Serikali irudishe Tsh 20,000/= Ada ya sekondari kwa mwaka

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Kwema Wakuu!

Serikali inapaswa iirejeshe Ada kwa wanafunzi wanaosoma shule, nchi yetu bado hatujafikia nyakati za kutoa vitu bure,

Shule ya Msingi ndio iwe Bure lakini sekondari, wanafunzi watoe pesa,
Isiwe pesa kubwa Sana, iwe Tsh 20,000/= Kwa familia yenye watoto watano ni 100,000/= Kwa mwaka, nusu mhula 10,000/=

Raia wasipende Dezodezo, wasipende burebure Kwa kisingizio nchi ni Tajiri, hakunaga Utajiri Kwa watu wanapenda Dezo, wanaopenda vyabure.

Mimi sikubalianagi na Wanasiasa wanaohubiri kutoa vitu vya bure, unatoa vitu vya bure kwa misingi ipi, bure inafaa Kwa makundi maalumu ya watu Kama Walemavu lakini tofauti na hapo hakuna bure.

Watoto wanatoka shuleni mapema Kwa vile hawana kazi wanaishia mitaani vijiweni Kupiga Umbeya, kujadili vitu vya kipuuzi, wengine wanajiingiza kwenye madawa ya kulevya huku wasichana wakijitafutia mabwana Kwa sababu ya kukosa kazi watokaoo shuleni.

Wakati tunasoma wengine tumeshalima Sana vibarua, tumebeba Kago, tumeosha magari, tumeuza miwa na sambusa ili kupata pesa za kujikimu kuwasaidia wazazi ambao ni masikini.

Ndio wazazi wetu Sisi Kama watoto ilikuwa wajibu wetu kuwasaidia na sio kwenda vijiweni bila ya kazi alafu ukikosa Ada shuleni mnailaumu serikali.

Serikali lipisheni Ada na iwe ni lazima watoto waende shule,
Ada itasaidia mambo mengi, itawarahisishia mambo katika sekta ya elimu,

Masuala ya mishahara ya waalimu unaweza kusaidia, kuajiri waalimu wapya itasaidia, na miundombiny mingine katik sekta ya elimu.
Kila sekta inatakiwa iwe na uwezo wa kujitegemea ili Kupunguza utegemezi Kati ya sekta moja na nyingine.

Faida zingine za kurejesha Ada
1. Uzazi wa mpango utazingatiwa.
Tabia ya watu kuzaa bila mipango itapungua.
Maana kuna watu wanazaa bila mpango alafu watoto wanawatupia shuleni Kwa waalimu Asubuhi mtoto anaondoka hanywi hata chai anarudi jioni. Wanaichukulia shule Kama sehemu ya Kupunguza bajeti ya familia. Elimu sinibure bhana!

Moja ya mbinu ya kudhibiti ongezeko kubwa la watu lenye athari Hasi ni kupandisha gharama za maisha, ukiachia mbinu zingine Kama Elimu, propaganda, Maradhi n.k.

2. Kuondoa kasumba ya Kupenda burebure na utegemezi!
Kasumba ya uburebure ipo Kwa jamii masikini, mtoto tangu akiwa mdogo anasoma lazima aone wazazi wake na Yeye mwenyewe akiwajibika, hii itamfanya ayaelewe maisha Kwa upesi zaidi kuwa Maisha sio burebure.

Vile mtoto anavyosumbuliwa Ada au kufukuzwa Ada inamjengea fikra za majukumu, nyakati za jioni akirudi lazima ashiriki kazi za nyumbani za uzalishaji kama kilimo, ufugaji, au biashara ndogondogo kuwasaidia wazazi wake kwani anajua Kwa kufanya hivyo ni ili apate Ada asome.

Wazazi nao wawaambie watoto kuwa kazi wazifanyazo ndizo zinazolisha familia na kuwasomesha watoto, hii itafanya watoto waheshimu kazi kwani watakuwa wanashiriki kazi hizo.

Siku hizi ni nadra Sana kumkuta mtoto akimsaidia mzazi wake kazi za uzalishaji Mali awapo likizo au akitoka jioni shuleni Ile saa tisa, hasa huku mjini.

Mambo ya burebure yametengeneza Matoto ya burebure, kupenda vitu bila kutoa jasho, sio Kwa mabinti sio Kwa Vijana.
Mabinti yanapenda pesa za burebure Kwa vile yamelelewa hivyo, yaani kisa ni mwanamke ndio upewe bure hiyo ni Akili za jamii fukara.

Taikon mara zote nawaambiaga ukiona Msichana anapenda burebure kuomba pesa hata hajafanya kazi yeyote huyo ni Shetani chumaulete, ni aibu Kwa mtu mwenye akili timamu zenye kufanya kazi kuomba pesa au kukubali pesa ya burebure.
Halikadhalika na vijana.

Mambo haya yalisababishwa na ujamaa, mambo ya ujamaa tuachane nayo Kwanza.

3. Kizazi chenye kuwajibika na wachapakazi.
Huwezi ukazaa watoto ukitegemea serikali ikusomeshee watoto hao, huo ni uhuni. Ukizaa watoto wajibika Kwa watoto wako, wazazi wanachopaswa kuiomba serikali ni Kupunguza gharama na sio kuiondoa kabisa, huko ni kuipa serikali mizigo alafu baadaye unailaumu serikali Kwa nini inakopa.

Wazazi waelewe kuwa kadiri unavyozaa ndivyo unatakiwa kuzidi kuchapa Kazi zaidi na zaidi Kwa ajili ya familia yako. Sio uzae Matoto mengi alafu Ada utake bure alafu uanze kuilaumu serikali haijajenga madarasa, sijui haijaajiri waalimu WA kufundisha watoto wako, sijui shule haina vifaa huo ni ukichaa.

Wingi unamaana Kwa watu wenye akili, unaweza kuzaa watoto hata Mia moja lakini kama ni wazembe hawana maana yoyote zaidi ya kuleta mabalaa katika Dunia.

4. Watoto kuwa na uchungu wa shule.
Siku zote kitu cha Bure kamwe hakijawahi kuwa na thamani. Mtoto vile anavyoona wazazi wake wanahenyeka kumsomesha anapata hamasa ya kusoma zaidi ili kuwafurahisha wazazi wake.

5. Kuongeza Upendo wa mtoto Kwa wazazi.
Alafu jinsi ilivyo kadiri mzazi anavyohangaika kumsomesha mtoto Kwa nguvu kubwa ndivyo mtoto anavyoongeza mapenzi Kwa mzazi wake.

Wazazi wanaopenda mambo ya burebure husababisha watoto wao wasiwachukulie Sirius Sana ukilinganisha na wazazi waliomenyeka kuwalea watoto wao(shule ikiwemo).

Ndio maana watoto wa Matajiri wanaupendo mara mbili Kwa wazazi wao tofauti na watoto wa masikini, kanuni inasema ukitoa kidogo utapendwa kidogo, ukitoa kikubwa utapendwa pakubwa.

Mzazi aliyemenyeka kuuza mitumba au pombe za kienyeji au vitumbua kisa kumsomesha mtoto, anapendwa zaidi na mtoto wake kuliko mzazi ambaye hakufanya jitihada yoyote zaidi ya kuitupia serikali asome mtoto bure Kwa kisingizio cha umasikini. Upendo hauna kisingizio.

Serikali inachopaswa kufanya ni kuweka gharama ndogo zinazoendana na Watanzania waliowengi na sio kuondoa kabisa Ada katika shule za sekondari.

Tuache kulipia Ada za Shule ikifika mwaka 2200 huko Nchi ikiwa imeendelea,
Sio sasa Waalimu hawatoshi, hakuna vifaa, hakuna miundombinu.

Hao wanaotoa elimu bure walimenyeka miaka iliyopita,
Vinginevyo tuvamie mataifa mengine Kama nilivyowahi kusema.

Nawatakia maandalizi Mema ya SABATO
 
ILI KUWEZA KUPATA KURA ZA WANAWAKE UCHAGUZI WA MWAKA 2015 IKABIDI WATEUE MGOMBEA MWENZA MWANAMKE ILI KUZIPATA KURA HIZO KWA URAHISI.

WAKASAHAU KUWA KUNA KESHO NA YULE WALIEMTEUA HAWAKUJUA AU KWA KUJUA KUWA HATOSHI KABISA KUWA RAISI LIKITOKEA LA KUTOKEA.

WOTE WALIOSHIRIKI MCHAKATO ULE WALAANIWE WAO NA KIZAZI CHAO HADI CHA NNE.
 
Sijui Kama ulichoandika unakielewa vizuri. Nchi zenye uchumi imara karibu zote hutoa huduma za kijamii bure, Sasa tuseme na wao wanaupenda umaskini?

