Serikali: Kila Mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi

Juzi Kati nimeenda ku-renew leseni ya biashara nimeandaa 52k niliyozoea, nafika naambiwa eti kuna upuuzi mwingine umeongezeka inaitwa service levy. Kwahiyo itakuwa jumla 77k (52+25 k)

Sijui ni national wide, sijui ni halmashauri yetu!!

Upuuzi!!!!
Service levy ya zaman Sana,
sema ulipona pona TU mkuu
 
Hii itaitwa Kodi ya kichwa !! Hakiyani tulipiga hatua 6 mbele ,Sasa tumerudi hatua miaka miaka ya 1954 nyuma.kazi kwelikweli !! Watupatie tu tutalipa maana tumekopa Sana huko wordbank ,Imf .hakuna namna tupeni hizo control number tu , tulipe hiyo Kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hii utasikia haiwahusi wa Zanzibari, wakatu mikopo yote wamechukua wao
 
Mzee wa watu, Ndugai alishambuliwa sana kwa kejeli na mtusi alopojaribu kukosoa hii selikali ya kodi, tozo na mikopo, kwa sasa mwananchi hana tena mtetezi, lile tabaka la watawala na watawaliwa limeshashika hatamu.
Selikali hii sioni ikitafuta mbinu mbadalabza kukusanya mapato hasa kupitia laslimali zetu zaidi ya kukopa na kuwakamua walalahoi kwa kodi na matozo zisizoisha.
Mitaani kwa sasa tunalipishwa elfu 3 badala ya elfu 1 kwa ajili ya uzoaji taka, gari lenyewe likopita kuliona tena ni majaaliwa.
Maendeleo kwa mtanzania wa kawaida yatachelewa sana.
 
Kodi ya kichwa inarudi, nakumbuka miaka ile ya gizani kule kwetu watu wengi walikimbilia Malawi na Zambia kwasababu ya ile Kodi..........
 
Juzi Kati nimeenda ku-renew leseni ya biashara nimeandaa 52k niliyozoea, nafika naambiwa eti kuna upuuzi mwingine umeongezeka inaitwa service levy. Kwahiyo itakuwa jumla 77k (52+25 k)

Sijui ni national wide, sijui ni halmashauri yetu!!

Upuuzi!!!!

Mimi nimeambiwa kuanzia sasa wafanyakazi wangu wa Bar wanatakiwa kulipiwa Kodi kila mwezi! Inaitwa SDL!
 
Mwakani wataweka kodi kwenye Mbunye.
Walipoingia madarakani walianza
Tozo za simu, makato ya jengo kwenye luku next kodi kwenye Mbunye
 
Unalipa Kodi unaingiza Nini?
umewapa kazi?au mitaji ya biashara?
Hauwezi kuvuna kitu ambacho haujapanda.
Nchemba ni mzigo.
Sasa hivi hakunaa wa kututetea watu wanakaribishwa kuramba assaal
Kwani hapo hulipi kodi ya bidhaa ununuazo?
 
Kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao"

- @mwigulunchemba ,Waziri wa Fedha na Mipango
Mafuta tu (petroli na dizeli) yana utitiri wa Kodi na tozo mbalimbali zaidi ya 20🙄 ambazo zimesababisha gharama na bei za kila kitu kupanda. Na hapa kila mwananchi anahusika kupitia kulipa bei kubwa za nauli, vyakula, vinywaji, mavazi, mawasiliano, umeme, nk.

Mwigulu Nchemba bado haridhiki na yote hayo, anataka apelekee watu Kodi za kughushi na kubambikizia kupitia simu!!!
 
View attachment 2261264

"Kila mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi. Ili kutimiza amza hiyo, Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi"

"Kwa kuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unamtaka kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 au zaidi kujisajili NIDA, napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi"
"Kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao"

- @mwigulunchemba ,Waziri wa Fedha na Mipango

#BajetiKuu
Yes it can be done! Na kuwasaidia vijana zaiadi ya hao milioni 7. Na wakatengenezewa ajira endelevu. Kuna nchi tayari wanafanya hivyo na tax base yao imekuwa for 45% . Ukiiangalia unaweza ona aiwezekani na pia ni kituko- Lakini hii inaweza kuwa mkombozi wa Vijana wetu hapa nchini.
 
Katika hili waziri amepuyanga haliwezi kuwa applicable maana hakuna mazingira yaliyopo ya kuwezesha hilo liwezekane, maana ktk bajeti yake amekiri kuwa kuna tatizo kubwa la ajira hasa Kwa kundi kubwa la vijana na akaenda mbele na kusema wazazi tena wazee ndiyo wanalihudumia kundi hilo kutokana na kutokuwa na ajira wala mitaji na akadai serikali lzm ije na mkakati wa kulisaidia kundi hilo moja akasema wameongeza bajeti ya kilimo, mifugo nk

Sasa hilo pendekezo hata halijaanza utekelezwaji wake hapohapo unaotaka uwasaidie unataka walipe kodi wee uliona wapi mheshimiwa in bwege voice

Hili pendekezo lingekuja miaka 2 au 3 hivi ingekuwa sawa siyo sasa
Hujui unalipa kodi bila kutambulika kuwa ni mlipakodi?
 
Mimi nilidhani kila ninapofanya manunuzi huwa nalipa kodi.

Kwa hiyo kwa andiko lako unataka walio chini ya 18 wauziwe bidhaa zisizo na kodi ama?.
wafanyakazi wote wa umma na sekta binafsi wanalipa kodi wanaponunua bidhaa lakini wanalipa kodi kwa kukatwa kwenye mishahara yao. Hii ilikuwa substandard, wafanyakazi wa umma walikuwa wakilipa kodi kuliko wananchi wengine mfano mkulima, mfugaji, mfanyabiashara nk
 
View attachment 2261264

"Kila mtanzania mwenye umri wa zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi. Ili kutimiza amza hiyo, Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi"

"Kwa kuwa utaratibu wa usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unamtaka kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18 au zaidi kujisajili NIDA, napendekeza kuwa wale wote wenye NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika ndani ya nchi"
"Kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao"

- @mwigulunchemba ,Waziri wa Fedha na Mipango

#BajetiKuu
Na sisi vijana wa CCM hizi kodi zinatuhusu?
 
Back
Top Bottom