Unahitaji Kuelimishwa!
Kwanza, Serikali haijatoa fedha zozote kwa ATCL baada ya kujitoa from South Africa.
Hapa jukwaani tunaongelea ukweli na wala si ubabaishaji, ATCL ilikuwa inachotewa pesa kutoka hazina kila mwezi kiasi cha 500m/=, muulize Mattaka Au Nyang'anyi juu ya hilo. Suala la msingi ni Mwenyekiti na CEO waeleze hizo pesa walizitumiaje, kukopeshana magari au kulipana posho za vikao. Pia waulize walitaka wachotewe kutoka katika pesa za walipa kodi hadi lini?
Vilevile kama serikali haijatoa fedha YEYOTE, je zile ndege mbili za D-8 fedha zake zimetoka katika mifuko ya nani?
Pili, Serikali inabidi itoe maelzo ya jinsi gani imeisaidia ATCL financially, badala ya kuja na lugha ya kutoa siku saba. Tatu, Mataka ndiyo mtendaji mkuu wa ATC, Board members na Mwenyekiti wao Balozi Nyanganyi ni washauri kutokana na uzoefu wao kusaidia kuliendesha shirika la ndege.
Ni vema ukaelewa kazi za Mtendaji Mkuu ni zipi na za Bodi zipi. Mtendaji Mkuu anawajibika kuendesha na kusimamia shughuli za kila siku za ATCL.
Bodi ina wajibika kusimamia shughuli za ATCL kwa niaba ya Serikali, ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi yote ya kisera kwa niaba ya serikali.
Hata siku moja bodi haiwezi kuwa ni washauri wa ATCL.
BALOZI Nyanganyi aliacha shirika la ndege likiwa na ndege kibao alikpokuwa waziri wa mawasiliano, huduma zilikuwa safi. nilikuwa nikisafiri kwenda Uingereza na ATC, serikali haitaki kusema ukweli "what happened", same stories "Mikataba mibovu" ndiyo imeliuwa shirika hili.
Ndugu yangu wewe ndiye hasa husemi ukweli, wakati Balozi Nyang'anyi akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi ATC ilikuwa haitengenezi faida zaidi ya hasara. Kumbukumbu za mahesabu ya ATC zinaweza kubainisha haya ninayoyaandika. Zaidi ya hapo wakati wa Balozi Nyang'anyi ATC ilikuwa haendi Uingereza kama unavyodai. Na kama Balozi Nyang'anyi aliendelea kuwepo baada ya kumng'oa Rwebangira (Mmoja kati ya GM wengi waliopita ATC), basi atakuwa na maswali mengi ya kujibu juu ya Mradi uliyoiletea hasara ATC wa International Operations (IOPS). Katika kipindi hicho ATC ilikodi ndege moja ya aina ya Boeing 767 kutoka Ethiopian Airlines kwa ajili ya safari za UK nadhani na Rome, Italy. Mradi ambao haukudumu kwa muda mrefu baada ya kuingizia ATC hasara ya mamilioni ya fedha.
Kina MATAKA NA NYANGANYI, wamekabidhiwa shirika halina ndege, madeni kibao, no money, sasa mnataka hawa watu wafanye mazingaombwe. Please hembu tuwe wachambuzi wa mambo na kutafuata ukweli badala ya kupenda kupiga gumzo.
Hawa jamaa unavyojaribu kuwasafisha ndiyo unazidi kuwachafua kabisa, kama hawa jamaa wangekuwa ni wakweli na wanania safi sidhani kama wangeliweza kukubali kuingoza ATCL wakati wakijua kuwa ATCL ina matatizo ambayo wao hawana uwezo wa kuyatatua. Isitoshe kama wali-oversight wakati wanapewa nyadhifa hizo kwanini hawakutumia busara zao kuomba kujiuzulu kama kweli wameona hawawezi kutimiza matakwa ya mwenye mali, walikuwa wanangoja nini au walikuwa wanafanya biashara gani wakati wote huo?.[/QUOTE]
Mwisho kabisa bado nitasimamia ushauri wangu ambao nimekuwa nikiutoa kila siku, Serikali haina budi kukodisha menejimenti kutoka kwenye makampuni yaliyobobea katika kutoa huduma za kimenejimenti za usafiri wa anga. Menejimenti itakayokodishwa inaweza kupewa mkataba wa miezi 36 hadi 48 huku serikali ikiwaajiri watanzania (hapa ninapendekeza vijana) ambao watafanya kazi sambamba na wataalam hao ili waweze kupatiwa uzoefu ambao utakuwa ndiyo mhimili wa uongozi baada ya mkataba kumalizika. Sasa hivi ATCL haina capacity ya kufanya kazi zake au kubuni mipango mbalimbali kwa kufanya tafiti ambazo zitakuwa zimetoa mwanga na mwelekeo wa kutosha katika uendeshaji na usimamiaji wa shughuli za kila siku. Kwa kukodi menejimenti ya wataalam ni rahisi kutumia researches ambazo ziko ready made ambazo wataalam hao watakuwa nazo kutoka na uendeshaji wa menejimenti nyingi na tofauti. Hizo tafiti ambazo zimekwisha fanyika ni rahisi kuzihuisha (Customize) na hali halisi ya ATCL na kupata mwelekeo ulio sahihi.
Endapo serikali itaamua kuendelea na ATCL katika mfumo ule ule usiobadilika basi drama ndani ATCL hazitakwisha.
In short katika ulimwengu wa leo wa Mashirika ya ndege ATCL inaendeshwa kiubabaishaji kabisa.
Jamani, hivi nyinyi hamjiulizi kwa nini serikali haijatoa tamko hadi leo?? Mataka na balozi nyanganyi wameeleza wazi tatizo ni nini, pesa haijatoa hata sumni SINCE Ahadi hizo zianze last two years. Issues zote za madeni yaliyoachwa baada ya kutenguana na afrika kusini hayajalipwa. Tatizo si uongozi, tatizo ni FEZWA!!! Na ukiwa na madeni hakuna benki itataka kukukopesha. Serikali imesikia yote yaliyosemwa na uongozi wa ATC mbona hakuna majibu?? Na sababu ni kubwa ni UTEKELEZAJI WA MAAGIZO SERIKALINI, HUU URASIMU LAZIMA TU-UTAFUTIE DAWA. Tusubiri kama serikali itasema kuwa iliwapa shilingi ngapi ATC na wakashindwa kufanya kazi, hembu wabongo tuwe wapembuzi wa mambo. Mimi siko bongo lakini ninafuatilia habari hizi kwa utaratibu na kumake sense out of it.
ok tuseme serekali hakutoa fedha kwa uongozi wa atc, sasa hizo hela walizo kuwa wanafuja walitoa mfukoni kwao.
ATCL yawatupia mzigo Mramba, Chenga, Lowassa
Leon Bahati
SAKATA la kusimamishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania Tanzania (ATCL) katika kuto huduma limechukua sura mpya baada ya Ikulu pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Basil Mramba na Andrew Chenge kuhusishwa hivyo kutakiwa kutoa maelezo.
Wengine ambao nao watatakiwa kutoa maelezo kuhusiana na suala hilo ni Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na maofisa watendaji wa Wizara ya Miundombinu wakati ikiwa chini ya mawaziri wawili wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne, Basil Mramba na Andrew Chenge.
Habari za kuaminika zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zilieleza kuwa maelezo yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL, Balozi Mustapha Nyang'anyi kwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa wiki iliyopita, zimehusisha vigogo hao katika kiini cha matatizo ndani ya shirika hilo.
Wiki iliyopita, Dk. Kawambwa alimpa siku saba Nyang'anyi kutoa maelezo yanayohusu sababu zilizosababisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA) kunyang'anywa ATCL leseni ya kurusha ndege.
Nyang'anyi aliwasilisha maelezo hayo wiki iliyopita na kutaja baadhi ya mamlaka hizo za serikali kuwa zilipatiwa maelezo ya kina kuhusu hali ilivyo ndani ya ATCL pamoja na mapendekezo yanayotakiwa kufanywa, lakini hakuna kilichofanyika katika kuliokoa shirika hilo.
