#COVID19 Serikali itoe mwongozo wa kuainisha ipi mikusanyiko ya lazima na ipi ni mikusanyiko isiyokuwa na lazima

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Habari wanajamvi,

Kuhusiana na janga hili la Corona sasa tumeanza kujionea tena kuwa kila kiongozi wa sehemu anapiga marufuku mikusanyiko isiyokuwa ya lazima. Lakini ukiachilia mbali hili pia tunajionea kuna mikusanyiko inaendelea lakini inahisiwa siyo ya lazima. Sasa kumekuwa na Mkanganyiko hapa, haijulikani Exactly ni ipi ya lazima.

Kuna mifano hapa, Je mikusanyiko michezoni ni ya lazima ama lah?, mikutano ya siasa ni ya lazima ama lah?. Bado kuna utata sababu utakuta mkoa huu unazuia mkutano fulani na kuita ni mkusanyiko usio na lazima, lakini sehemu nyingine mkusanyiko kama huo unaendelea(rejea mikutano ya katambi, shaka, kongamano la CDM tabata).

Kwa nini suala la COVID limekuwa na sera za mikoa wakati linahitaji sera ya Afya ya kitaifa, kwa nini suala la kuainisha mkusanyiko wa lazima vs usio na lazima unafanywa na vyombo vya dola.

Ni wakati sasa wa Wizara husika (AFYA nadhani) kutoa sera au muongozo wa kutambua hii miksanyiko ili hata vyombo vya dola au Tawala za mikoa zinapozuia au kuruhusu mkusanyiko zifuate huu muongozo na si kufanywa kwa utashi wa mtu.

Muwe na Ijumaa Njema Wanajamvi
 
MaCCM wanafaya mikutano mpaka vichochoroni na hakuna hata mmoja anapewa hata kesi ya kuiba kuku.

IMG_20210723_131155.jpg
IMG_20210723_131144.jpg
IMG_20210723_131152.jpg
 
Back
Top Bottom