Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Serikali na unyanyasaji kwa Mbowe

Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.

Huenda mbowe alikuwa anamtuma mfanyakaz wake wa ndani akalipe kodi halafu huyo mfanyakaz akawa anakula kodi. Dah
 
mnapiga domo tu hapa, mpelekeni mahakamani kwanini mnakimbilia kuomba huruma ya wananchi?

ndomaana serikali inakosa pesa sababu ya kesi za kijinga, mnaishia kuwatajirisha hawa wana siasa.

ingekua kweli msemayo hahahaahaaaa mkuu angetoka magogoni kwenda kumkamata mbowe personally
 
Watetezi wa wakwepa kodi hii nchi ina watu wa ajabu , wanaohalalisha kosa kwa kosa ,

Kwanza wamemuona huruma kosa la kukwepa kodi ni kufungwa

Mbona sisi tunalipa kodi na mambo yanaenda ,tukubali mambo yamebadilika jamani
 
Kama taifa tukisema tuanzishe oparesheni ya wakwepa kodi, yawezekana Mbowe akawa wa mbali sana asijadiliwe kabisa. Lakini tumefikaje hapa? Hakuna chuki ya kisiasa naomba majibu?
Ukwepaji kodi wa namna yoyote ile haukubaliki, lakini kwa awamu hii hivi wakwepa kodi ni watu wa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha tu? Mbona akina maganga wako wengi wakwepa kodi lakini wanapeta tu?
 
Huyu mkuu wa wilaya ya hao, ni mnoma, kaza baba hawa jamaa wanafikiri nchi hii ni ya kuvunavuna tu, wamevuna we, wakaona kumbe pia tuwaweza kwenda kula ikulu ee,
Kama kweli Mbowe anadaiwa kodi, kiasi kilichotajwa kwa miaka mitano ni tone la maji kwenye bahari ya Lugumi, lakini Lugumi wanapeta tu.
 
Kwenye shutuma kwamba eti shamba lipo kwenye vyanzo vya mto weruweru, mkuu wa wilaya katumwa tu kutekeleza amri ya wakubwa. Nijuavyo mimi kijiji cha Nshara kiko karibu na barabara kuu ya Arusha-Moshi, huku chanzo cha mto weruweru kikiwa kwenye maporomoko ya mlima kilimanjaro zaidi ya km 30 toka Nshara.
 
JANGA JINGINE KWA MBOWE





Na OMARY MLEKWA-HAI

MIEZI takribani mitano tangu aondolewe Bilicanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, jana tena Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 13.5 ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame mkoani Kilimanjaro vinginevyo itafungwa.

Uamuzi huu mpya wa Serikali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analolimiliki Mbowe kutokana na kile alichosema kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.

Takribani miezi mitano iliyopita, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilivamia na kutoa vitu vyote katika jengo maarufu la Bilicanas lililopo Mtaa wa Mkwepu na Makunganya, Dar es Salaam.

Jengo hilo lililovunjwa wiki mbili zilizopita lilidaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Aikael Mbowe ambaye ni baba mzazi wa Freeman Mbowe.

Hata hivyo, NHC ilieleza kuchukua uamuzi huo kutokana na mteja wake (Mbowe) kushindwa kulipa kodi ya pango zaidi ya sh bilioni 1.172 ambayo ni malimbikizo tangu miaka ya 1990.

Ingawa Mbowe mwenyewe amepata kusema kuwa jambo hilo limefanywa kwa sababu za kisiasa, lakini alipolifikisha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, kesi yake ilifutwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.

Alisema hali hiyo imesababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.

Byakanwa alisema Serikali ya awamu ya tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbunge huyo ambaye ni mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo Kijiji cha Nshara, hajawahi kulipa kodi ya huduma licha ya kuandikiwa barua Januri 21, 2016 ya kumtaka kulipa kodi hiyo ambayo hakuijibu.

“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi.

“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.

Alisema deni hilo lilipwe ndani ya siku 14 na akishindwa atachukua hatua ikiwa ni pamoja na kufunga biashara.

“Ikiwezekana tufafunga biashara hii, kwa kuwa amekuwa na tabia ya kutokujali kama nilivyomwita ofisini kwangu na hakufika na wala kujibu barua, sasa na hili puuzeni tutachukua hatua,” alisema Byakanwa.

“Mnaweza kusema kuwa DC labda anamwonea, mimi nakwenda na vielelezo na hapa pia nina taarifa nyingine kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa hajapeleka taarifa ya mauzo ili aweze kukadiriwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Hai, David Mlay.

Gazeti hili jana lilimtafuta Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, lakini hakupatikana.

Jana hiyo hiyo MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na dada wa Mbowe aitwae Neel Mbowe, anayesimamia shamba la Veggies, ambaye alisema nyaraka na taratibu zote za umiliki wa shamba hilo anazo kaka yake huyo.

Kuhusu umiliki wa shamba hilo, Neel alisema lilikuwa likimilikiwa na babu yao tangu mwaka 1940 na baadae akampa baba yao, marehemu Aikael Mbowe.

Kwa mujibu wa Neel, walimua kulima katika eneo hilo ambalo lilikuwa pori kwa muda mrefu ili kuongeza ajira kwa vijana wanaolizunguka.

Kuhusu sheria ya mazingira na umiliki wa shamba hilo, alisema anayejua yote hayo ni kaka yake Mbowe.

Juzi Byakanwa alitoa amri ya kusitisha shughuli za kilimo katika shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara.

Byakanwa alimshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.

“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (juzi) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.

“Pia naliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hili na kuchukua hatua pamoja na kuniletea taarifa walizochukua. Maofisa maliasili wa wilaya wafanye tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14,” alikaririwa Byakanwa.


mkuu mwisho wa siku mbowe alipe kodi au asilipe hizo fedha ni zake yeye na familia yake na ukoo wake sasa wewe kazana kumtetea mtu ambaye hakupi hata shillingi tano....

all in all utaumiza kichwa chako hapa bureee kubishana na watu ila kaa ukijua kuwa wanasiasa wote lao huwa ni moja na ni walaghai wakubwa wakitutumia wananchi kutafuta huruma huku familia zao zinaendelea kuneemeka kupitia sisi
 
Kutetea haki ifanyike katika sheria za nchi si mpaka ulipwe iwe shilingi tano au million/billion bali ni haki ya kila Mtanzania kutoa maoni yake hadharani pale ambapo anaona sheria za nchi zinapindishwa. Na hapa ni JF where we dare to talk openly kuhusu mustakabali wa nchi katika mambo mbali mbali hivyo haihusu kitu eti mpaka ulipwe ndiyo uje hapa kujadili.

Sheria za nchi ni kama msumeno zinatakiwa zikate pande zote bila visingizio vya aina yoyote ile. Na kwa taarifa yako kichwa change kiko bomba hakijawahi kuumia hata siku moja katima mjadala wowote ambao niliwahi kushiriki humu.

mkuu mwisho wa siku mbowe alipe kodi au asilipe hizo fedha ni zake yeye na familia yake na ukoo wake sasa wewe kazana kumtetea mtu ambaye hakupi hata shillingi tano....

all in all utaumiza kichwa chako hapa bureee kubishana na watu ila kaa ukijua kuwa wanasiasa wote lao huwa ni moja na ni walaghai wakubwa wakitutumia wananchi kutafuta huruma huku familia zao zinaendelea kuneemeka kupitia sisi
 
Hata kukwepa kodi ni kuiba, kwa hiyo huyu.ni mwizi analiibia taifa na hana dalili za kubadilika.

Huyu ni sugu, historia inasomeka hivo


Na angefanikiwa Lowassa angechukuwa urais, Mbowe alikuwa ameukata na mali ya Watanzania, jengo lilikuwa linatoweka. Mungu ni mkubwa amempiga full stop. Alipe kodi kama Watanzania wengine. Wengi walikuwa wakitajirika kwa deals, sasa waliokuwa na biashara za bila deals wataendelea, waliokuwa wanapiga deals na kuwaibia wengi wataporomoka. Kweli Mbowe alikuwa sugu na ni mwizi wa kutumia njia ya ujanja.
 
