jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,975
- 4,264
Serikali imesema kuwa itajenga daraja jipya mto Wami kwa kuwa Daraja linalotumika sasa ni dogo na limekuwa likisababisha usumbufu iwapo gari itaharibika katikati ya Daraja.
Ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 3.
=====
Bilioni 3/- kupanua daraja mto Wami
SERIKALI imetenga Sh bilioni tatu katika mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kuanza upanuzi wa daraja la mto Wami.
Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mgeni Jadi Kadika(CUF) aliyetaka kujua lini serikali itapanua daraja hilo.
Nganyani alisema Serikali inatekeleza mpango huo kwa sababu inatambua kuwa daraja la Wami katika barabara ya Chalinze- Segera ni kiungo muhimu kati ya Dar es Salaam, pwani, Morogoro na mkoa ya kaskazini mwa Tanzania.
Alisema, daraja hilo ambalo ni jembamba, lilijengwa miaka mingi iliyopita halikidhi mahitaji ya magari yanayopita kwenye barabara hiyo kwa sasa.
Kwa kuzingatia umuhimu huo, daraja hilo ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo serikali kupitia Wakala wa Barabara (Tanroads) imekamilisha kazi ya upembuzi.
Zabuni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja jipya la mto Wami zitaitishwa mwezi huu na tayari serikali imetenga fedha hizo.
Chanzo: Habari leo