Mara kadhaa humu watu wanasifi nchi za ulaya kuwa elimu kuanzia kindergarten hadi chuo kikuu ni bure. Sasa sijui na wao tusemaje
Huko wameenda mbali wana hadi package kwa wale ambao ni unemployed.
 
Nakubaliana. Hii bure ni gharama kwani pesa za serikali huchelewa kupelekwa shuleni au hupelekwa kidogo. Naamini wazazi wamelea mtoto kwa gharama kubwa hawezi shindwa ada ya elf 20 au hata 40 kwa mwaka.
Wenzetu sijui mnavichwa vya aina gani. Serikali haichelewi kupeleka pesa shuleni bali sehemu nyingi tu na hio Ni sababu ya urasimu, na hapo wanaofanywa urasimu wanapaswa kuwajibishwa.

Leo unataka watu walipe 20000, Ila ukisikia Kuna kikundi Cha watu wamechukua bil 200 unaona sawa? Nchi zote tunazotamani tuwe Kama wao, huduma za kijamii ni bure.
 
ILI KUWEZA KUPATA KURA ZA WANAWAKE UCHAGUZI WA MWAKA 2015 IKABIDI WATEUE MGOMBEA MWENZA MWANAMKE ILI KUZIPATA KURA HIZO KWA URAHISI...
Bajeti ya kilimo imeongezwa toka 200b to 700b kwa 2022/2023.Tayari nami nimeongeza heka 50 fasta.Mama kwa hakika anajua wapi tulikwama.

Kwa mama mi 5 tena.
 
Sijui Kama ulichoandika unakielewa vizuri. Nchi zenye uchumi imara karibu zote hutoa huduma za kijamii bure, Sasa tuseme na wao wanaupenda umaskini?

Mara kadhaa humu watu wanasifi nchi za ulaya kuwa elimu kuanzia kindergarten hadi chuo kikuu ni bure. Sasa sijui na wao tusemaje
Huko wameenda mbali wana hadi package kwa wale ambao ni unemployed.

Sio Kwa nchi Masikini Kama yetu.

Angalia historia za nchi hizo utaelewa nazungumzia nini
 
Wenzetu sijui mnavichwa vya aina gani. Serikali haichelewi kupeleka pesa shuleni bali sehemu nyingi tu na hio Ni sababu ya urasimu, na hapo wanaofanywa urasimu wanapaswa kuwajibishwa.

Leo unataka watu walipe 20000, Ila ukisikia Kuna kikundi Cha watu wamechukua bil 200 unaona sawa? Nchi zote tunazotamani tuwe Kama wao, huduma za kijamii ni bure.
Uchumi wetu unaweza kuhimili huduma za kijamii bure? Hata hiyo elf 20 ni mchango tu sio kwamba ni ada toshelevu!
 
Mkuu lipa kwanza deni lako la helsb
Kwema Wakuu!

Serikali inapaswa iirejeshe Ada kwa wanafunzi wanaosoma shule, nchi yetu bado hatujafikia nyakati za kutoa vitu bure,

Shule ya Msingi ndio iwe Bure lakini sekondari, wanafunzi watoe pesa,
Isiwe pesa kubwa Sana, iwe Tsh 20,000/= Kwa familia yenye watoto watano ni 100,000/= Kwa mwaka, nusu mhula 10,000/=

Raia wasipende Dezodezo, wasipende burebure Kwa kisingizio nchi ni Tajiri, hakunaga Utajiri Kwa watu wanapenda Dezo, wanaopenda vyabure.

Mimi sikubalianagi na Wanasiasa wanaohubiri kutoa vitu vya bure, unatoa vitu vya bure kwa misingi ipi, bure inafaa Kwa makundi maalumu ya watu Kama Walemavu lakini tofauti na hapo hakuna bure.

Watoto wanatoka shuleni mapema Kwa vile hawana kazi wanaishia mitaani vijiweni Kupiga Umbeya, kujadili vitu vya kipuuzi, wengine wanajiingiza kwenye madawa ya kulevya huku wasichana wakijitafutia mabwana Kwa sababu ya kukosa kazi watokaoo shuleni.