Waziri Kawambwa pamoja na timu ya wataalamu wake waliyapitia maelezo hayo mwishoni mwa wiki walibaini kuwa katika kufikia maamuzi ya utetezi huo, inabidi wapate maelezo ya kina kwa mamlaka hizo ambazo kwa nyakati tofauti siku za nyuma, walitakiwa tarifa ili wanusuru shirika hilo.
Dk. Kawambwa jana aliliambia gazeti hili kuwa bado wanaendelea kushughulikia maelezo hayo ya bodi na kuahidi kutoa tamko rasmi baada ya kukamilisha mchakato.
Chanzo chetu ndani ya wizara hiyo, zilisema kuwa mkakati huo umefikia mahali pagumu kwa kuwa mbali na kupata maelezo ya vigogo kadhaa, itabidi wachunguze msimamo wa serikali tangu ilipoazimia kuvunja mkataba na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).
"Utetezi wa bodi umetupa wakati mgumu na wala sifikiri kama maamuzi yanaweza kutoka mapema," kilieleza chanzo hicho kikifafanua:
"Ofisi nyeti sasa zimehusishwa... Maamuzi hayawezi kufikiwa mpaka tupate kauli zao, kama ni kujikwaa itajulikana ni wapi."
Ingawa chanzo hicho hakikuweza kuweka bayana namna watakavyoweza kupata maelezo ya mamlaka hizo, lakini kimeweka wazi kuwa chunguzi huo, utafanywa pia kwa kuzingatia mikakati na mipango ya serikali kwa ATCL kuanzia utawala wa serikali ya awamu ya tatu.
Kulingana na maelezo ya bodi, serikali ya awamu ya nne ilipoamua kuvunja mkataba na SAA, iliweka maazimio ya kutoa fedha za kuifufua ATCL jambo ambalo halikutekelezwa.
Miongoni mwa mambo ambayo yamo kwenye maelezo hayo na ambayo pia Balozi Nyang'anyi aliwahi kulieleza gazeti hili ni serikali kutotekeleza ahadi yake ya kulipa deni la ATCL linalofikia Sh19 bilioni pamoja na mtaji wa dola za Marekani 67 milioni.
Wakati huo huo, serikali imetoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA) kwenda kukagua karakana zinazotumika kufanyia matengenezo ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) nchini Kenya na Afrika Kusini.
Sehemu ya fedha hizo pia itatumika kwa ajili ya kununua vipuri vya ndege ambavyo ni kwa ajili ya matengenezo madogomadogo ya dharura kwenye karakana ya ATCL.
Habari zilizopatikana jijini Dar es salaam jana na kuthibitishwa na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa zilisema kuwa mkakati huo ni sehemu ya kuhakikisha kuwa ATCL inarejeshewa haki yake ya kurusha ndege waliyonyang'anywa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Anga (TCAA).
Katika kufanikisha hilo, alisema serikali imekusudia kutumia dola za Marekani 273,000 kwa ajili ya kufanikisha kusudio hilo.
Hata hivyo, Dk. Kawambwa hakuwa tayari kuelezea kwa undani taarifa ya serikali kutoa zaidi ya dola 100,000 kwa ajili ya kusafirisha maofisa wa TCAA na ununuzi wa vipuri, kwa maelezo kwamba ni suala la kiutendaji zaidi.
Wakati huo huo, Ofisa Uhusiano wa TCAA, Abel Ngapemba alithibitisha kuwa wataalamu wake wanaendelea kupitia nyaraka mbalimbali za ATCL zilizopelekwa mahususi kusahihisha kasoro zilizoonekana ndani ya shirika hilo.
Hata hivyo, alisema ni vigumu kueleza iwapo kuna uwezekano wa ATCL kurejeshewa leseni yake katika siku za karibuni kwa maelezo kuwa wataalamu wa TCAA, kwa sasa wametingwa kiasi kwamba imekuwa vigumu kupata upenyo wa kueleza hatua waliyofikia.
"Wataalamu wetu wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana. Hata walipo siyo rahisi kuwasiliana nao maana 'wako-buzzy' (wametingwa) sana," alisema Ngapemba.
