Mkurugenzi wa Uchimbaji Visima aondolewa kwa kutofika Hanang baada ya Mafuriko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuondoa kwenye nafasi yake Mkurugenzi wa Sehemu ya Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa, Mhandisi Mashaka Sitta baada ya Mhandisi Sitta kutotimiza vema majukumu yake katika eneo hili muhimu la uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa na usimamizi wa mitambo na zaidi kutofika Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara baada ya kutokea changamoto ya mafuriko yaliyosababisha vifo 80, majeruhi na uharibifu wa miundombinu ikiwemo ya maji licha ya Maboss zake akiwemo Waziri Aweso kufika Hanang.

Kufuatia mabadiliko haya Aweso amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa RUWASA Mhandisi Ndele Mengo kuchukua nafasi hiyo ya Sitta na amemuelekeza Mhandisi Ndele kufika mara moja Wilayani Hanang na kuanza kazi ya usimamizi wa uchimbaji wa visima kwa maeneo ambayo miundombinu ya maji imeathiriwa na mafuriko.

Aweso amesema mabadiliko haya yamelenga kuimarisha sehemu ya uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa na kusisitiza kuwa mchakato wa uundwaji wa Wakala kamili wa DDCA unaendelea na utakamilika kwa wakati.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemteua Mhandisi Mariam Majala kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Ufundi, RUWASA, kabla ya uteuzi huo Majala alikuwa Meneja wa RUWASA mkoa wa Simiyu na amemteua pia Mhandisi Abbas Pyarali kuwa Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Usanifu na Usimamizi wa Miradi ya Maji Wizara ya Maji, awali alikuwa Mhandisi Mkuu katika Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Wizara ya Maji.

Waziri Aweso amefanya uteuzi huu kwa mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Namba 5 ya Mwaka 2019 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira.

Millard Ayo
 
Yaani uokoaji bado mnataka kuchimba visima, mtakuta maiti huko chini, pia Sasa hivi water table iko juu sana, msubiri kiangazi.

Watu muhimu kwa Sasa ni WA ujenzi, utafiti wa miamba, na Wizara ya ardhi ikafanye kuwa-reallocate watu wa hapo wasiendelee kukaa eneo hatarishi, wawapimie viwanja.

Watu wa kilimo, jkt kikosi Cha ujenzi wahamishie mitambo yao huko ikafyatue tofali, kilimo wapeleke mbegu, ustawi wa jamii kwa counselling, elimu kwa kuwa organize wanafunzi for january

Waziri alikuwa anamtafuta muda mrefu may be, kapata timing ya kumchinja
 
Nakazia hasa water table kuwa juu
 
Kwa maelezo yako kwa sasa maji sio muhimu ? Hiv unatumia nin kufikiria lakin wew 😂😂😂😂 Au ndio Pinga Pinga Fc 😂😂😂😂
 
Yaani uokoaji bado mnataka kuchimba visima, mtakuta maiti huko chini, pia Sasa hivi water table iko juu sana, msubiri kiangazi.

Watu muhimu kwa Sasa ni WA ujenzi, utafiti wa miamba, na Wizara ya ardhi ikafanye kuwa-reallocate watu wa hapo wasiendelee kukaa eneo hatarishi, wawapimie viwanja.

Watu wa kilimo, jkt kikosi Cha ujenzi wahamishie mitambo yao huko ikafyatue tofali, kilimo wapeleke mbegu, ustawi wa jamii kwa counselling, elimu kwa kuwa organize wanafunzi for january

Waziri alikuwa anamtafuta muda mrefu may be, kapata timing ya kumchinja
AWESO MPUMBAVU, LIMBUKENI NA MTAFUTA SIFA KWENYE MEDIA. MSIMWAMINI HUYU MSANII HATA SIKU 1
 
Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemteua Mhandisi Mariam Majala kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Ufundi, RUWASA, kabla ya uteuzi huo Majala alikuwa Meneja wa RUWASA mkoa wa Simiyu na amemteua pia Mhandisi Abbas Pyarali kuwa Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Usanifu na Usimamizi wa Miradi ya Maji Wizara ya Maji, awali alikuwa Mhandisi Mkuu katika Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Wizara ya Maji.
Majala awe makini na huyo kiumbe, soon naye atamwambia mumewe aendelee na utawala binafsi majukumu yamemzidi
 
1000005837.jpg
 
Huyo Mkurugenzi alipewa nafasi ya kueleza kilichofanya asifike Hanang? Kwanini tuwakomoe watu na tuingeze majanga juu ya majanga?
Watu wengine wameichoka miamri.. anaamua kujikalia home wafanye watakalo..
 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuondoa kwenye nafasi yake Mkurugenzi wa Sehemu ya Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa, Mhandisi Mashaka Sitta baada ya Mhandisi Sitta kutotimiza vema majukumu yake katika eneo hili muhimu la uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa na usimamizi wa mitambo na zaidi kutofika Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara baada ya kutokea changamoto ya mafuriko
Kwani waliofika walifanya nn? Kazi ya kiongozi ni kuratibu, kupanga pamoja na kuwezesha kazi kufanyika.

Hizi ni kiki tu za huyu mdudu anayeitwa Aweso. Pambaafu!
 
Back
Top Bottom