Serikali Kujenga Standi ya Kisasa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya

Serikali Kujenga Standi ya Kisasa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

SERIKALI KUJENGA STANDI YA KISASA KATIKA HALMASHAURI YA WIRAYA YA RORYA​

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Serikali imepanga kujenga standi ya Kisasa katika Halmashauri ya wilaya ya Rorya ili kusaidia upatikana wa huduma za usafiri na kuongeza mapato katika Halmashauri hiyo.

Mhe. Dkt. Dugange ameyasema hayo wakati wa maswali na majibu wakati akijibu swali la Mhe. Jafari wambura Chege (Mb) mbunge wa Jimbo la Rorya aliyetaka kujua “Je, kuna mpango gani wa ujenzi wa stendi Wilayani Rorya ili kuongeza mapato ya Halmashauri.” katika Bunge la bajeti linaloendelea Jijini Dodoma.

”Serikali inatambua umuhimu wa Wananchi wa Rorya kuwa na Stendi ya Mabasi kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi. Kwa sababu hiyo, Serikali kupitia Halmashauri imetenga eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 10 katika Kijiji cha Mika na Nyasoko kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya Wilaya ya Rorya.” Mhe. Dkt. Dugange.

Amesema Halmashauri kupitia mapato ya ndani imetumia shilingi milioni 98 kujenga stendi ya muda katika Kijiji cha Mika ili kuwezesha wananchi kupata huduma ya stendi na kuongeza mapato ya halmashauri ya Rorya.

Ameongeza kuwa, Halmashauri imefanya mazungumzo ya awali na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) chini ya Wizara ya Fedha ili kuweza kutekeleza mradi huo wa Kimakakati.
 

Attachments

  • mfano.jpg
    mfano.jpg
    34.3 KB · Views: 39
  • GoGEeELXUAAhtuz.jpg
    GoGEeELXUAAhtuz.jpg
    499.2 KB · Views: 31
Kuna bus gani inayoenda Rorya? Waste of money bila mipango. Stend tulizonazo zinatosha.
Next move iwe ni kuridisha Ada shuleni na huduma ya afya kuolewa bure.
 
Back
Top Bottom