Wakati tunasoma wengine tumeshalima Sana vibarua, tumebeba Kago, tumeosha magari, tumeuza miwa na sambusa ili kupata pesa za kujikimu kuwasaidia wazazi ambao ni masikini.
Ndio wazazi wetu Sisi Kama watoto ilikuwa wajibu wetu kuwasaidia na sio kwenda vijiweni bila ya kazi alafu ukikosa Ada shuleni mnailaumu serikali.

Serikali lipisheni Ada na iwe ni lazima watoto waende shule,
Ada itasaidia mambo mengi, itawarahisishia mambo katika sekta ya elimu,

Masuala ya mishahara ya waalimu unaweza kusaidia, kuajiri waalimu wapya itasaidia, na miundombiny mingine katik sekta ya elimu.
Kila sekta inatakiwa iwe na uwezo wa kujitegemea ili Kupunguza utegemezi Kati ya sekta moja na nyingine.

Faida zingine za kurejesha Ada
1. Uzazi wa mpango utazingatiwa.
Tabia ya watu kuzaa bila mipango itapungua.
Maana kuna watu wanazaa bila mpango alafu watoto wanawatupia shuleni Kwa waalimu Asubuhi mtoto anaondoka hanywi hata chai anarudi jioni.
Wanaichukulia shule Kama sehemu ya Kupunguza bajeti ya familia. Elimu sinibure bhana!

Moja ya mbinu ya kudhibiti ongezeko kubwa la watu lenye athari Hasi ni kupandisha gharama za maisha, ukiachia mbinu zingine Kama Elimu, propaganda, Maradhi n.k.

2. Kuondoa kasumba ya Kupenda burebure na utegemezi!
Kasumba ya uburebure ipo Kwa jamii masikini, mtoto tangu akiwa mdogo anasoma lazima aone wazazi wake na Yeye mwenyewe akiwajibika, hii itamfanya ayaelewe maisha Kwa upesi zaidi kuwa Maisha sio burebure.
Vile mtoto anavyosumbuliwa Ada au kufukuzwa Ada inamjengea fikra za majukumu, nyakati za jioni akirudi lazima ashiriki kazi za nyumbani za uzalishaji kama kilimo, ufugaji, au biashara ndogondogo kuwasaidia wazazi wake kwani anajua Kwa kufanya hivyo ni ili apate Ada asome.

Wazazi nao wawaambie watoto kuwa kazi wazifanyazo ndizo zinazolisha familia na kuwasomesha watoto, hii itafanya watoto waheshimu kazi kwani watakuwa wanashiriki kazi hizo.

Siku hizi ni nadra Sana kumkuta mtoto akimsaidia mzazi wake kazi za uzalishaji Mali awapo likizo au akitoka jioni shuleni Ile saa tisa, hasa huku mjini.

Mambo ya burebure yametengeneza Matoto ya burebure, kupenda vitu bila kutoa jasho, sio Kwa mabinti sio Kwa Vijana.
Mabinti yanapenda pesa za burebure Kwa vile yamelelewa hivyo, yaani kisa ni mwanamke ndio upewe bure hiyo ni Akili za jamii fukara.
Taikon mara zote nawaambiaga ukiona Msichana anapenda burebure kuomba pesa hata hajafanya kazi yeyote huyo ni Shetani chumaulete, ni aibu Kwa mtu mwenye akili timamu zenye kufanya kazi kuomba pesa au kukubali pesa ya burebure.
Halikadhalika na vijana.

Mambo haya yalisababishwa na ujamaa, mambo ya ujamaa tuachane nayo Kwanza.

3. Kizazi chenye kuwajibika na wachapakazi.
Huwezi ukazaa watoto ukitegemea serikali ikusomeshee watoto hao, huo ni uhuni.
Ukizaa watoto wajibika Kwa watoto wako, wazazi wanachopaswa kuiomba serikali ni Kupunguza gharama na sio kuiondoa kabisa, huko ni kuipa serikali mizigo alafu baadaye unailaumu serikali Kwa nini inakopa.

Wazazi waelewe kuwa kadiri unavyozaa ndivyo unatakiwa kuzidi kuchapa Kazi zaidi na zaidi Kwa ajili ya familia yako. Sio uzae Matoto mengi alafu Ada utake bure alafu uanze kuilaumu serikali haijajenga madarasa, sijui haijaajiri waalimu WA kufundisha watoto wako, sijui shule haina vifaa huo ni ukichaa.

Wingi unamaana Kwa watu wenye akili, unaweza kuzaa watoto hata Mia moja lakini kama ni wazembe hawana maana yoyote zaidi ya kuleta mabalaa katika Dunia.

4. Watoto kuwa na uchungu wa shule.
Siku zote kitu cha Bure kamwe hakijawahi kuwa na thamani.
Mtoto vile anavyoona wazazi wake wanahenyeka kumsomesha anapata hamasa ya kusoma zaidi ili kuwafurahisha wazazi wake.

5. Kuongeza Upendo wa mtoto Kwa wazazi.
Alafu jinsi ilivyo kadiri mzazi anavyohangaika kumsomesha mtoto Kwa nguvu kubwa ndivyo mtoto anavyoongeza mapenzi Kwa mzazi wake.

Wazazi wanaopenda mambo ya burebure husababisha watoto wao wasiwachukulie Sirius Sana ukilinganisha na wazazi waliomenyeka kuwalea watoto wao(shule ikiwemo).

Ndio maana watoto wa Matajiri wanaupendo mara mbili Kwa wazazi wao tofauti na watoto wa masikini, kanuni inasema ukitoa kidogo utapendwa kidogo, ukitoa kikubwa utapendwa pakubwa.
Mzazi aliyemenyeka kuuza mitumba au pombe za kienyeji au vitumbua kisa kumsomesha mtoto, anapendwa zaidi na mtoto wake kuliko mzazi ambaye hakufanya jitihada yoyote zaidi ya kuitupia serikali asome mtoto bure Kwa kisingizio cha umasikini. Upendo hauna kisingizio.

Serikali inachopaswa kufanya ni kuweka gharama ndogo zinazoendana na Watanzania waliowengi na sio kuondoa kabisa Ada katika shule za sekondari.

Tuache kulipia Ada za Shule ikifika mwaka 2200 huko Nchi ikiwa imeendelea,
Sio sasa Waalimu hawatoshi, hakuna vifaa, hakuna miundombinu.

Hao wanaotoa elimu bure walimenyeka miaka iliyopita,
Vinginevyo tuvamie mataifa mengine Kama nilivyowahi kusema.

Nawatakia maandalizi Mema ya SABATO
 
umewaza vizuri sana kuchangia elimu ni jambo ambalo halihitaji mjadala ni muhimu sana,,shule zinajiendesha kwa kusuasua ruzuku inayotolewa haitoshi kuziendesha shuele na kupata matokeo makubwa

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini usiilipe wewe kwa niaba ya Wanafunzi kama inakuuma hivyo ? Unaonea wivu hata watoto yatima wanaojitahidi kujikomboa ? Hata hicho kidogo unataka wanyang‘anywe pia ? Hiyo Ni psyochopathy!
 
Sio Kwa nchi Masikini Kama yetu.

Angalia historia za nchi hizo utaelewa nazungumzia nini
Huenda hujakisoma ulichoandika. Umesema kasumba burebure ipo kwa maskini, nikakuambia mbkna nchi tajiri ndio zinaongoza kwa kutoa hizo huduma burebure?

Unasema Watoto wakisoma bure wanakosa uwaajibikaji na uchapakazi, huko wanaposoma bure hakuna uwajibikaji na uchapakazi?
Tulikuwa tunalipia elimu, je tuliwahi kuwa na huo uwajibikaji na uchapakazi??
 
Uchumi wetu unaweza kuhimili huduma za kijamii bure? Hata hiyo elf 20 ni mchango tu sio kwamba ni ada toshelevu!
Nimemjibu kutokana na sababu alizosema huyo kuwa kasumbaa ya burebure ipo kwa maskini ndio nikamtolea mfano wa nchi ambazo ni tajiri.

Unasema uchumi wa nchi yetu hauwezi kuhimili huduma za kijamii bure? Ila unaweza kuhimili kila mwaka wa fedha upotevu wa mabilion ya pesa kukwapuliwa?
 
umewaza vizuri sana kuchangia elimu ni jambo ambalo halihitaji mjadala ni muhimu sana,,shule zinajiendesha kwa kusuasua ruzuku inayotolewa haitoshi kuziendesha shuele na kupata matokeo makubwa

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
Swali langu linarudi palepale, hatuwezi kuendesha shule kwa ruzuku Ila hapo hapo kila mwaka mabilioni ya pesa yanaibwa. Kipi ni rahisi hapo kufanya? Kudhibiti hayo mabilioni yasiibiwe au kutoa hiyo ruzuku ya elimu bure?
 
Back
Top Bottom