Ujenzi wa viwanda unawezekana zaidi chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita

Tao

Senior Member
Nov 10, 2018
104
190
Na Otieno Peter Baraka

Sote tunajua kuwa ilikuwa ni ndoto ya Hayati Dr John Joseph Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi mkubwa kwa kuwa na viwanda vidogo,vya kati na vikubwa,Hayatti Dr John Joseph Pombe Magufuli aliinadi sana sera hii na tulivutiwa nayo kwani tuliamini kuwa atatutoa kimasomaso kwani viwanda vingi vilivyojengwea hapa nchini nyakati zile za utawala wa mwalimu Nyerere vimekufa kitambo huku ujenzi wa viwanda vipya ukifanyika katika spidi isiyoridhisha.

Kwakuwa hayatI Dr Magufuli alitamani sana kuona ndoto yake hiyo ikitimia ilifika wakati baadhi ya wasaidizi wake hasa mawaziri wakitoa takwimu feki kuhusu idadi ya viwanda vilivyokuwa vimejengwa katika wakati huo,hata hivyo ukiangalia kwa makini unaona kuwa ilikuwa ni vigumu sana kwa ndoto hiyo kuweza kutimia kutokana na misimamo ya hayati Magufuli,baadhi ya sera zake na maamuzi kama kiongozi mkuu wa nchi ambaye katiba imempa mamlaka na madaraka makubwa sana.

Tanzania ya viwanda ilibaki kuwa kauli mbiu tu,hakukuwa na mkakati au mpango kabambe wa kitaifa wa kujenga viwanda,hakakuwa na sera ya kitaifa ya Tanzania ya viwanda na namna ya kuifikia na hata washikadau muhimu katika sekta ya viwanda na uzalishaji kwa ujumla hawakuhusishwa bali walibaki kutazama tu kwenye runinga zao jambo hilo likinadiwa na wanasiasa.

JPM hakupenda kuona wawekezaji wakubwa wa kigeni wakija hapa nchini kuwekeza,yeye aliwachukulia wawekezaji hao na nchi wanazotoka kama wezi wa rasilimali za taifa hivyo alijikita kutoa hotuba mbalimbali kuwananga mabeberu,jambo hili si jema kwa taifa linalotoka kupiga hatua kubwa za maendeleo kwani utafiti unaonyesha kuwa mataifa yaliyofungua milango na madirisha kwa wawekezaji wa kigeni ndiyo yamepiga hatua kubwa katika maendeleo.

JPM alitaka kurudisha mfumo wa centralized economy unaotumiwa na mataifa yanayofuata sera ya ujamaa na kujitegemea na hivyo hakupenda kuona sekta binafsi ikiimarika,hili ni tatizo kubwa na ifahamike kuwa kama taifa hili linataka kupiga hatua kubwa ya maendeleo ni lazima pamoja na mambo mengine liimarishe sekta binafsi

Katika zama hizi siyo lazima serikali ifanye kila kitu na kwakuwa serikali ya JPM ilitaka kufanya biashara mashirika mbalimbali binafsi yalifilisika au tunaweza kusema yalihujumiwa na kufa. yakiwemo maampuni ya mawasiliano, mashirika ya ndege kama fastjen na kadhalika

JPM hakuwekeza ipasavyo katika sekta ya kilimo,alitumia muda wake mwingi zaidi kupunguza kero kwa wakulima hasa kwenye suala la kodi za usafirishaji wa mazao lakini hakufanya vizuri katika kuongeza uzalishaji kwani tunapaswa kama taifa kuondokana na jembe la mkono,kuwekeza katika umwagiliaji, tafiti za kilimo na mambo megine mengi.

Hili tatizo la serikali kutowekeza ipasavyo kwenye kilimo halikuwa tatizo la serikali ya awamu ya tano pekee bali ni tatizo la serikali za awamu zote hapa Tanzania

Serikali ya awamu ya tano iliwaingilia sana wakulima na kuwaumiza kutokana na tabia ya kutoa maelekezo ya pupa kama lile la wakulima wa korosho kule Mtwara

Kwenye sekta ya kilimo Serikali ya awamu ya sita imeanzisha mpango kabambe uitwao BBT unaosimamiwa ipasavyo na wizara ya kilimo chini ya Hussein Mohamed Bashe

Dr Samia Suluhu Hassan anafanya jambo zuri sana kwa kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini na hili litachukua muda na ndio maana anasafiri sana ili kuweka mambo sawa.Mkutano wa uchumi wa Dunia uliofanyika Davos Uswisi ni moja ya forums ambazo yeye kama mkuu wa nchi aliweza kuzitumia kukutana na wawekezaji, kutambua fursa za kibiashara na kuwahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania inawahitaji.

Dr Samia Suluhu Hassan vilevile ameweza kutuondoa kwenye madhila yaliyosababishwa na maamuzi ya pupa ya JPM kama lile la kuondoa fedha za serikali kwenye mabenki,jambo lililosababisha tatizo kubwa kwenye mzunguko wa fedha.Isitoshe serikali yake haikuwalipa kwa wakati wakandarasi mbalimbali waliokuwa wanaidai serikali,hii nayo ilipelekea baadhi ya makampuni hayo kufilisika.

Mama amewapa confidence wafanyabiashara kwani wakati wa JPM baadhi yao walikimbia nchi na kwenda kuwekeza nje kutokana na masuala ya utekaji na hata kunyanganywa fedha na mali zao,Yes kuna mengi mazuri alifanya.

katika kukuza viwanda kama vile ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha umeme yaani stiglers gorge na ujenzi wa reli ya kisasa,haya hayatapuuzwa kamwe lakini ieleweke kuwa ili nchi ipate maendeleo katika sekta ya viwanda haina budi kuunganisha sekta mbalimbali na siyo kuishia kwenye ujenzi wa barabara,viwanja vya ndege na miradi ya umeme pekee.

kila sekta ni muhimu na lazima ichukuliwe kwa uzito unaotakiwa hivyo tunapaswa kuimarisha skta ya fedha,tuwe na sheria zinazowavutia wawekezaji, tuwe na ardhi zilizoandaliwa kwa ajili ya uwekezaji na siyo mapori,tuwe na umeme wa kutosha,maji, tuwekeze katika vyuo vya kati vya ufundi na kuimarisha taasisi zinazofanya tafiti za maendeleo.

Taifa letu lina tatizo la kuwa na siasa zisizotabirika na kila rais anakuja na mambo yake,hili ni kikwazo hivyo imefika muda muafaka nchi yetu iweze kuwa na DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO na rais anapoingia madarakani ale kiapo cha kuitekeleza na kuisimamia la sivyo tutaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu

Hivyo tunaweza kusema bila uoga kuwa Rais wa awamu ya sita Mama yetu kipenzi Dk Samia Suluhu Hassan anaweza kutufikisha katika Tanzania ya viwanda kutokana na maono aliyonayo,uwezo wake wa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi,Hekima aliyonayo,Uadilifu, upole,unyenyekevu. na taaluma aliyonayo inayompa uweza wa kujua mifumo ya kidunia,umuhimu wa mahusiano mazuri ya kidiplomasia na maendeleo kwa ujumla
 
Back
Top Bottom