Serikali itoe elimu ya kozi za ufundi online

Serikali itoe elimu ya kozi za ufundi online

MKuu bwana sasa sijui tunabishana nini....kwenye ufundi unapewa malelekezo na ticha na unafanya darasani, tofauti hapa unapewa maelekezo kwenye compyuta na uinafanya mwenyewe.....it is the same thing...chukulia kupamba keki...kompyuta inakuambia kwanza chukua unga chekecha je hapa kuna tofauti gani ukiwa darasani mwalimu anapokuambia chukua unga sasa chekecha????? labda useme wewe courses gani za ufundi haziwezi kufundishwa online na serikaliianzie hapo kufanya utafiti?
Nakubaliana na hoja yako, hii inakuwa na tofauti gani kati ya kutumia kitabu chenye miongozo na kutekeleza?

Kwenye vitabu ni fasihi andishi, kweye 'online' ni fasihi simulizi.

Kwenye ufundi, ni kutenda kwa vitendo.

Kijana aliyehitimu chuo kikuu kwenye ufundi wa magari hawezi kuwa bora zaidi kuliko yule aliyeko gereji.​
 
Kwanini elimu hiyo itolewe na serikali?
  • Kwa hali ilivyo vitahitajika vikao kwa kipindi cha mwaka mzima ili kuandaa mchakato wa kuandaa mtaala wa hiyo elimu.
  • Halafu itachukua vikao vingine vyakutosha ili kuandaa na kuupitisha mtaala huo pamoja na hafla mbali mbali.
  • Kutahitajika mchakato wa manunuzi ya vifaa vitakavyotumika kurekodi hayo mafunzo na kuyasambaza mtandaoni.
Mpaka masomo yatolewe mtandaoni tutakuwa tumetumia billions of shillings kutoa mafunzo ambayo probably yapo outdated maana ufundi huenda haraka zaidi na wakati kuliko nadharia.

YouTube, Google na Chatgpt ni bure.
 
Inabidi aanze kufuatilia matangazo maana Tangazo liliopita ilikuwa Januari.

Thanks mkuu sikujua kitu kama hiki kipo,rafiki yangu ni mlemavu wa miguu, katika discussions zetu nikamshauri kufanya kazi ya ukarani manake unachotakiwa ni kusikiliza simu na kujua kompyuta...maana unakaa kwenye kiti mizunguko ni michache .ukiona mahali zinatolewa free online mambo hayo ni PM tafadhali.
 
Hata akiweza kupata ujuzi wa mikono siyo mbaya, maana Halmashauri pia zinakopesha 10% kwa walemavu hata mmoja anapata.

Akishakuwa na kiujuzi na kimradi ni rahisi kujiendeleza
 
Kwanini elimu hiyo itolewe na serikali?
  • Kwa hali ilivyo vitahitajika vikao kwa kipindi cha mwaka mzima ili kuandaa mchakato wa kuandaa mtaala wa hiyo elimu.
  • Halafu itachukua vikao vingine vyakutosha ili kuandaa na kuupitisha mtaala huo pamoja na hafla mbali mbali.
  • Kutahitajika mchakato wa manunuzi ya vifaa vitakavyotumika kurekodi hayo mafunzo na kuyasambaza mtandaoni.
Mpaka masomo yatolewe mtandaoni tutakuwa tumetumia billions of shillings kutoa mafunzo ambayo probably yapo outdated maana ufundi huenda haraka zaidi na wakati kuliko nadharia.

YouTube, Google na Chatgpt ni bure.
Kweli kuna serikali isiyojua kunatakiwa technology innovations kila muda mpaka itoe mafunzo outdated, kama ni hivyo serikali yetu iko hopeless kabisa..
 
Inaitwa ufundi stadi, nadharia kidogo, vitendo zaidi.
 
Kweli kuna serikali isiyojua kunatakiwa technology innovations kila muda mpaka itoe mafunzo outdated, kama ni hivyo serikali yetu iko hopeless kabisa..
Serikali inafahamu lakini shughuli za kiserikali zina ka-process ambako ni very complicated na kanakula hela nyingi sana
 
Ni wazo zuri, ila ufundi unahitaji vitendo zaidi, na vitendo vinatakiwa vifanyike maeneo ya kazi/ karakana.​
Online courses ni nzuri endapo una elimu msingi inayo husu utakacho soma online kumbuka tekinolojia ina badilika na usipo badilika jinsi tekinolojia inavyo badilika unaachwa nyuma sana unakuwa umepitwa na wakati
 
Hata akiweza kupata ujuzi wa mikono siyo mbaya, maana Halmashauri pia zinakopesha 10% kwa walemavu hata mmoja anapata.

Akishakuwa na kiujuzi na kimradi ni rahisi kujiendeleza
Ujuzi wa mikono kama upi mkuu embu fafanua...
 
Je ni watanzania wangapi wanaelewa kuhusu online course.

Watanzania bado wako nyuma aache umbea aje akae YouTube kusoma au katika website n.k

Serikali ifanye hivyo Ila output itakuwa tofauti na in put.

Watanzania tupo nyuma sana bado hatuji matumizi sahihi ya mitandao.
 
Huko online kuna kilakitu.

Ni personal desicion, Wewe mwenyewe tu hujaamua kuzitafuta hizo course!!
 
Back
Top Bottom