Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Nimeongea kama Mtanzania ambaye ana uhuru wa kikatiba wa kutoa maoni yake hadharani. LOL! Kila mmoja ataguswa kwa wakati wake! Utasubiri sana kuona mafisadi wa lugumi, escrow etc na Wabunge wapiga madili wakiguswa umesahau kauli ya "sifukui makaburi ya zamani" na makaburi ya zamani yote yanawahusu MACCM.


Kila mmoja ataguswa kwa wakati wake na kama unadhani mbowe anaonewa nenda mahakamani ukamsaidie.Mbona mbowe mwwnyewe yuko kimya weee kimekuuma nini?
 
Serikali inadaiwa na shirika la nyumba NHC, TANESCO,Mifuko ya hifadhi za jamii, Mabenki ya ndani, Walim, Mgodi wa Mwadui trion 24, lakini sioni juhudi za wao kuandamwa kila siku, hivi Tanzania hii kuna wakwepa kodi kuzidi hao makada watiifu kwa CCM? Au mambo mengine yanafanywa ili watu wapate kiki? Kama shamba ni la kwao mbowe toka mwaka 1940 huko ina maana serikali ya MWL.NYERERE haikuona uharibifu huo, ya Mwinyi haikuona, ya Mkapa haikuona ya Kikwete haikuona leo hii ya Magufuli ndo serikali makini imeona sio, hivi kweli kati ya serikali ya MWL. NYERERE na serikali ya Magufuli ipi iliongozwa na watu makini na wazalendo wa taifa?
Huu ni mchezo mchafu, na kama taarifa ilitolewa na watafiti kutoka mkoani inakuwaje MKUU wa mkoa ashindwe kuifuatilia taarifa hiyo ilihali na yeye yupo hapo mkoani hadi taarifa hiyo ije kufuatiliwa na MKUU wa wilaya?

Pambaneni na matajiri tuuone mwisho wenu ila kwa nchi yetu ilivyo hadi sasa unapopambana na tajiri mmoja unaumiza walalahoi 200 na familia zao.
 
MARASTAFARIAN WANA USEMI WAO KUWA "JELOUS PEOPLE WILL NEVER WIN"

OVA
Serikali inadaiwa na shirika la nyumba NHC, TANESCO,Mifuko ya hifadhi za jamii, Mabenki ya ndani, Walim, Mgodi wa Mwadui trion 24, lakini sioni juhudi za wao kuandamwa kila siku, hivi Tanzania hii kuna wakwepa kodi kuzidi hao makada watiifu kwa CCM? Au mambo mengine yanafanywa ili watu wapate kiki? Kama shamba ni la kwao mbowe toka mwaka 1940 huko ina maana serikali ya MWL.NYERERE haikuona uharibifu huo, ya Mwinyi haikuona, ya Mkapa haikuona ya Kikwete haikuona leo hii ya Magufuli ndo serikali makini imeona sio, hivi kweli kati ya serikali ya MWL. NYERERE na serikali ya Magufuli ipi iliongozwa na watu makini na wazalendo wa taifa?
Huu ni mchezo mchafu, na kama taarifa ilitolewa na watafiti kutoka mkoani inakuwaje MKUU wa mkoa ashindwe kuifuatilia taarifa hiyo ilihali na yeye yupo hapo mkoani hadi taarifa hiyo ije kufuatiliwa na MKUU wa wilaya?

Pambaneni na matajiri tuuone mwisho wenu ila kwa nchi yetu ilivyo hadi sasa unapopambana na tajiri mmoja unaumiza walalahoi 200 na familia zao.
 
Kama taifa tukisema tuanzishe oparesheni ya wakwepa kodi, yawezekana Mbowe akawa wa mbali sana asijadiliwe kabisa. Lakini tumefikaje hapa? Hakuna chuki ya kisiasa naomba majibu?
Wameamua kufuata zile siasa za kihuni za kukomoana.
 
Ndiyo maana yake Mkuu mafisadi akina Lugumi & Co waliochota 57 billion hawaguswi!, Wale wa Escrow waliochota 321 billion za Tanesco akina Rugemarila & Co na kugawa rushwa hadi ndani Ikulu kwa kutumia mifuko ya Rambo na ndoo za sandarusi hawaguswi, Wabunge waliopokea rushwa ya milioni 10 kila mmoja kama ahsante yao ya kupitisha muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini hawaguswi lakini Mbowe ndiye amekuwa mhalifu nambari one nchini ukilinganisha na wezi na mafisadi akina lugumi 37 billion, escrow 321 billion, wakwapuzi wa pesa za wahanga 16 billion.

Wameamua kufuata zile siasa za kihuni za kukomoana.
 
Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
Kwa hiyo ndio sababu Mbowe asidaiwe kulipa kodi?
 
JANGA JINGINE KWA MBOWE





Na OMARY MLEKWA-HAI

MIEZI takribani mitano tangu aondolewe Bilicanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, jana tena Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 13.5 ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame mkoani Kilimanjaro vinginevyo itafungwa.

Uamuzi huu mpya wa Serikali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analolimiliki Mbowe kutokana na kile alichosema kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.

Takribani miezi mitano iliyopita, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilivamia na kutoa vitu vyote katika jengo maarufu la Bilicanas lililopo Mtaa wa Mkwepu na Makunganya, Dar es Salaam.

Jengo hilo lililovunjwa wiki mbili zilizopita lilidaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Aikael Mbowe ambaye ni baba mzazi wa Freeman Mbowe.

Hata hivyo, NHC ilieleza kuchukua uamuzi huo kutokana na mteja wake (Mbowe) kushindwa kulipa kodi ya pango zaidi ya sh bilioni 1.172 ambayo ni malimbikizo tangu miaka ya 1990.

Ingawa Mbowe mwenyewe amepata kusema kuwa jambo hilo limefanywa kwa sababu za kisiasa, lakini alipolifikisha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, kesi yake ilifutwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.

Alisema hali hiyo imesababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.

Byakanwa alisema Serikali ya awamu ya tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbunge huyo ambaye ni mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo Kijiji cha Nshara, hajawahi kulipa kodi ya huduma licha ya kuandikiwa barua Januri 21, 2016 ya kumtaka kulipa kodi hiyo ambayo hakuijibu.

“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi.

“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.

Alisema deni hilo lilipwe ndani ya siku 14 na akishindwa atachukua hatua ikiwa ni pamoja na kufunga biashara.

“Ikiwezekana tufafunga biashara hii, kwa kuwa amekuwa na tabia ya kutokujali kama nilivyomwita ofisini kwangu na hakufika na wala kujibu barua, sasa na hili puuzeni tutachukua hatua,” alisema Byakanwa.

“Mnaweza kusema kuwa DC labda anamwonea, mimi nakwenda na vielelezo na hapa pia nina taarifa nyingine kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa hajapeleka taarifa ya mauzo ili aweze kukadiriwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Hai, David Mlay.

Gazeti hili jana lilimtafuta Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, lakini hakupatikana.

Jana hiyo hiyo MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na dada wa Mbowe aitwae Neel Mbowe, anayesimamia shamba la Veggies, ambaye alisema nyaraka na taratibu zote za umiliki wa shamba hilo anazo kaka yake huyo.

Kuhusu umiliki wa shamba hilo, Neel alisema lilikuwa likimilikiwa na babu yao tangu mwaka 1940 na baadae akampa baba yao, marehemu Aikael Mbowe.

Kwa mujibu wa Neel, walimua kulima katika eneo hilo ambalo lilikuwa pori kwa muda mrefu ili kuongeza ajira kwa vijana wanaolizunguka.

Kuhusu sheria ya mazingira na umiliki wa shamba hilo, alisema anayejua yote hayo ni kaka yake Mbowe.

Juzi Byakanwa alitoa amri ya kusitisha shughuli za kilimo katika shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara.

Byakanwa alimshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.

“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (juzi) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.

“Pia naliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hili na kuchukua hatua pamoja na kuniletea taarifa walizochukua. Maofisa maliasili wa wilaya wafanye tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14,” alikaririwa Byakanwa.
Always the hunter becomes the hunted.
 
Hv ni mbowe tu ndio mwenye hotel na shamba au ni viongozi wote na waupande ule? Nimeuliza tu jamani
 
Yeah! I know but when it comes to Lugumi, Escrow etc we don't see the same efforts. The Government is MIA.

Always the hunter becomes the hunted.
 
Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Wacha wamwandame yeye si ndio anakwepa kodi kwa miaka mingi zaidi, imagine NHC ni kiasi gani then anakuja kudanganya watu humu, hata Jambazi Sugu alilowauzia Chadema kwenye gunia nalo ni lake. Crime doesn't pay.
 
Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
Kwa hiyo, unadhani kwa sababu ya deni serikali inadaiwa na Tanesco, basi Mbowe aachwe asilipe kodi, mpaka serikali iilipe Tanesco sio?
 
Simtetei Mbowe kama anadaiwa alipe kodi..

Lakini namshangaa mkusanya kodi kuvunja sheria za nchi kwa matumizi ya kodi zetu na yeye kutolipa kodi......

Hivi unatoa wapi moral authority ya kumwambia mtu alipe kodi wakati wewe si mlipa kodi?......

Hiyo ndio Tanzania mpya bwana watu walipe kodi lakini sheria za kusimamia kodi zikiukwe .....


Tuchukue pesa za kodi tumpe mtoto Wa shangazi ajenge majengo chato bila tenda kutangazwa wala bunge kupitisha hizo pesa.......

Irrelevant, ulitaka akajenge uwanja kwenu? Mbona mifano ipo mingi tu JK aliamua kujenga Bandari Bagamoyo. Wacha JPM ajenge kwao. Yaani Chato kusiwe na uwanja wa ndege kisa kuna jamaa JF anatumia jina la bandia la technically hapendi, what stupidity is that!
 
Unapokusanya kati ya 1.1 trilioni mpaka 1.4 trillion kwa mwezi kamwe huwezi kushindwa kulipa deni la 125 billion tena kwa mkupuo mmoja kama una nia ya kufanya hivyo.
Hawawezi!

Mapato ya serikali kwa mwezi anayotokana na kodi ni karibia nusu ya matumizi yetu kwa mwezi!!
 
Back
Top Bottom