Serikali kumfunga Sugu was a political mistake!

Serikali kumfunga Sugu was a political mistake!

Mimi ni mwana CCM, tena natembelea sana huko Mbeya.

Kwa kusema ukweli, kumfunga Sugu imemuongezea sana umaarufu.
Mbaya zaidi kitendo hicho hakijaiongezea CCM umaarufu kanda hii.

Sipendi viongozi wakitukanana hadharani, lakini thats part of politics, ila hi drastic action sana sana Sugu amejijengea public sympathy na mwishowe yeye ndo anaonekana kaonewa kisiasa.
Hiyo public sympathy inageuzwa kuwa political strength.

Tujifunze.
Amefungwa na mahakama. Kutukana hadharani (Kama kumethibitika mahakamani) si sehemu ya siasa n tusikubali iwe sehemu ya siasa.
 
Amefungwa na mahakama. Kutukana hadharani (Kama kumethibitika mahakamani) si sehemu ya siasa n tusikubali iwe sehemu ya siasa.

Bro, so you are saying rules are rules; even if the rule is "... akizini apigwe mawe mpaka afe". I thought you were a human rights advocate!
 
Amefungwa na mahakama. Kutukana hadharani (Kama kumethibitika mahakamani) si sehemu ya siasa n tusikubali iwe sehemu ya siasa.
Nisingependa kucheza na lugha au maudhui ya kosa lenyewe la Sugu kwa maana kosa linabaki kuwa kosa.
Na tukumbuke Sugu hakujipeleka mahakamani.
Kapelekwa huko na Serikali kwa kosa.
Argument yangu si kama kuna kosa au la, kosa lipo na mahakamani ni mahali pake.
Argument yangu ni wisdom ya kufanya hivyo, wakati kuna njia nyingi mbadala.
Humulity, busara na hekima ni vitu adimu, lakini hivi ndivyo vinahitajika kulingana na mazingira.
Sasa hivi kwa Mbeya mjini Sugu ni kama chura aliyepigwa teke, ameongezewa tu umaarufu wa kisiasa.

Huko Kenya, Odinga amejiapisha kuwa " rais wa wananchi".
Kosa kubwa hilo, na si tu kisiasa bali potentially treasonous, uhaini.

What did Rais Kenyatta do?
Nothing, absolutely nothing!
And that was a very clever move by Kenyatta.
Uvumilivu wake, busara na hekima paid off.
Sasa tunasikia huko Kenya wanapeana mikono.

Matusi kwenye siasa si jambo zuri, but heavy handedness is not either.
 
Ni kweli Jidulamambasi, Sugu ni MAARUFU kwa matusi hivyo kajiongezea umaarufu kufungwa jela kwa matusi !
 
Mimi ni mwana CCM, tena natembelea sana huko Mbeya.

Kwa kusema ukweli, kumfunga Sugu imemuongezea sana umaarufu.
Mbaya zaidi kitendo hicho hakijaiongezea CCM umaarufu kanda hii.

Sipendi viongozi wakitukanana hadharani, lakini thats part of politics, ila hi drastic action sana sana Sugu amejijengea public sympathy na mwishowe yeye ndo anaonekana kaonewa kisiasa.
Hiyo public sympathy inageuzwa kuwa political strength.

Tujifunze.

But Sugu alifungwa na Mahakama baada ya kumpata na hatia. Kama jela inaongeza umaarufu wake, angekataa kutoka bbaada ya kupata msamaha au ajichakate wamfunge tena umaarufu uzidi kuongezeka.

Mie naamini siasa za kistaarabu zitamfaa zaidi ili apate kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na umakini zaidi.
 
Siasa is a political chess game.
Kama mtu huoni steps tatu au nne mbele basi ndo una mmwagia jitu kama Sugu umaarufu asio stahili.
Alitukana nini, wengi wala hawajui.

Ni kweli kumfunga kumemwongezea umaarufu.
Na hili ni kikwazo kwa CCM kumwodoa pale kwa ushawishi.
 
Lema mwenyewe alifungwa..kama watavunja sheria kisha wataogopwa sijui litakuwa taifa la aina gani..yaani maana yake waachwe watukane watakavyo..si nchi itakuwa kilabu cha pombe za kienyeji
Hao watukanaji wako upande mmoja tu??
 
Hilo liko wazi kabisa!!

Hata baadhi ya wana-CCM hili limewaumiza.

Alafu mbona wapinzani wanatukanwa tu na kudhalilishwa kila siku majukwaani tangu wakati wa kampeni mpaka leo hii?

Na nani kila siku anakejeli wengine?

Nani aliita watoto wa masikini vilaza?

Nani aliita wasaidi wake wapumbavu hadharani?

Tabu sana kwakweli!!
Hao walioitwa Vilaza na wapumbavu ni upinzani?
 
Mfalme Suleiman aliombankitu adimu sana kwa Mungu.
Aliomba apewe hekima katika utawala wake.
Kutukanwa na kukaa kimya ndo hekima?Acheni kukariri mambo ya kijinga.Kwanini hamtumii nguvu kubwa kuhamasisha viongoz wenu waache kutumia lugha Kali zaid mnahamasisha wakitukana waachwe huru?
 
Kila jambo lina wakati wake kuna watu waliishika mbeya hatukutegemea kwamba watatolewa lakini wakati ukafika wakaondoka nchi hii kama upepo vile hugeuka kulingana na hali ya hewa.
 
Lema mwenyewe alifungwa..kama watavunja sheria kisha wataogopwa sijui litakuwa taifa la aina gani..yaani maana yake waachwe watukane watakavyo..si nchi itakuwa kilabu cha pombe za kienyeji
Lema alifungwa lini?

Kukaa Mahabusu kwa muda mrefu haina maana kuwa alifungwa. Actually, mfano wa Lema unaonyesha ni jinsi gani uonevu wa kisiasa unavyoendelea nchini.
 
Lema mwenyewe alifungwa..kama watavunja sheria kisha wataogopwa sijui litakuwa taifa la aina gani..yaani maana yake waachwe watukane watakavyo..si nchi itakuwa kilabu cha pombe za kienyeji
Unaweza toa shuhuda ya alichotukana au unashabikia tu ili uhesabiwe
 
Lema mwenyewe alifungwa..kama watavunja sheria kisha wataogopwa sijui litakuwa taifa la aina gani..yaani maana yake waachwe watukane watakavyo..si nchi itakuwa kilabu cha pombe za kienyeji
mtoa mada hana maana hiyo, yeye kaongelea hili swala in political world, not in legal grounds......ndio maana kasema hapendi au haitakiwi viongozi kutukanana public ila in polical career it's a total mess done by the rulling class, which adhere and Boost sugu political strength
 
Lema mwenyewe alifungwa..kama watavunja sheria kisha wataogopwa sijui litakuwa taifa la aina gani..yaani maana yake waachwe watukane watakavyo..si nchi itakuwa kilabu cha pombe za kienyeji
Mbona hawamfungi mkurugenzi wa matusi Lusinde? Maana mikutano yote ya Lusinde ni matusi tena makubwa ambayo yanadhalilisha jamii
Anaongea point moja waliyo baki yote ni kashfa na matusi
 
Yaliyopita SINDWELE tugange yajayo.....tupendane,tusaidiane,tushikamane tuipeleke nchi yetu mbele zaidi
 
sasa sijui hizi sheria zitakuwa na maana yeyote kama zitakua zinachagua..

Katiba yenyewe Inasema utekelezaji wa sheria usibague..

sasa sijui hapo mleta mada unatuambia nini??
 
Kutukanwa na kukaa kimya ndo hekima?Acheni kukariri mambo ya kijinga.Kwanini hamtumii nguvu kubwa kuhamasisha viongoz wenu waache kutumia lugha Kali zaid mnahamasisha wakitukana waachwe huru?

Jamani Sugu alitukana matusi gani?
Tusaidieni basi na sisi tusije ingia hatiani.
Yawekeni hapa.
 
Back
Top Bottom