10 September 2023
Geita, Tanzania
Wakaazi hao wa mwambao katika kijiji pwani ya ziwa Victoria wilayani Geita wanasema waliamshwa asubuhi mapema sana na watoto walioamka asubuhi na kukutana na kitu cha kutisha mithili ya ruhani kikionekana kuja taratibu kijijini kwao kutoka ziwa Victoria
Baada ya muda kitu hicho kikafikia kijiji na Nyumba kadhaa mapaa yake yachukuliwa na kimbunga cha chamchele kutoka ziwa Victoria wakaazi wasimulia katika video hii hapa chini kitu cha kuogofya kilivyomelea kijiji chao huku mbingu ikigeuka kuwa giza na kusababisha maafa
View: https://m.youtube.com/watch?v=CW3l1VsJ4HE
Watoto wanakijiji wakapiga kelele wazee wakatoka nje na kuona wingu zito likijifungafunga / kujinyonga nyonga mithili ya joka kubwa lililoamka toka ziwani kisha kuanza kusimama kama joka la cobra lililiweza kufika hadi mawinguni kutoka majini na kuanza kuja taratibu kuelekea pwani ya ziwa Victoria ktk kijijini kimoja cha Geita.
Wenyeji wa kandokando ya ziwa Victoria huamini kuwa wakijitokeza watu wengi na kupiga mayowe pamoja na kugonga chochote iwe ngoma mabati kwa wingi wa umoja wao kimbunga kama hicho hakitafika katika makaazi yao, wazee wa maeneo hayo wanasimulizi hizo.
Katika video hii hapa chini Hali kama hiyo ya kimbunga cha chamchele cha maji ziwani imewahi kutokea nchini Kenya tarehe 20 July 2023 na bahati wenyeji walibahatika kuweza kupiga picha za video na kupata uhalisia kinachosimuliwa na kutokea wilaya ya Geita Tanzania na kuchukua hatua za 'kimila' kuepusha madhara.
View: https://m.youtube.com/watch?v=7AfWdI1KGT4
Kimbunga cha Chamchele cha ziwani kitaalamu ni safu ya Maji inayonyonywa na anga inayofanana na kimbunga ya hewa inayozunguka na ukungu unaotokea juu ya maji.
Kinyume na imani maarufu ya wenyeji, mizuka au maruhani ya mababu wa kale huzuka kuwatembelea au kuja kwa kunyanyuka kama joka kuu kudai kafara . Hiki ni kimbunga halisi kisayansi cha chamchele dhaifu (waterspouts) kuliko vimbunga vingine lakini mwingine kinaweza kusababisha vimbunga na dhoruba kali ziwani hadi nchi kavu. Source:30a.com