Sasa Mkuu hiii inahalisha kwamba Mbowe asilipe kodi kama anadaiwa? Mimi naamini Kiongozi wa upinzani ni kama mke wa Kaisari (hata kuhisiwa ni kosa!). Sidhani kwa Kiongozi kama Mbowe atakuwa na moral standing ya kusimama na kukemea madudu wafanyayo wengine kama na yeye anafanya hayo hayo. Ni kanuni za uongozi. Ujinga hauhalalishi ujinga. Wizi hauhalalishi wizi.
Kipindi cha nyuma wengi tulijisahau kwa kweli. Na kipindi hiki cha Magufuli watu tutapata wakati mgumu. Huwezi kusema eti serikali inakuonea wakati ni kweli inakudai! cha msingi lipa deni la watu malizana nao. Dawa ya deni ni kulilipa si vinginevyo. Ya Lugumi na mengineyo yana mda wake.