Serikali ku-renew mkataba wa IPTL?

Hawa si ndio wana kashfa nyingi!?

Kwa hiyo Ewura ndio wanatuaminisha kuwa hakuna tatizo au? Je ni hao tu wanaomba na hawawapi makampuni mengine hafasi ya kutuma maombi au kwanini pia hakuna ushindani kwenye hili kama tenda?

Wangeandika kabisa kwa kirefu na kila kipengele ni kwa sababu gani wameamua kuwapa waendeleee, na pia kwa kuwalipa kiasi gani kutoka kwenye pesa za walipa kodi.
Hapa nimekuelewa, maana sehemu kubwa huwa unasifia kila jambo ila kwa hili umelitendea haki.
Kifupi hii mitambo ingetaifishwa ili iwe chini ya TANESCO maana hawa jamaa wametupiga hela nyingi sana, natumai Mh. Rais atafanyia kazi ushauri wa Zitto kama alivyoshauri kipindi kile cha escrow
 
Mie nafikiri hii ni leseni ya kufanya shughuri zao sio mkataba umeongezwa.

Nafikiri wanahitaji leseni kuendesha shughuri zao nchini na si lazima wawe na mkataba na TANESCO
 
wakiongezewa mkataba kabda watakua na maelezo ya kutupatia vinginevyo sijui km nitaelewa mtu
 
EWURA
Hawa jamaa wakiongezewa mkataba basi nitajua hii nchi ya wasengerema! Bahati nzuri tuna fursa ya kushawishi hawa jamaa wasiongezewe muda. Shime wote tutenge siku tupeleke barua zetu za kupinga kwa mkono, posta na EMS (mimi binafsi nitapeleka kwa mkono na DHL). Wanaharakati na wanasiasa mliowahi kukemea wizi huu wa mchana, hii ni nafasi yenu ya kuitisha mikutano na hata maandamano (Yuvisisimizi mnaweza kuruhusiwa na polisi) kupinga hawa mumiani kupewa nafasi nyingine ya kutuibia.

Na hapa ndo kuna kipimo cha rais wetu, hawa wezi wenye suti wakipewa tena mkataba basi tusisikie tena kelele za ufisadi. Kampuni hii imetudhalilisha kama nchi, imetuibia sana kupitia bei ya umeme ambayo haiingii akilini. Mim kama mwananchi, nipo radhi kukosa umeme kwa nyakati fulani au nyakati zote ili mradi mumiani kama IPTL na wengineo wameondoka ktk sekta ya umeme.
ambayo nddiyo seikali yenyewe imeshaamua kuhuisha mkataba huo. Yawezekana hata sisi tukipeleka objections watadai "walioafiki wameshinda" maana ndio watakaochukua maamuzi ya mwisho.
 
Hawa jamaa wakiongezewa mkataba basi nitajua hii nchi ya wasengerema! Bahati nzuri tuna fursa ya kushawishi hawa jamaa wasiongezewe muda. Shime wote tutenge siku tupeleke barua zetu za kupinga kwa mkono, posta na EMS (mimi binafsi nitapeleka kwa mkono na DHL). Wanaharakati na wanasiasa mliowahi kukemea wizi huu wa mchana, hii ni nafasi yenu ya kuitisha mikutano na hata maandamano (Yuvisisimizi mnaweza kuruhusiwa na polisi) kupinga hawa mumiani kupewa nafasi nyingine ya kutuibia.

Na hapa ndo kuna kipimo cha rais wetu, hawa wezi wenye suti wakipewa tena mkataba basi tusisikie tena kelele za ufisadi. Kampuni hii imetudhalilisha kama nchi, imetuibia sana kupitia bei ya umeme ambayo haiingii akilini. Mim kama mwananchi, nipo radhi kukosa umeme kwa nyakati fulani au nyakati zote ili mradi mumiani kama IPTL na wengineo wameondoka ktk sekta ya umeme.

Ndugu yangu weee unajisumbua Bure.Naibu Waziri ndiye yule aliyetuingiza mkenge.Unategemea kuna kuturn back hapo wakati wapiganaji wamepewa ban ya miaka kumi oh sorry miezi kumi na hakuna rukhsa kusema hapana ,ukisema hapana tu utapigwa ban out!

Waache wale wakishashiba watanawa mikono
 
Heheee! Kuna wale waliokaririshwa kazi yao kuimba...ooh jamaa mchapa kazi, anachukia ufisadi, ding dong-ding dong. Aibu yenu hiyo, mko uchi mubashara kabisa! Baba yake ESQROW anapita mitaani anadunda, mnasemaje??? Iwe ni kuongeza mkataba au ku-renew leseni kama wengine wanavyodai, hii ni fursa ya kulitimua jini mnyonya ngawira za wabongo akwende zake.... Ukoo wa ESQROW mtadhubutuuu???
 
Tatizo Afrika wanaolalamika ni wale walioko nje ya geti, mathalan ukivutwa ndani tu,ewalaaah!! tumelogwa tangu zamani, tumebakiwa na pepo tu ambapo pia tunatapeliwa taratibu na manabii na mitume wa uongo! kazaneni wandugu!!
 
Notice imemalizia kwa kusema "Any comments or objections to the application should be submitted in writing to EWURA ......".
Sijui baba Jesca kaiona hiyo Notice? Asije tu kuunda tume nyingine baadae au kumtumbua MTU baada ya Mkataba kuwa renewed
 
IMG-20170607-WA0046.jpg

IPTL, ile kampuni inayoinyonya usiku na mchana Tanesco na ikakwapua pesa za Escrow, imeomba muda zaidi iendelee kuiuzia umeme Tanesco!

Kampuni hii inaomba leseni wakati nchi ikihangaika na mikataba ya hovyo ya makinikia, na serikali hii itapimwa kama kweli ina nia ya kuondoa unyonyaji sekta zote mpaka kwenye umeme na si makinikia tu.

Je, Magufuli atawapa leseni?

Je, wabunge watasemaje? Hasa wa CCM waliowafungia wenzao mpaka mwaka 2018?

IPTL pia haikuwahi kupewa mkataba wala kutetewa na UKAWA.
 
Mtihani wa kwanza wa Makufuli
Ni shujaa kweli au ni Chui wa karatasi punde tutajuaa
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom