Hapana inawezekana kabisa Mkuu! Mbona imewezekana kununua ndege kwa cash kwa trilioni moja!? Sasa kama imewezekana kulipa trilioni moja kununua ndege iweje washindwe kulipa deni la TANESCO la 125 billion!? Hawana nia ya kulipa deni hilo pamoja na kujua fika kwamba hali ya fedha katika shirika hilo ni mbaya sana. Labda uniambie hii tuliyoambiwa kwamba ndege zimenunuliwa kwa cash nao ulikuwa ni uongo mwingine uliotukuka.
Ikiwa ni kweli anadaiwa, lazima alipe kodi ila hapa najaribu kuwaza tu kwa sauti, huyu DC aliemkalia kooni kuhusu kodi kwani mamlaka husika haipo katika kulisema hilo? Hapa napata ukakasi mbona
Hapana inawezekana kabisa Mkuu! Mbona imewezekana kununua ndege kwa cash kwa trilioni moja!? Sasa kama imewezekana kulipa trilioni moja kununua ndege iweje washindwe kulipa deni la TANESCO la 125 billion!? Hawana nia ya kulipa deni hilo pamoja na kujua fika kwamba hali ya fedha katika shirika hilo ni mbaya sana. Labda uniambie hii tuliyoambiwa kwamba ndege zimenunuliwa kwa cash nao ulikuwa ni uongo mwingine uliotukuka.
Hata ningekuwa mimi nisingelipa hilo deni kwa sababu kulipa deni ni lazima ujiridhishe kwanza wewe mwenyewe (ie Mlipaji), kwa nini unalilipa na unamlipa nani, kwa sababu gani etc. JPM anapotoa cash kununua ndege amejiridhisha kwamba huo ndio uamuzi sahihi kwa hivi sasa. Hizi pesa za kulipa kwa kukurupuka hazipo na hana mpango huo. Ni sawa na wafanyakazi hewa, JPM yupo vizuri sana tutakula machungwa huko mbeleni.
kila mtu lazimaalipe kodi ila ingekuja jambo jema kama watu wote wangefuatiliwa kama mbowe anavyofuatiliwa kwe swala la kodi kinyume na hapo itakua ni unafiki tu na siasa za majitaka..eti halmashauri imeshndwa kufikia malengo kwasababu ya den la mbowela sh mil 13? huu ni uongo ambao hata shetani ataushangaa
Ndiyo maana yake Mkuu mafisadi akina Lugumi & Co waliochota 57 billion hawaguswi!, Wale wa Escrow waliochota 321 billion za Tanesco akina Rugemarila & Co na kugawa rushwa hadi ndani Ikulu kwa kutumia mifuko ya Rambo na ndoo za sandarusi hawaguswi, Wabunge waliopokea rushwa ya milioni 10 kila mmoja kama ahsante yao ya kupitisha muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini hawaguswi lakini Mbowe ndiye amekuwa mhalifu nambari one nchini ukilinganisha na wezi na mafisadi akina lugumi 37 billion, escrow 321 billion, wakwapuzi wa pesa za wahanga 16 billion.
Yaani pamoja na kukipora chama chake ushindi naye akasamehe kuepusha umwagaji wa dam haya ndiyo malipo wanayomlipa.,ama kweli ccm sio watu ni majini yaliyotumwa dam za watanzania.
Unapokusanya kati ya 1.1 trilioni mpaka 1.4 trillion kwa mwezi kamwe huwezi kushindwa kulipa deni la 125 billion tena kwa mkupuo mmoja kama una nia ya kufanya hivyo.
Tunajenga CIA na pia tunalipia dream liner kama nne hivi in advance. Hivyo ndo vipaumbele vyetu. Mbowe lazima alipe hiyo pesa chap au tupige mnada mali zake. Kugumi, escrow na kadhalika ni makaburi ya zamani mno na hatutayafukua!
Ndiyo nchi yetu ilipofikia Mkuu. Hakuna anayetaka kuona Mbowe halipi kodi lakini wasiolipa kodi wapo wengi sana ndani ya MACCM pia. Mafisadi wa Lugumi, escrow wapo pia ndani ya MACCM lakini hakuna juhudi za kuwafuatilia hawa kama tunavyoona juhudi za kumfuatilia Mbowe. Tusingehoji juhudi za kumfuatilia Mbowe na ulipaji wa kodi kama pia tungeona juhudi hizi zinafanywa pia ndani ya MACCM na pia kuwagusa mafisadi akina Lugumi, na wale wote wahusika wa Escrow ambao wamechota mapesa chungu nzima ya walipa kodi. Cha kushangaza utasikia "sifukui makaburi ya zamani".
Yaani pamoja na kukipora chama chake ushindi naye akasamehe kuepusha umwagaji wa dam haya ndiyo malipo wanayomlipa.,ama kweli ccm sio watu ni majini yaliyotumwa dam za watanzania.
Kama taifa tukisema tuanzishe oparesheni ya wakwepa kodi, yawezekana Mbowe akawa wa mbali sana asijadiliwe kabisa. Lakini tumefikaje hapa? Hakuna chuki ya kisiasa naomba majibu?
Sawa Mkuu umeeleweka, but kuna kitu kinaitwa KARMA. Naona hapa juhudi ni kumfilisi Mbowe baada ya kumuona kwamba amekuwa tishio kubwa kwa MACCM kwa miaka mingi sasa pamoja na juhudi kubwa za propaganda chafu dhidi yake CHADEMA na UKAWA pia.
Tunajenga CIA na pia tunalipia dream liner kama nne hivi in advance. Hivyo ndo vipaumbele vyetu. Mbowe lazima alipe hiyo pesa chap au tupige mnada mali zake. Lugumi, escrow na kadhalika ni makaburi ya zamani mno na hatutayafukua!
Mfumo wa ulipaji kodi ulikuwa wa hovyo hovyo Sana, inawezekana kodi jamaa analipa lakini wajanja kumbukumbu walikuwa wanapoteza, hilo pia liangaliwe ili tusiumizane sana hii ni nchi yetu sote.
itabidi atoe vielelezo vyake, maana najua kampuni zote ni lazima wanakuwa na documents za kuonyesha kodi wanayolipa! hvyo mbowe itabidi aonyeshe hzo documents kama kweli alikuwa akilipa kodi
Naamini Mbowe kama mwananchi mwingine yeyote anapaswa alipe kodi.
Lakini hivi awamu hii ambaye halipi kodi ni mbowe tu!!? Kuna ulazima wa kumuandama kiasi hiko!?
Serikali inadaiwa na TANESCO 125 bilioni. 85 billioni kule Zanzibar na 40 billioni Serikali ya Tanganyika lakini hatuoni juhudi za Serikali kukusanya deni hili kubwa pamoja na Serikali kujua fika hali mbaya ya kifedha inayoikabili TANESCO.
MIEZI takribani mitano tangu aondolewe Bilicanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, jana tena Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufikia Sh. milioni 13.5 ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame mkoani Kilimanjaro vinginevyo itafungwa.
Uamuzi huu mpya wa Serikali ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, umekuja ikiwa ni siku moja tu baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analolimiliki Mbowe kutokana na kile alichosema kuwa lipo ndani ya chanzo cha maji ya Mto Weruweru.
Takribani miezi mitano iliyopita, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilivamia na kutoa vitu vyote katika jengo maarufu la Bilicanas lililopo Mtaa wa Mkwepu na Makunganya, Dar es Salaam.
Jengo hilo lililovunjwa wiki mbili zilizopita lilidaiwa kumilikiwa na familia ya marehemu Aikael Mbowe ambaye ni baba mzazi wa Freeman Mbowe.
Hata hivyo, NHC ilieleza kuchukua uamuzi huo kutokana na mteja wake (Mbowe) kushindwa kulipa kodi ya pango zaidi ya sh bilioni 1.172 ambayo ni malimbikizo tangu miaka ya 1990.
Ingawa Mbowe mwenyewe amepata kusema kuwa jambo hilo limefanywa kwa sababu za kisiasa, lakini alipolifikisha Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, kesi yake ilifutwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.
Alisema hali hiyo imesababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Byakanwa alisema Serikali ya awamu ya tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, mbunge huyo ambaye ni mmiliki wa hoteli hiyo iliyopo Kijiji cha Nshara, hajawahi kulipa kodi ya huduma licha ya kuandikiwa barua Januri 21, 2016 ya kumtaka kulipa kodi hiyo ambayo hakuijibu.
“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi.
“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.
Alisema deni hilo lilipwe ndani ya siku 14 na akishindwa atachukua hatua ikiwa ni pamoja na kufunga biashara.
“Ikiwezekana tufafunga biashara hii, kwa kuwa amekuwa na tabia ya kutokujali kama nilivyomwita ofisini kwangu na hakufika na wala kujibu barua, sasa na hili puuzeni tutachukua hatua,” alisema Byakanwa.
“Mnaweza kusema kuwa DC labda anamwonea, mimi nakwenda na vielelezo na hapa pia nina taarifa nyingine kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwa hajapeleka taarifa ya mauzo ili aweze kukadiriwa kodi kwa kipindi cha miaka mitano,” alisema mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na Ofisa Mapato wa Halmashauri ya Hai, David Mlay.
Gazeti hili jana lilimtafuta Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, lakini hakupatikana.
Jana hiyo hiyo MTANZANIA Jumapili lilifanikiwa kuzungumza na dada wa Mbowe aitwae Neel Mbowe, anayesimamia shamba la Veggies, ambaye alisema nyaraka na taratibu zote za umiliki wa shamba hilo anazo kaka yake huyo.
Kuhusu umiliki wa shamba hilo, Neel alisema lilikuwa likimilikiwa na babu yao tangu mwaka 1940 na baadae akampa baba yao, marehemu Aikael Mbowe.
Kwa mujibu wa Neel, walimua kulima katika eneo hilo ambalo lilikuwa pori kwa muda mrefu ili kuongeza ajira kwa vijana wanaolizunguka.
Kuhusu sheria ya mazingira na umiliki wa shamba hilo, alisema anayejua yote hayo ni kaka yake Mbowe.
Juzi Byakanwa alitoa amri ya kusitisha shughuli za kilimo katika shamba hilo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari mbili lililoko Kijiji cha Nshara.
Byakanwa alimshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji ya mfereji.
“Nasitisha shughuli zote za kilimo zinazofanywa katika eneo hili ambalo ni chanzo cha maji ya Mto Weruweru kuanzia leo (juzi) mpaka pale mamlaka nyingine zitakapojiridhirisha na utapaswa kulipa faini zote kulingana na sheria ya mazingira.
“Pia naliagiza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika eneo hili na kuchukua hatua pamoja na kuniletea taarifa walizochukua. Maofisa maliasili wa wilaya wafanye tathmini ya miti iliyokatwa bila kibali na kuleta kiasi cha faini ndani ya siku 14,” alikaririwa Byakanwa.
...Na wewe kwa akili yako unaona ni sawa kwa Serikali kuweka juhudi kubwa kumfuatilia Mbowe mkwepa kodi lakini wakati huo huo inashindwa kuweka juhudi kama hizo kuwafuatilia mafisadi na wezi akina Lugumi, Escrow na ambao wamechota bilioni 37 na 321 billion na kugawa rushwa mpaka ndani ya Ikulu! na unakubali ujinga wa kuambiwa kwamba eti hafukui makaburi ya zamani! Ila hili kaburi jipya la Mbowe ndiyo la kufukua! ama kweli akili ni nywele kila mmoja ana zake.
Tia akili kichwani achana na kukurupuka na kuropoka kama kasuku.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.