Dah huruma inanijia kwa waliopo hilo shamba ukisikia eka 2 ni eneo dogo sana ila kwa Mbowe pana green house eneo lote na anazalisha mazao kama nyanya,hoho etc na anauza nnje ,kwa anaejua green house utaelewa na kuona eka mbili ilivyo eneo kubwa na limekula kiasi gani cha pesa je toka linaanza hawakuliona hilo !!?? Usiasa pembeni ila hii ni kumfilisi mtu nawafahamu watu ambao wameajiliwa hapo ndio wanakosa ajira tena wapo wataalam wengi sana wa kada ya kilimo achana mbali na vibarua sababu pale ni as kampuni kuna mpaka uongozi wake binafsi ,makampuni mengi ya madawa na mbolea huwa yanaenda pale kuuza bidhaa zao ila sasa dah pole yao wengi twamuona Mbowe ila kuna watu zaidi ya mia mbili wanaumia kwa hili

Huruma isikuijie, Mbowe ni mmojawapo amesababisha shida nyingi za Watanzania wa kawaida. Mali ya wengi anatumia kwa manufaa yake mwenyewe bila ya haya. Mbowe lazima afuate sheria kama Watanzania wengine. Hakuna Mtanzania bora kushinda mwingine. Mbowe alipe kodi, afuate sheria. Siasa za uchwara za kujitajilisha ziishe.
 
Kwahyo na mbowe naye risiti za malipo amepoteza?


Sasa ni serikali mpya mtindo mpya wa haki. Maswali ya Epa na Escrow ayaelekeze kwa Kikwete na Mkapa. Serikali ya Magufuli ni serikali ya watu, waliofanya makosa zamani watabeba misalaba yao na sio Rais Magufuli atawabebea. Mbowe sio serikali, lazima alipe kodi hayuko juu ya sheria. Hii kusema mbona serikali inadaiwa hii na hiyo ni ubishi hauna maana. Mbowe siyo serikali, alipe kodi ama afilisiwe. Siasa bila siasa
 
Mwenyekiti Mbowe inabidi awe anaweka utaratibu wa kujibu hizi 'spin' zinazojitokeza bila kuchelewa.. Watanzania wengi wanaamini sana habari za kuandikwa hata kama si za kweli.. Kama hatazijibu binafsi basi hata Afisa Habari wa CHADEMA.
Kwa hali ilivyo inabidi kujiweka salama kama vita iliyotukuka inahitaji kupiganiwa..
 
Ni sawa kuwa kodi inapaswa kulipwa na wafanyabiashara wote.

Ila kwa mtu mwenye akili lazima utajiuliza yafuatayo:~

■ Serikali zilizopita hazikuona hayo makosa mfano kulima karibu na chanzo cha maji?

Kuvuta maji mtoni kwaajili ya umwagiliaji kuna tatizo gani? Na ni yeye peke yake anayevuta hayo maji?

Na kulikuwa na conditions alizowekewa akakiuka?

■ Hiyo kodi ya Mil. 13 ndio inayokwamisha utimizaji wa ilani ya CCM?

■ JE , ni Mbowe pekee ndiye anayedaiwa kodi? Mbona ameandamwa sana na kuunganishiwa makosa mfululizo?


INASHANGAZA KWAKWELI.


Mbowe ni mdaiwa sugu, hadaiwi milion 13 tu. anadaiwa na kodi ya nyumba billion 1.3. Mbowe ni kiongozi anatakiwa aonyeshe mufano. Serikali zilizopita zilikuwa na mtindo wa kufumbia macho wezi, lakini serikali ya Rais Magufuli ni serikali ya watu wote na siiyo ya watu wachache waliokuwa wakiachiwa huru kudhurumu walio wengi. Sio viongozi wote walikuwa wakiunga mkono uongozi uliyopita wakufumbia wakwepa kodi na mafisadi. Mtu mwenye akili lazima aishukuru serikali hii ya sasa kwa kufanya kazi yake ya kuwataka watu walipe kodi na sio kufananisha na ubovu wa serikali zilizopita. Usisahau Mbowe ni kiongozi anatakiwa aonyeshe mfano, lakini badala yake ni mkwepa kodi sugu. Alipe kodi na aishi kama kiongozi sio crook, hawezi kuwa vyote. Tunataka risiti.
 
Umeona Serikali inawagusa mafisadi wa lugumi, escrow, iptl etc!? Jiulize hawa kwanini hawaguswi!? Wabunge wa MACCM wamepokea milioni 10 kila mmoja kama rushwa ili kupitisha muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini. Je, umesikia aliyetoa rushwa na hao Wabunge kufuatiliwa kama anavyofuatiliwa Mbowe!?
Weka ushahidi la sivyo utakua unaeneza propaganda za ufipa
 
Mbowe Kama Kiongozi kudaiwa kila kona Si mfano mzuri kumbe Ni mkwepa kodi mzoefu?! Kisha Ni muharibifu WA mazingira. Atawezaje kuikosoa serikali akiwa Na hali hii ?
Una ushahidi au unaropoka tu. Kosa la kukwepa kulipa kodi la kumburuza mtu mahakamani na si kumpa siku
 
Mbowe ni mdaiwa sugu, hadaiwi milion 13 tu. anadaiwa na kodi ya nyumba billion 1.3. Mbowe ni kiongozi anatakiwa aonyeshe mufano. Serikali zilizopita zilikuwa na mtindo wa kufumbia macho wezi, lakini serikali ya Rais Magufuli ni serikali ya watu wote na siiyo ya watu wachache waliokuwa wakiachiwa huru kudhurumu walio wengi. Sio viongozi wote walikuwa wakiunga mkono uongozi uliyopita wakufumbia wakwepa kodi na mafisadi. Mtu mwenye akili lazima aishukuru serikali hii ya sasa kwa kufanya kazi yake ya kuwataka watu walipe kodi na sio kufananisha na ubovu wa serikali zilizopita. Usisahau Mbowe ni kiongozi anatakiwa aonyeshe mfano, lakini badala yake ni mkwepa kodi sugu. Alipe kodi na aishi kama kiongozi sio crook, hawezi kuwa vyote. Tunataka risiti.
zile taasisi nyingine zilizokuwa zinadaiwa kodi pale jengo la NHIC DSM mrejesho wake ukoje?
 
Mwenyekiti Mbowe inabidi awe anaweka utaratibu wa kujibu hizi 'spin' zinazojitokeza bila kuchelewa.. Watanzania wengi wanaamini sana habari za kuandikwa hata kama si za kweli.. Kama hatazijibu binafsi basi hata Afisa Habari wa CHADEMA.
Kwa hali ilivyo inabidi kujiweka salama kama vita iliyotukuka inahitaji kupiganiwa..

Hana la kujibu. Kwanza alisema Jengo alilokuwa akifanyia biashara zake ni lake na anamkataba, mpaka Leo hajauonyesha mukataba huo. Kesi ameshindwa na sidhani kama amelipa chochote. Hakuna kiongozi kwenye nchi yeyote yenye uongozi mzuri, ambae hawezi kuyamudu madeni yake, tena madeni ya serikali na akaendelea kuwa kiongozi ni Tanzania pekee. Kiongozi lazima aishi kufuatana na pato lake, ukiona kiongozi anaishi zaidi ya pato lake, huyu ni kiongozi hatari, haaminiki na tafasiri yake ni mwizi.
 
Haya mkwere legelege xaxa kaja strong strong siye yetu macho ngoja move iyendelee !
 
Billion 1.3 za Watanzania sidhani kama amelipa chochote
Atalipaje wakati mmemdhuluma . BILCANAS ilikuwa na hisa pande mbili upande wa serikali na familia ya Mbowe. Mahakama mmetia mfukoni kisa wanap[ata pesakutoka kwenu
 
Back
Top Bottom