Serikali msiwafutie Watoto matokeo, toeni matokeo yao haraka. Hawana hatia. Tatizo ni Mfumo

Watoto kuponzwa hakuondoi ukweli kuwa matokeo husika ni batili, kwa hiyo haiwezekani kuwaachia tu. Waumie lakini tabia hii ife. Kama kuna mwalimu anaona mazingira ya kazi ni magumu hawezi kufundisha mtoto akafaulu, aiachie serikali shule zake badala ya kutufugia wezi. Hakuna shinikizo linalohalalisha wizi wa mitihani. Tabia hii ife.
 
Unaongea kama siyo mzazi vile.
Watoto wa kileo ni zaidi Ku cheating.
Hukumu hiyo ni stahiki. Acha wakajifunze walichoo chagua.
hawa jamaa ni wazi sasa wameanza kuingia majukumu ya serikali. Naiomba sana serikali izidi kukaza zaidi
 
Watoto kuponzwa hakuondoi ukweli kuwa matokeo husika ni batili, kwa hiyo haiwezekani kuwaachia tu. Waumie lakini tabia hii ife. Kama kuna mwalimu anaona mazingira ya kazi ni magumu hawezi kufundisha mtoto akafaulu, aiachie serikali shule zake badala ya kutufugia wezi. Hakuna shinikizo linalohalalisha wizi wa mitihani. Tabia hii ife.
mkuu katika jamii yoyote tunayoishi kuna sheria. baraza la mitihani lina sheria na ndio maana likaitwa baraza la mitihani. Kazi ya baraza ni kusimamia shughuli nzima ya mitihani. Kwa anayeiba mtihani adhabu yake ndio hiyo kufutiwa mtihani. ndio adhabu yake. Tusiingilie kazi za baraza. Mtoa maada shule yake iliiba mtihani ili wanafunzi wake wafauru sana. Sasa wanafunzi wa shule yake wameadhibiwa kwa mujibu wa sheria leo anakuja kulalama hapa. Inatakiwa nayeye akamatwe maana anahalalisha uwizi wa mitihani.
 
Hata akitoka mwl kutoka ulaya hakuna kitakachobadilika.
Mfumo wetu wa Elimu inabidi ubadilike.
Maana sahiz hii serikali inalazimisha kila mtoto ni lazima afaulu awe anajua kusoma au hajui kusoma.
Elimu yetu inapotea kwa kukosa maarifa na ujuzi.
Tatizo la mfumo wa elimu liko nchi nyingi, na ndio maana nchi nyingi zimezalisha watu wa wakuongea, kuandamana na kulaumu, Tunahitaji vyuo vya ujuzi vingi sana na sio hivi vyuo vikuu vilivyopo.
 
Back
Top Bottom