Serikali kuwaondoa Walimu kwenye sensa, sasa kuwatumia Wanavyuo!

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Wana JF baada ya walimu kugoma na kutotii Amri ya Serikali, sasa Serikali inajiandaa kutangaza nafasi za Maafisa watakaohesabu watu (sensa) badala ya kuwatumia Waalimu sasa kuwatumia wana vyuo.

Hii imetokana na walimu wengi kupanga hujuma ya kuvuruga sensa wakishinikiza madai yao, mpango unakaribia kukamilika na utatangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Source: Mmoja wa ma afisa wa juu wa takwimu
 
Wana JF baada ya walimu kugoma na kutotii Amri ya Serikali,sasa Serikali inajiandaa kutangaza nafasi za Maafisa watakaohesabu watu(sensa)badala ya kuwatumia Waalimu sasa kuwatumia wana vyuo,hii imetokana na walimu wengi kupanga hujuma ya kuvuruga sensa wakishinikiza madai yao,mpango unakaribia kukamilika na utatangazwa punde
Source:mmoja wa ma afisa wa juu wa takwimu

Acha utani weweee...unajua imechukua siku ngapi na gharama gani kuwatrain hao makarani wa sensa? Zimebaki wiki 3 tu sensa ifanyike...we dont afford to train a new team!
 
Hii kitu haiwezekani tayari mafunzo yameshatolewa kwa walimu hao hao. Mpaka sasa muda umebaki mchache lzm watawatumia walimu kwani walioko vyuo mpaka wapate ujuzi ni leo?
 
Labda wanavyuo wa ccm,binafsi siwezi kukubali mateso wanayopata walimu wangu kuwa fursa ya kujiingia kipato.
 
Wana JF baada ya walimu kugoma na kutotii Amri ya Serikali,sasa Serikali inajiandaa kutangaza nafasi za Maafisa watakaohesabu watu(sensa)badala ya kuwatumia Waalimu sasa kuwatumia wana vyuo,hii imetokana na walimu wengi kupanga hujuma ya kuvuruga sensa wakishinikiza madai yao,mpango unakaribia kukamilika na utatangazwa punde
Source:mmoja wa ma afisa wa juu wa takwimu

Kama waalimu walikuwa potential sasa hao wengine wataweza kweli?!
 
Acha utani weweee...unajua imechukua siku ngapi na gharama gani kuwatrain hao makarani wa sensa? Zimebaki wiki 3 tu sensa ifanyike...we dont afford to train a new team!

Usimsikilize huyo...kipolo cha ubwabwa kinaweza kikawa kinamchanganya ahsubuhi hii...
 
Sidhani kama hili litawezekana. Hivi wanavyuo wamekuwa wazuri leo? Mbona hata huk vyuoni walimu wapo wengi tu? Kama kweli ni hivyo basi, inamaana serikali yetu haitaki kujishughulisha na kutatua huu mgogoro huu wa waalimu. Maana hapo wameona sensa ndiyo ya muhimu kuliko kuwafundisha vijana wetu.
 
Bora hata maana hzo nafasi 2ngezkosa jaman
Ubinafsi unapoingilia uwezo wa kuitafakari hali halisi ni hatari. Wahenga walisema "ukiona mwenzio ananyolewa wewe Tia maji"....naona unachekelea wakati "mwenzio" anapata "kiwembe" wakati anauefuata "kunyolewa" ni wewe
 
Hii kweli ni serikali inayofikiri kichwa ni kwaajili ya kufungia/kuotesha nywele tu.

Walimu wamesema wazi mgomo wao hauhusika na zoezi la sensa, kwani sensa wao wanachukulia kama party time job ya kuwaongezea kipato.

Kama kweli ni hivyo kwanini serikali isiondoa majina yote ya KIISLAMU kwenye maofisa wa sensa, kwasababu WAISLAMU WOTE wameadhimia kususia sensa, na ma T-shirt na vipeperushi vya kuhamasisha waislamu kutoshiriki sensa vinasambazwa. Je kati ya Walimu na Waislamu nani enemy wa sensa? Be juror yourself.


Huyu JK ana akili gani? No wonder kale ka-mama ka-Malawi nako kameanza kumuchezea masaburi eti kanadai Ziwa lote la Nyasa ni mali ya Malawi!
 
sijui hata waliishia wapi!!! ila sijajuia hao wanachuo watakao tumiwa in walw wa UVCCM au wote???
yaani wewe mwanamke post zako zinachefua hasa..HIVI sensa na siasa wapi na wapi?

Hebu toa ukereketwa kwenye issue za msingi .
 
Kweli walimu ni jalala, kwanza wanakatwa asilimia 3 ya mshahara kulipia bima ya afya ambayo ukipiga mahesabu vizuri ni heri wangeingia kwenye hizi scheme zingine

Pili the only ever time they atleast get to have an allowance is during census...na hawajaigomea hata hiyo sensa

Ndio hivyo tena wasubiri miaka 10...

Hebu serikali acheni kuwakandamiza hawa duni kuliko kwenye ajira za serikali waachieni wafanye hiyo sensa
 
Back
Top Bottom