Serikali kuajiri Maafisa 800 wa TAKUKURU ili wakapambane na mafisadi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
32,639
36,498
SERIKALI imesema kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), itaajiri maofisa 800 wenye taaluma mbalimbali kwa lengo la kwenda kudhibiti upotevu wa fedha za umma hasa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alisema maofisa hao watasambazwa maeneo mbalimbali nchini ili kukabiliana na vitendo vya rushwa katika miradi ya serikali inayotekeleza.

“Ninakiri kuwa kuna upungufu na ubadhirifu katika miradi mingi inayotekelezwa ikiwamo ile ya kimkakati, hivyo serikali imeamua kuongeza nguvu ili kudhibiti ubadhirifu huo kwa kuongeza maofisa hawa watakaotawanywa wilaya zote,”alisema.

Chanzo: Nipashe

My Take
Vijana msipotoka awamu hii ya Samia mjue ndio basi watakuja watu dizaini ya Rais wa Wanyonge harafu mtaona mtakavyoishia kuwa machinga .
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom