 14 na akishindwa atachukua hatua ikiwa ni pamoja na kufunga biashara.

“Ikiwezekana tufafunga biashara hii, kwa kuwa amekuwa na tabia ya kutokujali kama nilivyomwita ofisini kwangu na hakufika na wala kujibu barua, sasa na hili puuzeni tutachukua hatua,” alisema Byakanwa.

“Mnaweza kusema kuwa DC labda anamwonea, mimi nakwenda na vielelezo na hapa pia nina taarifa nyingine kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa hajapeleka taarifa ya mauzo ili aweze kukadiriwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Hai, David Mlay.

Gazeti hili jana lilimtafuta Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, lakini hakupatikana.

Jana hiyo hiyo MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na dada wa Mbowe aitwae Neel Mbowe, anayesimamia shamba la Veggies, ambaye alisema nyaraka na taratibu zote za umiliki wa shamba hilo anazo kaka yake huyo.

Kuhusu umiliki wa shamba hilo, Neel alisema lilikuwa likimilikiwa na babu yao tangu mwaka 1940 na baadae akampa baba yao, marehemu Aikael Mbowe.

Kwa mujibu wa Neel, walimua kulima katika eneo hilo ambalo lilikuwa pori kwa muda mrefu ili kuongeza ajira kwa vijana wanaolizunguka.

Kuhusu sheria ya mazingira na umiliki wa shamba hilo, alisema anayejua yote hayo ni kaka yake Mbowe.

Juzi Byakanwa alitoa amri ya kusitisha shughuli za kilimo katika shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara.

Byakanwa alimshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.

“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (juzi) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.

“Pia naliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hili na kuchukua hatua pamoja na kuniletea taarifa walizochukua. Maofisa maliasili wa wilaya wafanye tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14,” alikaririwa Byakanwa.
Mbowe anatakiwa kutii sheria bila shuruti.Alipe kodi na asiharibu mazingira,hakuna mtu atakae msumbua.
 
Tukiweka mbali mambo ya kisiasa, Mbowe anastahili kulipa kodi kama kiongozi ili kuonesha mfano kwa jamii. Pia alitakiwa kufata taratibu zote za mazingira kabla ya kuendelea na shughuli za kilimo kwenye shamba husika. Lakini naamini kama rekodi zake ziko sahii hapo ni porojo tu.
Cha kujiuliza miaka yote chama gani kilikuwa kinatawala?
Mbowe ameonekana hafai sasa hivi?
Mbona magufuli alipokwenda kufungua barabara akiwa waziri alimsifia sana au ulikuwa unafiki?
Jengo la Billicanas amelikarabati kwa makubaliano ya NHC baada ya huyu jamaa kuingia ikulu ndiyo inaonekana anadaiwa?
Miaka yote walikuwa wapi? Au ndiyo wanatafuta umaarufu kupitia kwa Mbowe?
Njia rahisi ya kuonyesha kuwa anaonewa ni kutoa vielelezo kuonyesha uthibitisho wa alivyolipa hizo kodi.

Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?

Alipe kodi tu. Maendeleo hayawezi kuja kama watu hawalipi kodi.

Hongera Mh. Rais kwa kupambana na wakwepa kodi. Tunaendelea kukuombea ili ushinde hii vita.

Hapa hakuna kuangalia sura ya mtu
Mbowe ni mtanzania kama watanzania wengine
Lazima afuate utaratibu na sheria za nchi kama raia wengine.
Kulipa kodi ni lazima
Kukwepa kulipa kodi ni kosa kubwa
Nchi nyingine hawezi kuwa kiongozi kabisa.

Kama unadhani mbowe mkubwa
Mkubwa CDM
Sisi lazima afuate sheria.

Unapo kosoa na kuwa mpinzani
Inakupasa uanze kujisafisha wewe
Mbowe anajua kukosoa wenzie kumbe yeye ni mchafu zaidi
 
Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
Ndiyo maana walitaka tulips sisi kwa kuongeza bei
 
Back
Top Bottom