Serikali ku-renew mkataba wa IPTL?

Kisu Cha Ngariba

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
22,135
48,821
0653e940588cb078b1c5e8a3430ed545.jpg

--------------

iparamasa said;

IPTL, ile kampuni inayoinyonya usiku na mchana Tanesco na ikakwapua pesa za Escrow, imeomba muda zaidi iendelee kuiuzia umeme Tanesco!

Kampuni hii inaomba leseni wakati nchi ikihangaika na mikataba ya hovyo ya makinikia, na serikali hii itapimwa kama kweli ina nia ya kuondoa unyonyaji sekta zote mpaka kwenye umeme na si makinikia tu.

Je, Magufuli atawapa leseni?

Je, wabunge watasemaje? Hasa wa CCM waliowafungia wenzao mpaka mwaka 2018?

IPTL pia haikuwahi kupewa mkataba wala kutetewa na UKAWA.
 
iptl si ndo escrow hii!!!!
naona kila anachopinga zitto kuna mtu anafanya kinyume chake hata kama watakuja kutoa povu baadae kuwa tunaibiwa..
 
Hawa jamaa wakiongezewa mkataba basi nitajua hii nchi ya wasengerema! Bahati nzuri tuna fursa ya kushawishi hawa jamaa wasiongezewe muda. Shime wote tutenge siku tupeleke barua zetu za kupinga kwa mkono, posta na EMS (mimi binafsi nitapeleka kwa mkono na DHL). Wanaharakati na wanasiasa mliowahi kukemea wizi huu wa mchana, hii ni nafasi yenu ya kuitisha mikutano na hata maandamano (Yuvisisimizi mnaweza kuruhusiwa na polisi) kupinga hawa mumiani kupewa nafasi nyingine ya kutuibia.

Na hapa ndo kuna kipimo cha rais wetu, hawa wezi wenye suti wakipewa tena mkataba basi tusisikie tena kelele za ufisadi. Kampuni hii imetudhalilisha kama nchi, imetuibia sana kupitia bei ya umeme ambayo haiingii akilini. Mim kama mwananchi, nipo radhi kukosa umeme kwa nyakati fulani au nyakati zote ili mradi mumiani kama IPTL na wengineo wameondoka ktk sekta ya umeme.
 
"tusipo rennyuu mkattabha tutarara giza, sasa kipi bora"
Huo ndio utakuwa utetezi wa ofisi namba moja.

Ni utabiri tu lakini.
 
Mjadala wa ESCROW kurudi upya....naliona hili. Suala la kurenew Mkataba wa IPTL hakika Magufuli hatokubali
 
DOWANS.....IPTL....ESCROW.....si walisema ni mitambo ya Lowassa na watampeleka mahakama ya mafisadi? wamebadili gea baharini?
 
Mkataba utaongezwa nawaambia, ccm ni ileile labda ishuke ingine kutoka mbunguni na hii iliyopo sasa ishukie kuzimu tena wasikutane japo hata kwa sekunde 5 kwani iliyotoka mbinguni nayo inaweza kubadilika kuwa shetani.
 
Hawa si ndio wana kashfa nyingi!?

Kwa hiyo Ewura ndio wanatuaminisha kuwa hakuna tatizo au? Je ni hao tu wanaomba na hawawapi makampuni mengine hafasi ya kutuma maombi au kwanini pia hakuna ushindani kwenye hili kama tenda?

Wangeandika kabisa kwa kirefu na kila kipengele ni kwa sababu gani wameamua kuwapa waendeleee, na pia kwa kuwalipa kiasi gani kutoka kwenye pesa za walipa kodi.
 
Notice imemalizia kwa kusema "Any comments or objections to the application should be submitted in writing to EWURA ......"
Tunachotakiwa kufanya sisi JF ni kuitaarifu Wizara husika au TANESCO wapeleke objection zao huko. Wasipopeleka au tukibaki kujadiliana sisi kwa sisi huku mitandaoni tutapigwa tena kwa IPTL kupewa extension.
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom