Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Kwani ukarabati wa Lupaso utaisha lini? Tangu mwaka 2023 Serikali iliposaini mkataba wa Bilioni 30 mpaka leo bado mambo hayaeleweki.
Serikali imetangaza kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa utafungwa kwa ajili ya ukarabati wa mwisho kuanzia mwezi huu (Machi, 2026) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, wakati wa mahojiano na gazeti la The Citizen.
Msigwa amesema hatua ya mwisho ya ukarabati itahusisha maboresho ya nyasi za uwanja pamoja na maeneo mengine muhimu, na inatarajiwa kuchukua kati ya miezi sita hadi mwaka mmoja.
Amesema ukarabati huo ukianza, uwanja hautapatikana kwa michezo yoyote, hivyo kama ratiba za mechi zitakamilika kabla ya kuanza kwa ukarabati zitaendelea kama ilivyopangwa, lakini vinginevyo timu zitalazimika kutafuta viwanja mbadala.
Kufungwa kwa uwanja huo ni hatua muhimu kwa soka la ndani, kwani Uwanja wa Benjamin Mkapa umekuwa ukitumika kama kituo kikuu cha michezo ya ligi na mashindano makubwa nchini.
Soma zaidi;

- Serikali yasaini mkataba wa Bilioni 30 kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa
- Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungwa, Yanga na Simba kutafuta viwanja vingine kwa mechi za Ligi na CAF
- Serikali yakamilisha ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Bilioni 31.3
- Maendeleo na gharama za viwanja vitakavyotumika katika Michuano ya AFCON 2027