Serikali msiwafutie Watoto matokeo, toeni matokeo yao haraka. Hawana hatia. Tatizo ni Mfumo

Tunawadhulumu watoto kwa makosa tuliyoyaandaa wenyewe
 
UDANGANYIFU? Hii kali,kama tu udanganyifu unafanyika ili tu chama fulani chenye nguvu kishinde uchaguzi,iweje watoto wadogo wanyimwe haki yao ya msingi kupata elimu? Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha.Hii si haki,udanganyifu umekuwa ni sehemu ya kujipendelea,wakubwa ndiyo wameasisi hii tabia.Hakuna logic kifilosofia kufutia wanafunzi matokeo wakati mfumo wenyewe wa elimu umepitwa na wakati na haumsaidii mwanafunzi hususani wa ngazi hiyo kuyatumia maarifa aliyoyapata kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe
 

Yeye ndiye Sheria na ndiye Katiba ya Nchi hii. Atakalo linafanyika na asilotaka halifanyiki.. Usipomuomba yeye afanye, basi hizo Mahakama unazotaja hazina Uwezo wa kuamuru chochote.
 
Wakati huo askari na bunduki anakuwa yupo wap
 
Wakome kuibia!
 
Hata akitoka mwl kutoka ulaya hakuna kitakachobadilika.
Mfumo wetu wa Elimu inabidi ubadilike.
Maana sahiz hii serikali inalazimisha kila mtoto ni lazima afaulu awe anajua kusoma au hajui kusoma.
Elimu yetu inapotea kwa kukosa maarifa na ujuzi.
 
NECTA,chombo chenye jukumu la mitihani iliyo chini yake,chombo hiki kipo kisheria.Katika falsafa za elimu chombo hiki hakifuati misingi ya elimu hasa linapokuja suala la matokeo ya mtihani kwa wanafunzi.Inawezekanaje mwanafunzi atangaziwe kafeli? Kwani wanafunzi huenda shuleni au chuoni kufeli? Ina maana mwanafunzi aliyefeli hakujifunza chochote,ni debe tupu? Mfumo huu umeua vipaji na vipawa vingi vya wanafunzi,na hakuna utaratibu wa kufuatilia wanafunzi waliofeli huishia wapi na hayo maarifa e
waliyoyapata.Sasa kama tu hao wanaofeli hakuna wa kuwajali itawezekana vipi kwa hawa walifutiwa matokeo? Maana yake hao wanafunzi hawataendelea na masomo kama wazazi wao hawana uwezo wa kuwapeleka shule za kulipia.Itabidi waingie mitaani au kwenye ajira zisizo rasmi
 
Mkuu umeanza vizuri ila hapo kumhusisha mheshima rais kwenye upuuzi huu ni kosa kubwa

Kiufupi naunguna na hoja yako kuwa mtoto hahusiki kwa namna yoyote ile kwenye hili sakata, hivyo kumfutia matokeo na kumwacha aliyekuwa akimsimamia naona kama haileti maana,

Hivyo kama ulivyosema baraza la mitihani liwawajibishe wale wote waliohusika katika monitoring ya hii mitihani na watoto waliofutiwa matokeo watendewe haki ikiwemo eidha kutungiwa mitihani mwingine na kuufanya upya
 
Siyo kila Jambo lililokuwa linafanyika toka enzi za ukoloni likifanyika leo linakuwa zuri,
Ukiona linaendelea basi watz waliowengi wanalikubali. Unataka hata wakiiba mtihani waachwe tu kama mleta mada anavyoshauri hiyo elimu yetu itakuwa inaelekea shimoni
 
Wangeanza kufuta matokeo ya uchaguzi kwani watu wametumia hayo matokeo kama case study....Mungu anawaona walaih
 
Darasa la saba ana hatia gani? Kama vp wawape mtihani tofauti wawapime kivyao hao wanaofutiwa.
Kama umefika daraa la Saba na hamjui maana ya kuna huyu mtoto huko mbele atakuwa very corrupt nawapa kongole Necta..... waalimu nao wana makosa yao kila mtu ashinde mechi yake......
 
Afadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…