Komredi Shemsa Mohammed Aitaka Serikali Kutenga Fedha Kukamilisha Miradi ya SEQUIP & BOOST Mkoani Simiyu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu kimeitaka serikali kutenga bajeti ili kukamilisha maboma ya zanahati, vyumba vya madarasa, nyumba za walimu ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo, Shemsa Mohammed wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Mbugabanhya na Mwandu Itinje wilayani Meatu katika ziara ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Amesema licha ya serikali kuendelea kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika sekta za Elimu na Afya, watendaji wanatakiwa kuendelea kutenge bajeti ili kukamilisha majengo yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.

‘’Pitieni Maboma yote yaliyojengwa kwa nguzu za wananchi ili myakamilishe, tengeni bajeti ili wananchi waone tija ya michango yao kuliko kuyatelekeza na kuanza ujenzi mpya’’ amesema na kuongeza.

‘’Rais Samia anatoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya, Zahanati, Shule za Msingi na Sekondari, Maabara na Mabweni lakini katika maeneo yetu kuna majengo yalichangiwa kwa nguvu za wananchi na hayajakamilika…tengeni bajeti kuyakamilisha.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk. Yahaya Nawanda amemhakikishia Mwenyekiti huyo kuwa watashirikiana na Halmashauri kuhakikisha wanatenga bajeti ili kukamilisha maomba hayo.

Akiwa wilayani Meatu, Mwenyekiti Shemsa amekagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari Mbugabanhya inayotekelezwa kwa gharama ya shilingi Mil. 584 kupitia Mradi wa SEQUIP.

Pia amekagua ujenzi wa shule ya mpya ya msingi Mwandu Ikindilo inayotekelezwa kupitia mradi wa BOOST kwa gharama ya shilingi Mil. 540 na kuipongeza serikali kwa kutoa fedha pamoja na usimamizi mzuri wa watendaji katika miradi hiyo ambayo imeonyesha thamani halisi ya fedha.

MWISHO

DSC_3318.JPG
DSC_3282.JPG
DSC_3319.JPG
DSC_3317.JPG
DSC_3297.JPG
DSC_3292.JPG
DSC_3290.JPG
DSC_3287.JPG
DSC_3283.JPG
 
Back
Top Bottom