Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,922
- 5,626
EWURA
ambayo nddiyo seikali yenyewe imeshaamua kuhuisha mkataba huo. Yawezekana hata sisi tukipeleka objections watadai "walioafiki wameshinda" maana ndio watakaochukua maamuzi ya mwisho.
EWURA hawajaamua bado, ndo maana wametupa nafasi ya kutoa maoni yetu. EWURA wana kila sababu ya kulifanya jambo hili kwa ushirikiano na wananchi maana wasipowapa mkataba, basi ujue Megawati 100 zinapungua kwenye gridi ya taifa na hivyo lazima mgao utaanza mara moja. Lazima tushirikishwe ili baadae tusilalamike mgao ukianza au wakipewa mkataba mpya pia tusilalamike.
Binafsi nashauri serikali isihuishe mkataba, badala yake waongee nao ili mtambo wauziwe TANESCO (hapa tuwe makini tena na wapigaji) ili wauendeshe wenyewe. Huo mtambo unapaswa uuzwe kwa bei ya chini sana sababu ya depreciation. Mtambo wa IPTL ukiendeshwa na Tanesco itapunguza gharama za uzalishaji na bei ya umeme. Sasa kuna wanasiasa wakikosa hela ya mgao wakati huo mtambo utakapouzwa wataanza kelele zao.