Serikali Kufanya Mapitio ya Sera za Biashara Kwa Kuziboresha Kuwezesha Sekta Binafsi Kuchangia Uzalishaji Ajira Milioni 8- Waziri, Dr. Ashatu Kijaji

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
45,234
100,042
Wanabodi,
Nilihudhuria hii eventi
TotalEnergies Winners 1 first.jpg

Mshindi wa kwanza wa shindano la “STARTUPPER OF THE YEAR CHALLENGE BY TOTALENERGIES, Innocent Sule (mwenye Rasta ambaye picha yake pia inaonekana ukutani) wa kiwanda cha Soma Factories Tanzania Group ambao wanatengeneza mabegi ya shule yanye taa ya solar ya kusomea, kwa kutumia malighafi ya vitu vilivyotumiki ambavyo vingetupwa kama uchafu, akipokea zawadi yake ya hundi ya shilingi milioni 20, kutoka TotalEnergies Tanzania. Mgeni rasmi ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji., Bw. Ali Gugu, Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano, Getrude Mpangile. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
TotalEnergies Winners 2 First.jpg

Mshindi wa pili shindano la “STARTUPPER OF THE YEAR CHALLENGE BY TOTALENERGIES, Costantine Edward (ambaye pia picha yake inaonekana ukutani) wa kampuni ya AgriLife ambayo inatengeneza chakula cha mifugo kwa kuzalisha wadudu wanaotunza mazingira kwa kula uchafu na kuzalisha mbolea na chakula cha mifugo chenye viini lishe vingi, akipokea zawadi yake ya hundi ya shilingi milioni 20, kutoka TotalEnergies Tanzania. Mgeni rasmi ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji., Bw. Ali Gugu, Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano, Getrude Mpangile. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
TotalEnergies Winners 3.jpg

Mshindi wa Mwanamke wa shindano la “STARTUPPER OF THE YEAR CHALLENGE BY TOTALENERGIES, Hellena Sailas wa kampuni ya Arena Recycling Industry ambaye anazalisha matofali ya ujenzi kwa kutumia taka ngumu za plastiki, anazisaga na kutengeneza matofali ya ujenzi ambayo ni rafiki kwa mazingira na hayapitishi maji akifafanua jambo kwa Mgeni rasmi ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji., Bw. Ali Gugu, Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano, Getrude Mpangile. Hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jiji Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Serikali Kufanya Mapitio ya Sera za Biashara Kwa Kuziboresha Kuwezesha Sekta Binafsi Kuchangia Uzalishaji Ajira Milioni 8- Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Ashatu Kijaji​

Serikali kuboresha mazingira ya biashara ili kuiwezesha sekta binafsi kuzalisha ajira mpya kuchangia uzalishshaji wa ajira mpya , milioni 8, hivyo itazifanyia mapitio sheria zote za biashara ili kuboresha zaidi mazingira ya kufanya nchini na kuiwezesha sekta binafsi kuzalisha ajira na kuchangia kukua kwa uchumi na kuongeza pato la taifa.

Ahadi hiyo imetolewa na jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Ashatu Kijaji, katika hafla ya kuwakabidhi zawadi za fedha taslimu Shilingi milioni 60, kwa washindi watatu wa kwanza wa shindano la ubunifu wa miradi kwa vijana wa Kitanzania, iliyofanyika jana usiku katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijjini Dar es Salaam.

Katika Hotuba ilityosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Ali Gugu, Waziri Kijaji amesema, sekta binafsi ndio injini ya uchumi wa taifa, hivyo serikali ya awamu ya 6, itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara ili wajasiriamali wadogo na wakati, nao wakuwe na kuzalisha kada ya mamilionea na mabilionea wazawa ambao watachangia katika uchumi wa taifa.

“ Sisi kama serikali ya Mama Samia, neno letu kubwa tunalosema, na tunaloendelea kusema, tuweke mazingira mazuri ya biashara nchini, tunafanya kila jitihada kuhakikisha wawekezaji waliopo nchini, wanafanyabiashara zao na uwekezaji wao, katika hali ya utulivu bila kuwa na kero ya kodi korofi ambazo zinafifisha utendaji wao, lengo la kufanya hivi ni kuhakikisha wanaongeza uzalishaji kukidhi soko la ndani na ziada kuuza nje”. Alisema Gugu.

“sisi serikali lengo letu kwa kuzingatia dira yetu ya 2025 ni kuzalisha ajira milioni 8, ili kutimiza lengo hili ni lazima kuishirikisha sekta binafsi, kwa serikali kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya biashara kwa kuzalisha ajira mpya” Alisema Gugu.

Ali Gugu, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies kwa shindano hilo, na kutoa zawadi za zaidi ya shilingi milioni 100, kati ya hizo, washindi watatu wa mwanzo, kila mmoja amepewa hundi ya shilingi 20 za Kitanzania kuboresha mitaji yao na kuwalea kwa mwaka mmoja kwa kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo, na kuwaangazia fursa za masoko.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies Tanzania, Jean-Francois Schoepp, mesema lengo la kampuni ya TotalEnergies, kudhamini wabunifu hao ni ili kuwajengea uwezo Watanzania. “TotalEnergy, haifanyi tuu biashara na kuzalisha faida, bali kuitumia faida hiyo inayopatikana, kuwajengea uwezo na wengine ili kuwainua Watanzania na kuliinua taifa kiuchumi.

Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano, Getrude Mpangile, aliwataja washindi hao ni Costantine Edward wa kampuni ya AgriLife ambayo inatengeneza chakula cha mifugo kwa kuzalisha wadudu wanaotunza mazingira kwa kula uchafu na kuzalisha mbolea na chakula cha mifugo chenye viini lishe vingi.

Mwingine ni Innocent Sule wa kiwanda cha Soma Factories Tanzania Group ambao wanatengeneza mabegi ya shule yanye taa ya solar ya kusomea, kwa kutumia malighafi ya vitu vilivyotumiki ambavyo vingetupwa kama uchafu.

Na wa tatu ni binti, Hellena Sailas wa kampuni ya Arena Recycling Industry ambaye anazalisha matofali ya ujenzi kwa kutumia taka ngumu za plastiki, anazisaga na kutengeneza matofali ya ujenzi ambayo ni rafiki kwa mazingira na hayapitishi maji.

Mpangile amesema kilo mmoja amepatiwa fedha taslim, Shilingi milioni 20 za Kitanzania kuboreshea mitaji yao, na watapatiwa mafunzo ya kulelewa kwa muda wa mwaka ,mmoja kuboresha biashara zao, na kupatiwa fura ya kutangaswa na kufunguliwa fursa za masoko.

Watanzania, ya 1,000 wameshiriki, kati ya hao, miradi 439 ndio ilikidhi vigezo, kati ya hiyo miradi 15 ikaingia fainali ndio wakapatikana hao washindi watatu. Shindano hilo la “STARTUPPER OF THE YEAR CHALLENGE BY TOTALENERGIES limefanyika katika nchi zaidi ya 36 barani Afrika.
Paskali
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom