Kamati ya Bunge yatoa pongezi BMT kuendeleza michezo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

KAMATI YA BUNGE YATOA PONGEZI BMT KUENDELEZA MICHEZO

Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti Mhe. Husna Sekiboko imelipongeza Baraza la Michezo la Taifa kwa kuendelea kusimamia Sekta ya michezo ambayo kwa sasa inaitangaza vyema Tanzania na kusimamia Utawala Bora ambao umepunguza migogoro katika Sekta hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Utekekezaji wa Majukumu ya Baraza hilo leo Oktoba 25, 2023 Jijini Dodoma, iliyowasilishwa na Bi. Neema Msitha kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Bi. Neema Msitha amesema Sekta hiyo imeendelea kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuwa mwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027, kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ambao umesaidia Timu za Taifa katika mashindano mbalimbali.

"BMT imefanikiwa kuanzisha mfumo wa Kidigitali, Usajili wa Vyama na Mashirikisho, na Michezo mbalimbali ikiwemo Riadha, Timu za Mpira wa Miguu, Netiboli, Gofu, Ngumi zimefaidika na Mfuko wa Maendeleo ya Michezo" amesisitiza Bi. Neema Msitha.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo, Mhe. Husna Sekiboko ameielekeza Wizara iangalie namna bora ya kusimiamia vyema Idara zinazosimamia Maendeleo ya Michezo katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri pamoja na kuhakikisha mtiririko wa asilimia tano za michezo ya kubahatisha inafika kwa wakati.

Wakichangia taarifa hiyo Wajumbe wa Kamati wamepongeza uhusiano uliopo kati ya Wizara inayosimamia michezo Tanzania Bara na Zanzibar, Serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu huku wakishauri kuajiri walimu wa michezo, kufanyika mashindano mbalimbali ikiwemo Taifa Cup pamoja na kuhakikisha asilimia tano ya michezo ya kubahatisha inafanya kazi yake ipasavyo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.28.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.28.jpeg
    34.1 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.29(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.29(1).jpeg
    26.2 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.30(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.30(1).jpeg
    34.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.30(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-25 at 21.33.30(2).jpeg
    46.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom