Serikali isipoteze pesa kununua dawa za kupunguza makali ya UKIMWI

TULIA SOMA MARAMBILI KABLA YA KU-COMMENT
90% ya maambukizi ya ukimwi inatokana na kufanya ngono., tena ngono zembe.
Sasa ili watu waache kale kamchezo katamu, nashauri serikali isinunue hizo ARVs kama inavyofanya sasa, maana watu hawaachi ngono zembe kwa kuwa ARVs watapewa BURE.
Hivyo nashauri tusipoteze fedha zetu za maendeleo kuhudumia watu wanao fanya ngono zembe, ili likimkuta ajue dawa za bure hakuna.
Nafikiri hii itasaidia kufanya Watanzania waache zinaa, mtu unajuwa ukipata ngoma basi unapoteza maisha.
*** HII INAFANANA NA YA WANAFUNZI WANAOPATA UJAUZITO. Shangilieni na hili kama kweli nyinyi ni wazalendo***
Ni hayo tu waungwana.

Sasa wakiambukiza Kifua Kikuu kwenye basi na mikusanyiko inakuwaje?
 
TULIA SOMA MARAMBILI KABLA YA KU-COMMENT
90% ya maambukizi ya ukimwi inatokana na kufanya ngono., tena ngono zembe.
Sasa ili watu waache kale kamchezo katamu, nashauri serikali isinunue hizo ARVs kama inavyofanya sasa, maana watu hawaachi ngono zembe kwa kuwa ARVs watapewa BURE.
Hivyo nashauri tusipoteze fedha zetu za maendeleo kuhudumia watu wanao fanya ngono zembe, ili likimkuta ajue dawa za bure hakuna.
Nafikiri hii itasaidia kufanya Watanzania waache zinaa, mtu unajuwa ukipata ngoma basi unapoteza maisha.
*** HII INAFANANA NA YA WANAFUNZI WANAOPATA UJAUZITO. Shangilieni na hili kama kweli nyinyi ni wazalendo***
Ni hayo tu waungwana.
Upo karibu sana kuletewa HIV na Mke wako au yule Malaya wako unayedhania watu hawamjui ndiyo utajua wanaokunywa dawa walipaje??

'Muosha huoshwa'
 
naona mtoa mada umeanza muelewa mkuu wa kaya...na umeanza kumuunga mkono tunataka watu kama ww kwenye hii serikali yote hako kamchezo kaishe kabisaa
 
Hahahah

Ukimsoma mtoa mada btn the line utamwelewa

However, utakuwa ni uamuzi mbovu wa kihistoria wenye massive impact kwenye population na economy
Serikali makini yeyote haitokaa kufikir hivyo....
Mungu mwenyewe atunusuru

Mkuu;
Afadhali umemwelewa mleta mada lakini namuunga mkono pia. Nipo naye 100m kwa 100. Hofu inawashika wakubwa kwani wengi waliukwaa kutokana na viherehere vyao kuwatenda wake za watu na vijisichana ili wavipe kazi. Sasa mnafurahi kuwa kuna ARV za bure hamhusiki kuwanunulia wale mlio waambukiza kwani serekali ndiyo inahusika.
Swali ni kwamba, kwa nini serekali hiyo hiyo isihusike kuwasomesha hao mabinti ambao ni hao hao wakuu eg waalimu wao, maofisa elimu na wengine wengi tu wanawapa hizo mimba?? Wawapangie mpango waweze kusoma hata ka ni shule spesheli.
Haya, tuangalie pia ugonjwa mwingine unaopukutisha watu kwa wingi, Kisukari. Hata tu kuwapunguzia bei ya dawa na mnajua kuwa kila siku lazima wale dawa ambazo ni bei ghali ajabu. Jamani, msiangalie upande mmoja tu, angalieni na huku kwingine.
 
Ulifikiri kuhusu watoto waliozaliwa na maambukizi?
Wao kosa la ni nini mpaka wasipewe hizi dawa?
 
Mkuu pole sana. Yaelekea ni mdau wa NGO inayohimiza ngono kwa wanafunzi halafu mnawahadaa kuwa watarudi shule wakisha jifungua. Mkulu kasema noooooooo. Sasa hasira zako unazihamishia kwenye ngoma (HIV)
 
Kalianzisha mwenye nyumba kutosomesha wazazi. Hivyo tunamshauri maeneo mengine ya kubana matumuzi. Unapo mzuia binti aliyepata ujauzito asiendelee na masomo ni unyama sana.
Mimba mashuleni zinaletwa na ngono.
Ukimwi unaletwa pia ba ngono 90%.
Lengo wote tuache Ngono, tusihukumu wanafunzi wakike tu wanaopata ujauzito
Kalianzisha ili Watoto wetu wajali Masomo, wajiepushe na Ngono Zembe". Kazi ya mwanafunzi ni Kusoma Ngono baadaye. Nam support Mkulu. Wanafunzi siyo Wazazi si wajibu wao.
 
Wale wachangiaji wenye mrengo wa upinzani hua mnaonekana n great thinkers lakini kwa hapa mmezengua kinoma.
Narudia tena tumien akili kufikiri badala ya hisia kisa tu wamesemwa watu wenye ukimwi. Tumieni akili
Cc Babati, kisu cha ngariba, tety
 
Acha upuuzi wako,unadhani arvs kutolewa bure ni tatizo,hivi hata hizo dawa ulishawai kuziona,kumeza kwenyewe mtihani.
 
Back
Top Bottom