Namichiga
JF-Expert Member
- Jun 1, 2017
- 356
- 554
Katika vyombo vingi vya habari limetawala sakata la ukaguzi wa maduka ya kubadili fedha za kigeni,sakata ambalo limeleta taharuki kwa kuwa limehusisha jeshi la ulinzi (JW). Nyuma ya pazia kuna fununu!
Makampuni mengi yaliyojisajili kwa manunuzi ya korosho hapa Tanzania, mfano Afrisian, Export ,Olam, Alpha, Alpha Choice, Alpha Crust,Viikat,Alpha na Mata, Mkemi Agrix,Maviga na mengineyo mengi ni madalali (agents).Makampuni haya huingia makubaliano ya kuyanunulia korosho makampuni kutoka India, Vietnam ,Singapore na kwengineko duniani.
Hivyo basi bodi ya korosho Tanzania (CBT) inapotangaza ratiba ya manunuzi ya korosho kwenye minada,makampuni haya huanza kuingiziwa fedha na makampuni hayo ya nje kwa ajili ya manunuzi.
Hivyo basi kwa mwaka huu mpaka wakati serikali inatangaza kufuta leseni za ununuzi wa korosho,makampuni mengi tayari yalishakua na pesa za watu. Na kwakua biashara hakuna basi inawapasa kurudisha.
Lakini kilicho cha ajabu,hakuna zoezi gumu kwa sasa kama kutuma pesa za kigeni nje ya nchi. Lengo likiwa ni kuyakomoa makampuni yote yaliyotaka kununua korosho,kwani pesa zinahitajika zikafanye manunuzi ya korosho kwenye nchi nyingine lakini hazitoki.
Rai yangu kwa serikali kama raia mwema, figisu hizi zikizidi tutafukuza wawekezaji. Makampuni haya japo tumeshindwa kupata muafaka wa manunuzi ya korosho lakini bado tunawategemea kwenye manunuzi ya Ufuta, Dengu,Girigiriani,Choroko na mazao mengine.