Serikali na Hatima ya ATCL

Date::12/10/2008
Huduma za ndege ATCL zasitishwa ndani, nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), ambalo limekuwa na matatizo makubwa tangu ndoa yake ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ivunjike, limenyang’anywa cheti cha kuruka angani na Mamlaka ya Anga (TCAA) baada ya kukosa viwango vya ubora kuruka angani.

Taarifa kutoka ndani ya ya ATCL zimeeleza kuwa shirika hilo limenyang’anywa cheti hicho tangu Desemba 8 mwaka huu na hivyo litashindwa kusafirisha abiria hadi hapo litakapokidhi masharti ya usalama wa anga na kurejeshewa cheti hicho.

Miongoni mwa viwango hivyo vya usalama ni ukaguzi wa mara kwa mara wa ndege zake, kuwa na wataalamu wa kutosha kama marubani na wahandisi, vitu ambavyo vimeonekana kukosekana kwenye shirika hilo la serikali.

Kufungiwa huko kumekuja huku kukiwa na uwezekano wa shirika hilo kufungiwa na Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga (IATA) kufanya safari zake baada ya kubaini zaidi ya makosa 500.

Mwishoni mwa wiki iliripotiwa kuwa ATCL ilikaguliwa mwezi Oktoba na kubainika na makosa hayo ya usafiri wa anga, lakini ikashindwa kuyarekebisha na ndipo IATA ilipoanza mchakato wa kutaka kuizuia kufanya safari.

“Ni kweli ATCL imenyang’anywa cheti cha viwango kwa kukosa ubora wa kuruka angani hivyo haitafanya safari za nje wala ndani ya nchi,” alisema mmoja wa watu wa ndani TCAA alipohojiwa na Mwananchi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ndege za ATCL zilizokuwa zikifanya safari zake ndani na nje ya nchi haitaweza kufanya tena safari hizo na vigogo wa ATCL jana walikuwa na vikao na TCAA kuzungumzia suala hilo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo alisema hana taarifa kuhusu kunyang’anywa cheti kwa ATCL na kudai kuwa mkurugenzi wa shirika hilo, David Mataka ndiye anayeweza kueleza suala hilo.

“Sina taarifa kuhusu suala hilo... hayo ni mambo ya ATCL na anayeweza kukueleza ni Mataka, hivyo wasiliana naye... haiwezekani toka tarehe nane hadi leo mimi sijui,” alisema Chambo.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mataka alisema taarifa hizo si za kweli na kwamba wako kwenye kikao na watu wengine na si TCAA kama habari zilivyoeleza awali.

Mataka alisema taarifa hizo ni za uzushi na zinatokana na habari zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuhusu matatizo ya shirika hilo ambalo hivi karibuni lilishindwa kusafirisha abiria wake kwenda Afrika Kusini.

“Taarifa hizo ni za uzushi, na hivi sasa niko kwenye kikao na watu wengine na si TCAA,” alisema Mataka.

Mwananchi ilipojaribu kuwasiliana na TCAA, ilithibitishiwa habari hizo kuwa ATCL imezuiwa kufanya safari zake za ndani na nje.

ATCL imekuwa ikitegemewa sana kwa safari za mikoa ya kusini, kaskazini, Kanda ya Ziwa, Zanzibar na safari za Afrika Kusini, ambako katika siku za karibuni safari za kusini mwa Afrika zimekuwa na matatizo makubwa kiasi cha wasafiri kukwama kwa siku kadhaa jijini Dar es salaam.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi uliopita, ATCL ilikuwa na ndege mbili tu zilizokuwa zikifanya kazi, kati ya ndege zake tano na udhaifu huo ulilifanya shirika hilo lipoteze wateja wake wengi wa safari za Mwanza-Dar es salaam na Dar es salaam-Johannesburg.

Serikali imekiri kuwepo na tatizo kubwa la kuliendesha shirika hilo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwaambia wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wake wa Novemba 24 kuwa serikali itafanyia kazi matatizo hayo.

Alisema kuwa suala hilo amekaa nalo na atashughulikia na ili shirika hilo liweze kusimama na kujiendesha.
 
source;Mwananchi
 
Sasa zimesitishwa au hazijasitishwa, which is which?

Regardless, faults 500 ni nyingi sana, hii ni hatari sana!

Wataalamu mliosomea urubani na hasa wahandisi popote mlipo nje na ndani ya Tanzania, natoa wito, tafadhalini, nendeni mka salvage ATCL.
 
Hivi kumbe ATLC bado ipo? Mi nilidhani ilishakufaga siku nyingi....

Ilikufa siku waliyomteua Mataka aendeshe shirika hilo maana hana rekodi nzuri katika kuendesha mashirika, sijui wanangoja nini kuizika.
 
Hili shirika si limewahi kufa na kufufuka mara kadhaa, au nimekosea? I dunno, I don't even follow this stuff much less care for it....

The thought of flying in their planes scares the beejesus out of me. I don't know how people who fly in them even have confidence in them
 
duh,bora aiseeh maana balaa ambalo lingeweza kutokea ni kupoteza maisha ya watu,kumbe tuna watchdog wa kuangalia vitu ATCL,naona sasa watu wanafanya kazi zao,waingie sasa kwenye ile mimeli mibovu na magari...inatia moyo kidogo maana mtu kama Mataka akili yake ni ndogo sana kuendesha shirika kama ATCL,sasa tuone ataongoza nini maana ATCL sasa kaputi...labda wagawane hiyo midege mibovu iwaangushe wenyewe!
 
....kweli kijana inaonekana pale minazi mirefu kwako ukikanyaga ni one way,its time sasa kijana uweke mambo sawa uache michezo..home wanakuhitaji ukasalimie tuu!
 
Aisee kweli bana ile mimeli inayoenda Mtwara mibovu kweli. Na ile migari moshi inayoenda mikoani na yenyewe mikuukuu mno. Fungia yote hiyo
 
....kweli kijana inaonekana pale minazi mirefu kwako ukikanyaga ni one way,its time sasa kijana uweke mambo sawa uache michezo..home wanakuhitaji ukasalimie tuu!

Juzi juzi tu nilikuwa bongo. Mimi sio mwenzako wewe. Na nilienda mkoani lakini niliendesha. Sipandi midege yao mibovu mibovu mimi. Hivi mtu na akili yako timamu eti unapanda ATC....heheheheheee.....

Wewe ndio unahitaji kupata kijani. Nenda Illinois mazee Geeque akakutafutie tunye tunye la makaratasi. Huko Pasadena umelosti tu
 
m
duh,bora aiseeh maana balaa ambalo lingeweza kutokea ni kupoteza maisha ya watu,kumbe tuna watchdog wa kuangalia vitu ATCL,naona sasa watu wanafanya kazi zao,waingie sasa kwenye ile mimeli mibovu na magari...inatia moyo kidogo maana mtu kama Mataka akili yake ni ndogo sana kuendesha shirika kama ATCL,sasa tuone ataongoza nini maana ATCL sasa kaputi...labda wagawane hiyo midege mibovu iwaangushe wenyewe!

Kama ATCL ilikodisha ndege kutoka Liberia (kwa wachovu wenzetu), how low could we go?

Hii ndiyo Bongo bwana! Vitu vya serikali vipo ili kutunisha mifuko ya viongozi na cronies, na sio kuunufaisha umma. Shirika la ndege (ATCL) likiwa hoi, basi Precision Air na mengineyo yafanye biashara nzuri.

Mnataka sababu zaidi za kuing'oa CCM madarakani?
 
Inabidi watu wa nje waje waseme kuwa ATCL ni Maiti.
Hongera Mataka kwa kusaidia kulifikisha hapo lilipo.
 
Finaly nature takes its cause.....

sasa kali ni kwamba tumekodisha ndege majuzi tu ambapo hata pesa za kukodishia hazijarudi leave alone profit!! Duh, kaaz kweli kweli Bongo..... tuone Mkulu atafanya nini this time around manake................
 
Hatimaye yametimia, hivi Mustapha Nyang'anyi bado ni Mwenyekiti pale? Unajua ni aibu sana kwa sirikali kushindwa kuendesha haka kashirika.
 
Nilisikia kashaanza...lkn sina Hakika...Kama bado yupo basi MSIBA...

Ipo Haja ya kuaangalia namna ya kuingia UBIA na Serious Kampanies...ambao wana mitaji ya Uhakika...Ikiwa British Airways yenyewe..inayumba na inataka kuungana na QANTAS...How ATCL can survive in this competitive market?

Wenzetu wa UAE..kila Emirate....ina uwanja wake wa Ndege wa kuwafunza Urubani na Engineers wa Ndege...sie hata Chuo hatuna...Bahati Mbaya hata UDSM kufikiria kuwa College ya Mambo ya AVIATION hatuna....Hatuna MITAJI ...basi Hata AKILI ZA KUFIKIRIA HATUNA...???
 
SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL), ambalo limekuwa na matatizo makubwa tangu ndoa yake ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) ivunjike, limenyang’anywa cheti cha kuruka angani na Mamlaka ya Anga (TCAA) baada ya kukosa viwango vya ubora kuruka angani.

Taarifa kutoka ndani ya ya ATCL zimeeleza kuwa shirika hilo limenyang’anywa cheti hicho tangu Desemba 8 mwaka huu na hivyo litashindwa kusafirisha abiria hadi hapo litakapokidhi masharti ya usalama wa anga na kurejeshewa cheti hicho.

.
.
.
.
.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi uliopita, ATCL ilikuwa na ndege mbili tu zilizokuwa zikifanya kazi, kati ya ndege zake tano na udhaifu huo ulilifanya shirika hilo lipoteze wateja wake wengi wa safari za Mwanza-Dar es salaam na Dar es salaam-Johannesburg.

Serikali imekiri kuwepo na tatizo kubwa la kuliendesha shirika hilo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwaambia wahariri wa vyombo vya habari katika mkutano wake wa Novemba 24 kuwa serikali itafanyia kazi matatizo hayo.

Alisema kuwa suala hilo amekaa nalo na atashughulikia na ili shirika hilo liweze kusimama na kujiendesha.

Don't you love that phrase?!

.
 
Masatu fafanua...kama wameshindwa si waachie Ngazi? au Misifa tu ya kuwa unaongoza...matokeo yake Mataka na Nyang'anyi wanatengeneza CV mbovu...kesho na keshokutwa tukipata President mwingine...wao hawatokuwa na salama....

Leo Obama anaawacha baadhi ya watu wa Bush ktk Utawala wake....that's means wameonesha wanaweza kuendelea nae...!!!
 
Back
Top Bottom