Watu watano wanaacha kutumia dawa za ARV kila mwaka

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
WAZIRI wa afya Ummy Mwalimu ameeleza kati ya watu 100 Tanzania wanaoishi na virusi vya ukimwi 95 wanatumia dawa za kufubaza virusi (ARVs) huku watano kati yao wanaacha dawa hizo ,suala ambalo linakwamisha juhudi za mapambano dhidi ya gonjwa hilo.

Aidha amewaasa , wanaoishi na Virusi vya Ukimwi kutoacha kutumia dawa hizo na kuiasa jamii kuacha ngono zembe ili kujiepusha na maambukizi mapya ya Ukimwi.

Akizungumza na Wananchi katika kituo Cha Afya Disunyara na Mwendapole Kibaha mkoa wa Pwani, wakati alipoambatana na Mkurugenzi wa Mfuko wa kimataifa wa kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya (HIV), kifua kikuu (TB) na malaria (Global Fund) Peter Sand ,Ummy alieleza Kuwa ,hata Kama wanaona kuna unafuu wenye VVU wasiache matumizi ya dawa hizo .

Ummy alieleza, wanaona kuna kusuasua kwa matumizi ya dawa za ARV Kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi hivyo kusipokuwa na umakini wakati tunakaribia kuushinda tunaweza kurudi nyuma.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Abubakari Kunenge alieleza, Global Fund wanasaidiana na Serikali ya Rais Samia Suluh Hassan katika kuboresha huduma za afya.

Alieleza ,mkoa wa Pwani umefanikiwa kusogeza huduma za afya karibu na jamii ili kuwaondolea kero wananchi.

"Tunashukuru Waziri kwa ujio wako na mgeni katika mkoa wetu kujionea jinsia tunavyofanya kazi ya kutoa huduma ya afya kwa jamii"alisema Kunenge.

Mkurugenzi huyo wa Global Fund , Sand alifafanua Mfuko huo una utaendelea kushirikiana na nchi ya Tanzania na Kuna mahusiano ya kipindi kirefu ,na aliwahakikishia kuendelea kusaidia ili kuboresha sekta ya afya.
 
Shida kuna kuwa kuna uvumi kuwa kuna dawa za kienyeji zinaponesha ukimwi hata humu kuna jamaa wanajinadi wanauza dozi laki 9 kwa kuanzia matokeo yake mtu anaacha chap sana unamsafirisha
 
Back
Top Bottom