ATCL ilikuwa imeahidi kukamilisha mpango wa masahihisho wa nyaraka zake ndani ya siku 10 ambazo ziliisha jana.
Ngapemba alisema kuwa ATCL tayari imewasilisha vielelezo hivyo na sasa inasubiri maamuamuzi ya TCAA.
TCAA waliinyang'anya ATCL baada ya kubainika kuwa na kasoro kadhaa kwenye nyaraka zake za kuendeshea shirika ambazo ni kinyume na kanuni za Umoja wa Mashirika ya Ndege Duniani (IATA).
Serikali iliamua kuingilia kati na kusaidia fedha za kufanikisha mpango wa ATCL kurejeshewa leseni yake baada ya kubaini kuwa shirika hilo linakabiliwa na hali mbaya ya fedha.
Daily News 31 Dec.08 imeandika kuwa TCAA imeirudishia ATCL licence to fly na hivyo itaanza kuruka sasa. Lakini cha kushangaza ni kuwa - IATA bado imeifungia ATCL na haitaifungulia mpaka warekebishe mambo yao, hasa ya kiusalama wa anga na abiria.
TCAA imepewa pressure na serikari na vigogo wake mpaka imekubali kuwafungulia leseni bila kujali kuendelea kufungiwa na IATA na bila kujali kuwa ndege za ATCL hazina service ya kuaminika kutokana na ukata. Maamuzi hayo ni ya kusikitisha na kutojali usalama wa watanzania.
Kufungiwa na IATA kuna maana ndege za ATCL zisiruke na kama nchi italeta ubishi basi inaweza kuruka nchini mwao tu, kwani nchi nyingine hawataruhusu ndege za ATCL kuingia anga zao huko kwani zinaweza kuleta ajali. Pia ndege za mataifa mengine zinapoingia anga yetu huwa na wasiwasi sana kwani huenda wakakutana na ndege mbovu na sisizofuata taratibu za kimataifa huko angani na kusababisha hatari huko juu.
Hatua ya TCAA ni kuonyesha ukaidi wa Serikali yetu na itaweza kuleta madhara kwa raia.
Ni Bora TCAA ifanye kazi zake kwa - ki-professional and kuwa independence. Wasikubali pressure za kisiasa.
Jambo ya pili ni hatua ya Bodi ya ATCL kuwakodisha maconsultant wa Price Water Coopers kwa fedha nyingi sana. Kampuni kama TAC Associates au Kampuni ya Tija ya Taifa ingekuwa ya nafuu sana kulinganisha na Price WaterCoopers
Pia:
ATCL haikuitisha zabuni ya kazi hiyo waliyopewa Price Water Coopers, Rushwa imetembea kutokana na urafiki wa Partner Mndolwa za Price Coopers na Mr. Nyanganyi na Mataka
Hii pia ni kinyume cha taratibu za Public Procurement regulatory Authoryt - Dr. Angalia hapo
Kampuni ya Price Water Coopers pia ni wakaguzi wa mahesabu wa ATCL. Hivyo kwa taaluma yao huirihusu wao kujiingiza katika kazi za manajimenti ya kampuni. Wakaguzi huru kuruhusiwa kuwa Management Consultant kwa kampuni wanayoikagua ni kunyume cha professional ethics zao na pia kunawasababishiwa kukosa independence - Bodi ya wakaguzi iliyolala, na inayoongozwa na maPartners hao wa PriceCoopers wanatakiwa kukemea hili
Ukaguzi wa ATCL kwa kutumia Price Coopers Waters imegharimu zaidi ya millioni harobaini wakati TAC Associates walikuwa wanakagua kwa shillion million zisizozidi kumi
PriceCoopers imepeleka wafanyakazi ATCL akiongozwa na Mkuu wa idara ya fedha, mkuu wa ukaguzi ndani, hivyo hawa watendaji wakuu wamekuwa kwa muda mrefu wanapeleka kazi kwa mwajiri wao wa zamani. Hou ni Eliasaf Methew, William Haji (kaondoka) na dada wa kichaga binti Lyimo wa Kimara.
Kuna rushwa tupu inanuka ATCL katika mambo ya procurement.