Serikali: Matukio 21 ya watu kutekwa na kupotea yamepatiwa ufumbuzi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ameeleza kuwa robo tatu ya matukio yaliyoripotiwa ya watu kutekwa na kupotea kwa mwaka 2023 tayari yamepatiwa ufumbuzi.

“Sio kwamba labda watu wanapotea halafu hakuna kinachofanyika, watu hawawapati wahalifu, hawawapati wahanga sio sahihi, ameeleza Masauni.

Masauni alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima aliyeuliza na kutoa mfano kuhusu matukio ya utekaji Bungeni.

“Kuna taarifa za utekaji zimeanza tena katika nchi ya Tanzania, nakumbuka wiki mbili zilizopita, mtoto wa Muhammad Al-Jabriy wa Zanzibar Cable alitekwa kule Dar es Salaam, na maiti yake ikaja kuokotwa baadae imekatwa vipande vipande na macho yametobolewa,” alieleza Gwajima akiomba ufafanuzi wa serikali.

Akijibu swali hilo Masauni alieleza kuwa matukio 21 kati ya matukio 29 ya watu kutekwa na kupotea yalipatiwa ufumbuzi mwaka 2023.

“Kwa takwimu ambazo ninazo kuanzia Januari hadi Disemba 2023 kati ya matukio ambayo yanazungumzwa ya kusema watu wamepotea, haijulikani wameenda wapi haijulikani nini.Kati ya matukio 29, matukio 21 Polisi imebaini waliohusika.”

“Vyanzo vilivyobainika wivu wa mapenzi, ushirikina, kugombania ardhi, kujiteka, visasi, utapeli,” aliongeza.

Masauni pia kuwa amepokea malalamiko manne kuhusu matukio ya watu kupotea ambayo ameyaundia tume maalum.

BUNGENI
 
Area D
1707506843088.png

Walinzi wakaondolewa
Baadae CCTV zikaondolewa
 
kuna mambo yanachekesha sana ukimsikiliza kamanda murilo ni kama anakwepa.
ukamataji wa polisi na idara nyingine zimejipa mamlaka kutokuojiwa na kuvunja sheria ili inapelekea ndani ya jeshi na nje ya jeshi mfano watu wabaya kutumia mwanya uo.
mfano unakuja kukamata mtu bila taarifa unamuiba na mabunduki na gari mnayokuja nayo usajili hakuna utaelewa nini ?.
kama ukamataji kwa nini wasifikishwe sehemu usika kama mahakama au kuwa na jarada lakini hakuna jarada wala kinacho husika.
mi na kupa fact tu polisi na TISS kuna kitengo maalumu ambacho kipo kwa kazi hii na kimeundwa kutokana na sababu za kisiasa,uhalifu,ujumu uchumi,ugaidi na n.k ila umepitiliza mpaka kuwa wazi sasa
 
Back
Top Bottom