Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Picha na Pixabay.
Uwanja mpya wa JKNIA ni kioo cha nchi yetu yaani ni kama uso au sebule au mapokezi ya wageni wanaotembelea nchi yetu.
Uwanja wetu mpya wa JKNIA unasifiwa kuwa ni moja ya viwanja vipya vya ndege ambavyo vina hadhi ya kimataifa na sifa hizo ni kutoka kwa wageni mbalimbali wanaofika uwanjani hapo.
Lakini, kumezuka tabia ya baadhi ya watu kujichukulia picha za video na picha za kawaida za uwanja huo mpya na kuzisambaza mitandaoni na sehemu zingine.
Si jambo baya kwa watu kupiga picha zinazowahusu au (selfie) lakini picha zingine ni lazima zipatiwe kibali maalum kutoka mamlaka ya viwanja vya ndege.
Sababu kubwa ni usalama wa uwanja huo na abiria wote wanaoondoka na kuingia nchini Tanzania pamoja na wale wasindikizaji na watumishi au wafanyakazi wa kila sekta wanaofanya kazi ndani ya uwanja huo.
Katika miaka ya hivi karibuni suala la usalama limekuwa ni la lazima na linalopewa kipaumbele na nchi nyingi tu ambazo zinakuwa zimeamua kujenga au kupanua viwanja vyao au miundombinu muhimu iwe viwanja vya ndege, njia za reli, barabara na za majini.
Matishio ya usalama kwa uwanja wa ndege kama JKNIA yanaweza kuwa ni pamoja na watu wabaya kuanza kuchukua picha za uwanja huo kwa ajili ya kutengeneza mashambulizi au kwa kiingereza huitwa "reconnaissance" au "recon" ambapo mhusika anakuwa kipita sehemu lengwa kuchukua picha za video na za kawaida kwa ajili ya kwenda kutengeneza mashambulizi.
Hivyo ni jukumu la watu wa kitengo cha usalama kiwanjani hapo kuhakikisha kunakuwepo na alama au matangazo ya kutoa onyo kukataza kuchukua picha katika eneo lote la uwanja na viunga vyake.
Iwepo adhabu ya faini kwa atakaekiuka agizo hilo au kufunguliwa mashtaka kwa kukiuka onyo lililowekwa sehemu ya wazi.
Endapo mtu atahitaji kuchukua picha za video au za kawaida basi atapaswa kuwasiliana na kitengo maalum cha mahusiano na wateja au enquiries/cutomer services ambao watamuelekeza kwa afisa habari ambae mara nyingi huitwa "uncle Frank" ambapo watapata maelekezo yote na kupatiwa kibali.
Kuwepo kwa kibali kutasaidia kudhibiti uchukuaji holela wa picha hizo na pia kuwepo na utaratibu kwa wale wambao wanahitaji kutumia uwanja huo kwa shughuli kama sherehe, uchukuaji picha za filamu au matumizi mengine ya kijamii.
Huu ni ushauri kwa vyombo vya usalama na waziri wa mambo ya ndani kwani ni jukumu lenu kuhakikisha miundombinu hii ambayo ni kielelezo cha jitihada za serikali kuikwamu nchi kiuchumi yalindwa kwa gharama zozote zile.