Serikali iwakopeshe wanachuo pesa za ada, hizo Ada vyuo ndio vinazitegemea kujiendesha

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,908
51,904
Kwanza nishukuru Serikali kwa kuongeza mzunguko wa pesa mikoa mbalimbali kwa kuwakopesha wanafunzi pesa za chakula na malazi kwenye vyuo vilivyoko nchi nzima.

Pesa hizo wakizipata watazitumia huko wanakoenda kwa kulipia malazi, chakula nk hivyo kuongeza mzunguko wa pesa eneo husika kwa hela watakazotumia wakiwa maeneo ya vyuo viliko sababu njia mojawapo ya kuongeza mzunguko ni hi ya kuwakopesha wanavyuo.

Shida ipo kwenye wanafunzi wengi kunyimwa pesa ya Ada. Ada ndio Vyuo Roho yao ilipo bila Ada vyuo vitapata taabu mno kujiendesha sababu survival yao inategemea Ada zaidi for their existence.

Serikali Kama bajeti haitoshi basi wafute miradi mingine mipya pesa zipewe za Ada hata kwa wanafunzi wote ili vyuo vichangamke na kutoa ajira mpya nk wanafunzi serikali imewakumbuka kwa kuwapa si haba food and accommodation lakini ikasahau kutoa stimulus package kwa vyuo kwa kuhakikisha wanafunzi wengi inawapa hela ya Ada!!

Vyuo vingi vitakuwa na wakati mgumu sababu mwanafunzi ana pesa ya kula na kulala wakati chuo hakina pesa ya kutosha kutokana na wanafunzi kukosa pesa ya Ada kukilipa chuo.

Haya mambo ya mikopo kunakiwa kubalance mwanafunzi asiumie na chuo kisiumie utoaji mkopo ilivyotolewa safari hii imeegemea zaidi kwa wanafunzi tu na kutelekeza vyuo kwa kutowapa Ada wanafunzi wapeleke Ada chuoni.

Vyuo vyote vya serikali na binafsi vitapata wakati mgumu kujiendesha labda serikali itoe ruzuku Sababu ya watoto kukosa Ada!!!

Serikali itafute pesa ilipe Ada au ikopeshe ada
 
Back
Top Bottom