Na Mwandishi Wetu
Mwananchi
"Taarifa hizo ni za uzushi, na hivi sasa niko kwenye kikao na watu wengine na si TCAA," alisema Mataka.
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima
"Kwa hiyo walibaini kuwa cheti kilichotolewa kwa ATC na ambacho muda wake ulikuwa umalizike Desemba 15, 2008, hakikuwa kimefuata taratibu. TCAA kwa hiyo iliamua kuiondolea ATC cheti hicho hadi hapo itakapokamilisha taratibu za kuwa na vielelezo vinavyokidhi masharti ya TCAA," ...alisema Mattaka
"Tunajutia usumbufu wowote uliojitokeza kwa wateja wetu na tunawaomba watuvumilie wakati tukiendelea kulishughulikia suala hili," alisema.
Jana/juzi press imeripoti Mattaka kasema hivi kuhusu kufungiwa kwa ATC:
Leo wanaripoti:
Hakuna hata pressman mmoja aliuyemuuliza "sasa juzi ulikuwa unakanusha kanusha nini ?"
Au, alichokikanusha juzi sicho walichotuambia kakanusha. Yani hawakumuelewa.
Tunashindwa kujua nini kinaendelea uongozini kwa sababu hakuna wa kutuhabarisha. Na nusu ya matatizo yetu, I can almost guarantee, nusu ya matatizo yetu yangepotea kama tungekuwa na viable press. Watu wa serikali wangetia akili. The press is the weakest link, followed by parliament offcourse (parliament kazi yao wao ku rubber stamp bills za wizara ya sheria na kupigiana makofi vikaoni.)
Wanatu feed madudu na machafuchafu watu wa crummy press. Tanzania hakuna press hata chembe. You can not pick a newspaper and read a piece devoid of crummy coverage. Not one. Hakuna kitaarifa, news outlet yeyote ile, ambacho hakijapinda pinda!!
...I agree with you. This is the challenge of our time.
Hivi unajua juzi nilikuwa najiuliza, mpaka leo tangu nianze kuangalia internet, website ya IPPMEDIA haijawahi kubadilishwa (Yaani kwa kweli waga nakuwa irritated sana nikifungua ile webpage). Features zake ni zile zile..miaka nenda miaka rudi!....Wakati ukifungua hata zile za watani wetu wa jadi unaopna kabisa mabadiliko...Uptodate za website ndo usiseme kabisa....Yaani these people arent creative at al. Not all. Hawana webmaster jamani?
Newspapers ndo kabisa...hatuna waandishi critical wakuuliza HARD QUESTIONS.
Man we have a longway to go.
Hivi wandugu nchi yetu inaelekea wapi? we seem not to have learnt anything in our failures. Bado tunapeana nafasi za muhimu kwa kuangalia undugu na urafiki. This is WRONG.
Hivi kweli tujiulize mtu kama Mataka ana record gani ya ku-run public parastatals au hata private companies? (naomba nisimuhukumu mwenye kujua aniambie)
Lakini naamini kabisa Tanzania tunahitaji mapinduzi ya kiukweli jinsi tunavyoteuana na kupeana kazi. Shirika kama AIR TANZANIA ile ndo bendera yetu ambayo ingebidi tujivunie! Lakini mpaka leo shirika limekuwa burden kuliko chochote!
I suggest the following:
1. Kujaza nafasi nyeti kama za ukurugenzi wa mashirika muhimu (na mengineyo) kazi tuzitangaze GLOBALLY kwenye magazeti kama economist, guardian na mengineyo. Wenye sifa kutoka pande zote za dunia watume maombi. After all hii itasaidia hata kuwapata watanzania waliobobea katika management ya makampuni makubwa huko nje na ndani. Tukishampata tunayemtaka tunampa job discription na malengo tunayotaka ayatimize. Na Masharti ni kwamba mkataba utaongezwa kwa perfomance na delivery! after every ONE year.
2. TUPUNGUZE POLITICS!! kwenye shughuli nyeti kama hizi. Hebu angalia Management ya KQ ni wazawa na wageni (they complement each other). Jamani tunahitaji kujifunza. Kama tumekumbatia globalization, matakwa yake ndo hayo-let those who can deliver do the job.
3. Raisi ajitoe kufanya appointment kama hizi za maswala ya kiuchumi. Adeal na politics mengine awaachie wataalamu wake. Jamani iweje mkuu wa nchi afanye almost uteuzi wa kila kitu?
4. AIR TANZANIA inahitaji management mpya ya wazawa na wale wa nje. Ni shirika linaloweza kujiendesha kwa faida kabisa. Lakini people are obsessed with corruption and incompetence. Tangazeni nafasi hizo watu watume vyeti..tuache porojo. Tupeane kazi kwa kuangalia vyeti na utendaji wa mtu.
5. Mataka should just give way to another person.
It doesnt matter who runs the organization/company hata kama mtu anatoka El Salvador or Fiji...As long as He/She can deliver thats all we want!
Ona sasa, ashasahau hata jana kasema nini, anazunguka tuu, kiongozi gani huyu.
Pamoja na matatizo yote ya ATCL, bado sielewi ni vigezo gani vilitumika kumpa David Matakka jukumu la kuendesha ATCL. Hana rekodi nzuri ya kazi huyu. Alisimamishwa kazi PPF kwa kashfa ya kuhujumu shirika, huyu/hawa waliompa Mattaka uongozi wa ATCL inabidi wawajibishwe.
Huyu jamaa inabidi aachie ngazi... vinginevyo tutarudi kwenye mashirika ya ugavi watu wanatafuna wanapewa kwingine. Jamaa si alikuwa Bima huyu sasa si aliharibu kule hata shirika liko hoi then now bado wanamchelewesha!! Au kuna kamchezo kama kale kaTANESCO shirika life mashirika fulani ya ndege yapete?
Hawa watu wangekuwa wanafanyiwa confirmation hearing kabla hawajapitishwa. Kwenye confirmation hearing huwa machafuchafu yote ya nyuma yanaibuka. Rais anapeleka jina, wabunge kwenye kamati wanachambua wanapiga kura kama wanamwona anafaa au hafai. Vinginevyo ndo unachagua mtu Waziri wa mambo ya ndani unakuja kuta kakwepa National Service au kafilisi PPF huko in his past life halafu kawa reincarnated kapewa ATC. Duuuh!
Hawa watu wangekuwa wanafanyiwa confirmation hearing kabla hawajapitishwa. Kwenye confirmation hearing huwa machafuchafu yote ya nyuma yanaibuka. Rais anapeleka jina, wabunge kwenye kamati wanachambua wanapiga kura kama wanamwona anafaa au hafai. Vinginevyo ndo unachagua mtu Waziri wa mambo ya ndani unakuja kuta kakwepa National Service au kafilisi PPF huko in his past life halafu kawa reincarnated kapewa ATC. Duuuh!
Ajiuzulu ale wapi?ATC yanusa kifo
Mattaka akataa wazo la kutakiwa ajiuzulu
na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATC), limesema litapata hasara ya sh milioni 300 kila wiki kutokana na kusimamishwa kwa huduma za ndege zake.
Hatua hiyo imefufua maumivu kwa shirika hilo ambalo limekuwa katika jitihada za kuboresha huduma zake baada ya kukabiliwa na matatizo ya kifedha ambayo yalilikumba wakati na baada ya kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, David Mattaka, alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya sababu zilizofanya shirika hilo lifungiwe kurusha ndege zake kwa kushindwa kutimiza masharti 482 ya usalama wa anga.
Mkurugenzi huyo alisema kusitishwa kwa huduma ya ndege za ATC, kunatokana na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) kusimamisha huduma za shirika hilo baada ya ukaguzi uliofanywa na Jumuia ya Kimataifa ya Usalama wa Anga (IOSA) kupitia Kitengo chake cha ukaguzi wa usalama (AYATA), kubaini kuwa TCAA haikufuata taratibu katika kutoa cheti cha kurusha ndege kwa shirika hilo.
Mattaka alisema, ukaguzi huo uliofanywa Desemba, mwaka jana (2007), ulibaini kuwepo dosari 482 katika maeneo ya operesheni yaliyo chini ya TCAA.
Kwa mujibu wa Mattaka, dosari 39 zilibainika katika eneo la oganaizesheni na usimamizi, uongozaji wa ndege, dosari 206, matengenezo dosari 45, sehemu ya mizigo, dosari 44, ulinzi, dosari 36, kitengo cha utoaji, dosari 55, na uwanjani dosari 50.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa, Novemba mwaka huu, Shirika la Kimataifa Linalojishughulisha na Usalama wa Anga Duniani (ICAO), lilikuja kuifanyia ukaguzi TCAA kuhusiana na jinsi inavyosimamia mashirika ya ndege yanayofanya kazi nchini na kubaini kuwa vielelezo vya mashirika ya ndege vilivyokuwa TCAA, havikidhi masharti kwa mujibu wa taratibu zinazoongoza TCAA za mwaka 2006.
Kwa hiyo walibaini kuwa cheti kilichotolewa kwa ATC na ambacho muda wake ulikuwa umalizike Desemba 15, 2008, hakikuwa kimefuata taratibu. TCAA kwa hiyo iliamua kuiondolea ATC cheti hicho hadi hapo itakapokamilisha taratibu za kuwa na vielelezo vinavyokidhi masharti ya TCAA, alisema Mattaka.
Alisema kwa bahati nzuri, ATC iliweza kuwasilisha vielelezo vyote vilivyohitajiwa Desemba 10, 2008, na sasa shirika hilo linaisubiri TCAA ijiridhishe na vielelezo hivyo na kulirejeshea cheti ili liendelee kurusha ndege zake.
Kwa mujibu wa Mattaka, TCCA inatarajia kutumia takribani siku 10 kupitia nyaraka hizo za ATC na kurejesha huduma zake.
Alisisitiza kuwa mapungufu yaliyojitokeza ya kutokuwepo kwa vielelezo hivyo, hayana uhusiano wowote na suala la usalama wa ndege zake na hakuna kipindi ambacho wateja wake walikuwa katika hatari, kwa sababu ya ubovu wa ndege zake.
Tunajutia usumbufu wowote uliojitokeza kwa wateja wetu na tunawaomba watuvumilie wakati tukiendelea kulishughulikia suala hili, alisema.
Mattaka alisema hivi sasa shirika lake linarejesha nauli kwa abiria waliokata tiketi za kusafiri na ndege za shirika hilo katika siku za hivi karibuni, lakini waliomba kusafiri kwa tarehe za mbali, wataendelea kubaki nazo kwani wanaamini baada ya siku 10 kuanzia jana, watarejesha huduma zao.
Alipoulizwa kama yuko tayari kujiuzulu kutokana na kushindwa kuliendesha shirika hilo tangu alipokabidhiwa, Mattaka alisema hafikirii kufanya hivyo kwani anaamini bado anaweza na kutoa wito kwa serikali kuendelea kulisaidia shirika hilo linalochungulia kaburi.
Wakati Mattaka akitoa ufafanuzi huo, Waziri wa Miundombinu,Dk. Shukuru Kawambwa, alisema ATC imesimamishwa kutoa huduma kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya usalama wa anga.
Alisema kufungiwa kwa shirika hilo hakutokani na ubovu wa ndege zake kama inavyofikiria na wengi bali kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa ukaguzi.
Wamesimamishwa kwa muda tu na tatizo si mwekezaji, bali kutofuata utaratibu uliopangwa na IATA, alisema Dk. Kawambwa.
ATC ni shirika pekee la ndege la umma na hadi Mei mwaka huu, lilikuwa na ndege sita, tatu ikiwa inazimiliki na nyingine za kukodi.
Hivi karibuni Kamati ya Miundombinu ya Bunge, ilisema kuwa kulikuwa na mpango wa shirika hilo la ndege kuingia ubia na shirika moja la ndege la China.
David Mattaka alikuwa PPF- kainzisha yeye! aliyeuwa Bima ni Temu