Serikali: Madalali kupewa vitambulisho maalumu kwa Ada ya tsh 20,000. Dalali atalipwa na mwenye nyumba tu siyo Mpangaji

Unalinganisha nyumba ya kuishi mtu na familia yake na Taxi ya Uber/bolt ambayo unapanda na kushuka muda mfupi baada ya kufika unakoenda? Nyumba ya kuishi mtu na mkewe na watoto wanaosoma chekechea, msingi na sekondari ina attributes nyingi zaidi. Fanya utafiti kwanza kabla hujaandika
Ila kwanini asitokee mtu akatengeneza APP Tanzania nzima wenye nyumba wakawa wanaweka detail zao wanakatwa percent kidogo na watu wakawa waningia humo kutafuta nyumba mbona uber na bolt zimesaidia au nakosea wakuu... Sijui
 
Nilishawahi kuandikaga hii idea humu! Its very possible na itasaidia si tu kwa ku eliminate madalali wanyonyaji bali itapunguza usumbufu wa hali ya juu wa utaftaji nyumba hasa ikiwa on-hand app tu kwenye simu!

Unaangalia nyumba ambako ziko available kwa kanda unayotaka kwenda aidha kinondoni ama Ilala ama Temeke. Unachagua price range na nyumba pia ziwe ranked kwa stars. Kuanzia 5 stars mpaka 1 star house kulingana na ubora!

Ikuletee exactly nyumba unayohitaji kwa price range na ubora!
Utaitengeza mwisho wasiku utabaki nayo mswahili ni mgumu sana kubadilika Watu wanaishi kwa Mazoe wanapenda mifumo umiza

gharama za kutengeza App ku update hosting matangazo kodi ni kubwa sana sio kwa bongo
 
Yep ni changamoto, lakini kwa kuanzia simple app ya kuunganisha kwa simu au email kati ya wenye nyumba,madalali na wateja inaweza kusaidia na kubadilisha mawazo ya watu na kuanza kutumia technology kwenye mambo ya nyumba
 
Ni jambo jema kabisa.Lakini bila kuwa na sheria, dalali au mwenye nyumba ataepuuza agizo au amri hii atashiughulikiwa vipi?

Haya ndio yale ya kutanguliza mkokoteni mbele kisha ng'ombe/punda ndio anafuata.
Bila sheria atakuja. Mpuuzi mwingine na tamko lake watu tukatafutana
 
Hii sekta ilikua imesahaulika walivyoshtuka wanaimpose vitu heavy, naishauri serikali iwe na balance kwa wadau wote wanaohusika, mmoja asi feel anaumizwa na system

Madalali wapewe nafasi hata kama hawajasoma, ni sekta muhimu Watanzania, maskini wengi.

Ulaya unampigia simu mwenye nyumba unalipa deposit labda ya mwezi mmoja. Dalali unampa ikizidi sana alisimia moja ya kodi ya 6, 1 year. Dili.

Madalali wote wawekwe kwenye mfumo rasmi walipe kodi rafiki. Sio za kuwaumiza.

Ndio taifa litavyoweza kujitegemee kila mtu mwenye uwezo alipe kwa uwezo wake.

Tusitegemee misaada kwa bajeti yetu.
 
Waziri Lukuvi amesema kuanzia sasa Madalali wa nyumba na viwanja watapewa vitambulisho maalumu kwa ada ya tsh 20,000 kila mwaka na watasajiliwa na halmashauri za wilaya

Lukuvi amesema dalali atalipwa na mwenye nyumba tu na siyo mpangaji kama inavyofanyika sasa ambapo mwenye nyumba na mpangaji huwalipa madalali.

Source: ITV habari
Hii itasaidia maana wanachangia sana kupanda bei ya vyumba mjini nyumba yenye hadhi ya 50000 utaambiwa 150000 ili apate pakubwa
 
Unalinganisha nyumba ya kuishi mtu na familia yake na Taxi ya Uber/bolt ambayo unapanda na kushuka muda mfupi baada ya kufika unakoenda? Nyumba ya kuishi mtu na mkewe na watoto wanaosoma chekechea, msingi na sekondari ina attributes nyingi zaidi. Fanya utafiti kwanza kabla hujaandika
Attributes zinakuwaje nyingi kama utazi class?

-Size (single room, single-self room, self room+ Lounge,self room +lounge+ Kitchen, self room+extra room+lounge+kitchen)

-Amenities(Alluminium profile, Parking, Electricity,Water,Fence, Perving,None)

-Price range (30K, 50K, 80K, 100K,130K,150K,180K,200K,250K, 300K, 350K n.k)

-Region(Kinondoni, Ilala,Temeke)

-Residence (Tabata, Segerea,Magomeni,Masaki,Mbezi Beach,Kawe,Sinza,Kimara,Goba, Salasala,Mbweni,Bunju,Mwananyala, Makumbusho,Tandale,Mbagala,Tandika, Mtongani,Kijichi)

Duration: (1 months, 3 months, 6 months, 12 months)

Hapo bado tu hujapata picha tu?

Uki press button ya search inakuletea nyumba ambazo ziko “Available” hizi ambazo unaweza kulipia kwa list toka kwenye eneo ulilochagua.

“Taken” ambazo zimeshalipiwa.

“Pending/Due” ambazo wenyewe wameshatoa taarifa kwamba wanaplan kuachia one month ahead!

How it works, wenye nyumba watakuwa na section yao kwenye huu mfumo. Wata feed hizo taarifa na picha clear za nyumba zao na wataweka na contacts zao.

Revenue model:
Subscription, mwenye nyumba atalazimika ku subscribe kwenye mfumo kila mwaka subscription fees kwa mwanzo itakuwa free ila wakizoea tutaweka tozo.

Adverts:
Mwenye nyumba atachangia 3% toka katika pesa ya kila nyumba ambayo atapangisha kupitia mfumo huu. Hii inakuwa sasa ndio gharama za udalali ambazo atatulipa wenye kampuni yetu na app.
 
Hivi kweli tunalitakia mema taifa? unawezaje kuhalalisha uhuni kama huu kwenye taifa letu? udalali ni uhuni na kamwe haupaswi kuungwa mkono, walipane na mpangaji maana ndiyo wametafutana ila mwenye nyumba hapana.

haaa, mkuu udalali upo na unatambulika, kuna nchi nilienda huko nikawa natafuta nyumba ya kuishi
nikaelekezwa kwa makamission agents , nikawaambia bajeti yangu na nyumba ninayohitaji wakanionyesha kama kumi,
nikachagua moja nikawalipa hao madalali commision yao ambayo ilikuwa 10% ya monthly rent mi, nikawa naendelea kukomaa na land lord alikuwa anataka kodi yake kila mwezi (utaratibu kule kodi ya nyumba hizi ndogo (apartments) inalipwa kila mwezi).

Nina vi apartments vyangu navipangisha mara nyingi madalali wanaleta wapangaji, nitaendela na utaratibu wangu wa kawaida
wa kuwatoa hawa madalali ila sio kuwapa kodi ya mwezi 1 , atakuwa anakula kama kawaida 10% ya kodi ya mwezi.

serikali nayo inaingilia sana ishu ambazo si za lazima wala serious,
 
Madalali wapewe nafasi hata kama hawajasoma, ni sekta muhimu Watanzania, maskini wengi.

Ulaya unampigia simu mwenye nyumba unalipa deposit labda ya mwezi mmoja. Dalali unampa ikizidi sana alisimia moja ya kodi ya 6, 1 year. Dili.

Madalali wote wawekwe kwenye mfumo rasmi walipe kodi rafiki. Sio za kuwaumiza.

Ndio taifa litavyoweza kujitegemee kila mtu mwenye uwezo alipe kwa uwezo wake.

Tusitegemee misaada kwa bajeti yetu.
Na wapewe training hata ya week moja na kuwa certified kabla ya kuruhusiwa kufanya hizo kazi,wajue sheria za udalali, haki yao ,ya mwenye nyumba na ya mteja , uswahili na utapeli utapungua
 
Na wapewe training hata ya week moja na kuwa certified kabla ya kuruhusiwa kufanya hizo kazi,wajue sheria za udalali, haki yao ,ya mwenye nyumba na ya mteja , uswahili na utapeli utapungua

Ndio, ila yasiwe masharti magumu sana, wanaweza kupewa nafasi kupata ofisi, kujipanga, kujiendeleza miaka miwili. Sera zetu zote ziwe endelevu.
 
Back
Top Bottom