Serikali itoe pole tena kwa Wanafunzi waliozama Ziwa Victoria

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,520
86,078
Naandika Kwa uchungu sana, miezi michache iliyopita Kuna wanafunzi walizama hapa Kigoma Kwa mtumbwi.

Leo Tena tukio kama Hilo limetokea, kama kawaida Viongozi wa CCM na Serikali watalitumia Tukio hili kupata political mileage. Dah
---

Shughuli ya kutafuta watu 13 waliozama ndani ya Ziwa Victoria wakitumia mitumbwi imekwama kuendelea leo Jumatatu, Julai 31, 2023 kutokana na hali mbaya ya hewa ndani ya ziwa hilo. Miongoni mwa watu hao waliozama 11 ni wanafunzi wa shule ya Msingi Igundu Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Tukio la kuzama mitumbwi hiyo miwili limetokea jana Jumapili, Ziwa Victoria wakati mitumbwi hiyo iliyokuwa na watu 28 kupigwa dhrouba na kuzama ziwani.

Watu hao walikumbwa na tukio hilo walipokuwa wakitoka Kijiji cha Mchigondo kwenda Kitongoji cha Bulomba, Kijiji cha Igundu baada ya kumaliza Ibada katika Kanisa Takatifu la Mungu wa Kiroho (KTMK) lillopo Kijiji cha Mchigondo wilayani Bunda jana Jumapili saa 12.30 jioni.

Mkuu wa wilaya ya Bunda, Dk Vicent Naano akizungumza na Mwananchi Digital alisema, shughuli za uokoaji zilisimama kutokana na hali ya upepo,”kwahiyo tunajaribu kadri tuwezavyo kupambana na changamoto zilizopo ili tuweze kufanikisha jambo hilo la uokoaji.”

Dk Naano alisema kazi ya kutafuta watu hao wanahofiwa kufariki dunia imekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo jiografia ya eneo husika. Ndugu, jamaa na marafiki wakati wote walikuwa ufukwe wa Kijiji cha Mchigondo kusubiri hatima ya wapendwa wao.

Hadi saa 12:00 jioni ya leo, Mwananchi Digital inaondoka ufukweni hapo, shughuli za uokoaji zilikuwa zimesimama.

Mwananchi
 
Naandika Kwa uchungu sana, miezi michache iliyopita Kuna wanafunzi walizama hapa Kigoma Kwa mtumbwi.

Leo Tena tukio kama Hilo limetokea, kama kawaida Viongozi wa CCM na Serikali watalitumia Tukio hili kupata political mileage. DahView attachment 2704122
Hakuna jambo linalosikitisha kama vifo vya watoto wasio na hatia, ambao tulitakiwa kuwalinda, lakini tunawatelekeza na kuwafanya wasipate nafasi ya kuyafurahia maisha ya hapa Dunia kama tulivyofurahia sisi.

Walaaniwe watawala ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kuwajengea watoto mazingira salama kwa kisingizio hakuna fedha ilihali wanatapanya pesa nyingi kwa mambo ya kipuuzi kabisa.
 
Hao wanafunzi walikuwa wanatoka shule?
 
Back
Top Bottom