Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,001
- 9,866
SERIKALI imesema itaangalia namna ya kuwapa mtaji vijana wanaohitimu mafunzo katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili ujuzi wanaoupata usipotee badala yake wakautumie uraiani.Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajab Mabele,akimuonyesha ghala la kuhifadhia chakula waziri wa Ulinzi Elius Kwandika mwenye kofia la pama.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kwandika wakati akikagua mradi wa Skimu ya Umwagiliaji iliopo kikosi cha 837 Chita JKT,kinachoendesha kilimo cha Mpunga na Ufugaji wa Samaki katika mabwawa.
Kwandika, amesema wanaangalia namna ya kuwapa mitaji kwenye vikundi ili kile walichojifunza wakakitumie katika kujiajiri badala ya kutegemea ajira za serikali.
Amesema vijana hao wanapata mafunzo ya kutosha na yenye kuwajenga ambayo wanaamini wakihitimu mafunzo wanakuwa vijana bora wa mfano wa kuigwa katika kila nyanja.
“Tunaangalia namna ya kuwawezesha vijana lengo letu ni kuona vijana ujuzi wao haupotei,” amesema Kwandika.
Mbali na hilo Kwandika amewaagiza wananchi kutumia mashamba ya kilimo mkakati ya (JKT) kama shamba darasa kwa ajili ya kukuza sekta ya kilimo hapa nchini.
NIPASHE