Maoni yangu katika Bajeti 2023/2024 eneo la Elimu-Vyuo vya kati

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Nimefuatilia Uwasilishwaji wa Bajeti kuu ya Serikali 2023/2024. Hongera Mh. @mwigulunchemba na timu yako, ila nina jambo ambalo ningependa kupongeza na kushauri ili liboreshwe zaidi.

Ninapongeza hatua ya serikali kuondoa ada kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha 4 na kupangiwa na Serikali kujiunga na vyuo vya ufundi vya DIT, Mbeya University– MUST na Arusha Technical College – ATC.Ni hatua nzuri ila bado haitoshi, sababu kuna wanafunzi wengi wamemaliza kidato cha nne na wamepangiwa vyuo vya kati mbalimbali ambavyo havijatajwa miongoni mwa vyuo ambavyo ada imeondolewa. Mfano ,Kuna wanafunzi kidato cha nne wamepangiwa Mwalimu Nyererere Memorial na vyuo vingine kwa namna hii watapaswa kujilipia ada wenyewe sababu sio miongoni mwa vyuo vilivyotajwa kufuta ada kwa wanafunzi.Hii bado itaumiza wanafunzi wengine waliopelekwa vyuo ambavyo havijatajwa kufutiwa Ada,Je hawa wanafunzi wanasaidiwa namna gani ikiwa na wao pia hawana uwezo wa kugharamia Ada?.

Pia, ninapongeza pia hatua ya kuanzisha programu ya mikopo kwa wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu 2023/2024. Hii ni hatua nzuri lakini bado kuna wanafunzi kidato cha 4 wamechaguliwa na serikali kwenda vyuo vya kati kusomea fani kama "Community Development" mfano Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial na vyuo vingine fani ambazo hazijatajwa kama fani za kipaumbele. Je ,na hawa wanasaidiwa namna gani?

Nakubaliana na hoja ya serikali ya kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi na elimu inayohitajika katika zama hizi za mapinduzi ya nne ya viwanda (4th Industrial Revolution). Kufuatia mabadiliko ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014, toleo la Mwaka 2023 na mabadiliko ya mitaaala yanayofanywa.Ila serikali ingepeleka wanafunzi wa kidato cha nne vyuo vya kati kwa awamu kwa idadi ya uwezo wa serikali kuwahudumia kwa kuwapa mikopo au kuwapa fursa kusoma bure wote kwa awamu kulingana na uwezo wa serikali.

Mbali na hatua hii nzuri bado kuna wanafunzi hawataweza kugharamia Elimu sababu ya gharama. Hivyo nina shauri serikali itoe mikopo kwa wanafunzi wote vyuo vya kati na VETA au ifute ada kwa wanafunzi wote bila kujali aina ya fani ili wanafunzi wote wasio na uwezo waweze kupata fursa ya kupata Elimu na kukamilisha mzunguko wa Elimu kama ambavyo sera ya 2014 inavyosema.

Cc Rais @samia_suluhu_hassan
 
kazi ya kuongoza nchi ni kama kucheza drafti unapanga hapa unapangua unatoa pale una weka pale, mjumbe anahoja hebu waziri nenda kakae na timu yako hili nalo mkalitizame muiweke vizuri muje na majibu mazuri itakayo waridhisha hawa watanzania masikini ili mwisho wa siku tuondoe manung`uniko
 
Vyuo vingi vya kati ambavyo wanafunzi wamechaguliwa ada yake ni kubwa na mzazi ambaye serikali iliona hataweza kulipa ada ya masomo ya sekondari na kumpa offer ya elimu bure hakika nawaambieni hataweza kumsomesha mwanae huyo.Kwa hiyo wengi hawayareport vyuoni .Bora kutoa loan kwa wote pasipo kujali hivi ni kipaumbele au la
 
Back
Top Bottom