Serikali ipige marufuku uvaaji wa nguo fupi kwenye mabaa na sehemu zingine zinazotoa huduma za chakula na vinywaji

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,028
144,381
Habari wadau.

Uvaaji wa nguo fupi kwenye baadhi ya mabaa na mighahawa limekuwa ni kama jambo la kawaida ingawa kwakweli halipendezi na ni udhalilishaji wa utu wa mwanamke.

Na Kwasababu hakuna sheria inayokataza jambo hili, inaonekana pia ni sera ya baadhi ya wamiliki wa mabaa na mighahawa kawataka wahudumu wa kikee kuvaa vinguo vifupi tena sometimes vinavyopotiliza kiasi kwamba kina dada hawa inakuwa tabu hata kuinama ikitokea kaangusha sahani,chupa, n.k.

Ni wazi baadhi ya wamiliki wanakuwa na utaratibu huu kwa masilahi yao ya kibiashara wakiamini kina dada wanaovaa nguo fupi huvutia wateja wa kiume (vijana, kina baba na hata baadhi ya wazee ambao ujanja haushi)

Ukweli ni kwamba,kinachovutia wateja ni ubora wa huduma, lugha za wahudumu, eneo na mazingira ya biashara ilipo,bei, n.k na si mavazi mafupi ya wahudumu wa kike japo naamini wako baadhi ya wahudumu wasio na maadili hufurahia uvaaji huu wakiamini watapata wa kutoka nao.

Yaani kuna baadhi ya hizi sehemu inataka moyo kuambatana na mtu kama mzazi wako hasa mama wa kukuzaa ingawa hali hii siku hizi imezoeleka na kuonekana ni jambo la kawaida ingawa wewe na mzazi wako au Shanghai yako, n.k wote hulazimika kuamisha macho muhudumu wa aina hii anapopita mbele yenu(kufa na tai shingoni) kwani huu si utamaduni wetu.

Najua kuna watu watapinga wazo hili na kudai haya ni mabadiloko yanayotokana na wakati na kwamba dunia ya sasa ndio inavyokwena.Hata hivyo, watu hawa wakumbuke mavazi ya aina hii hayaruhusiwi kuvaliwa na watumishi wa umma iwapo makazini na hata vyuo vikuu vingi zikiwemo vya binafsi haviruhusu uvaaji wa aina hii katika mazingira ya chuo na wanaokiuka sheria huchukuliwa hatua.

Sasa tujiulize, kama ni kwenda na wakati, mbona ni marufuku kuvaa hivyo vyuoni, kwenye ofisi za umma au kuingia kwenye ofisi za serikali ukiwa na mavazi ya aina hiyo?

Nadhani wakati umefika uvaaji huu udhibitiwe kwa kuwataka kina dada hawa kuvaa nguo zinazofika kwenye magoti na kama ni lazima kuruhusu, basi waruhusiwe kuvaa nyakati za usiku au waruhusuwe huko kwenye club za usiku tu.

Tukumbuke tatizo la ajira linafanya watu wasichague kazi hivyo si wote wanapenda kuvaa nusu uchi na kudhalilisha milo yao hivyo tuwalinde dada zetu hawa kwa sheria maalumu na si kwa kuimba kinafiki kuhusu maadili yetu.

Katika kuandaa msaada husika,serikali inaweza kukusanya maoni ya kina dada hawa kuona kama wanaridhika na uvaaji huu na pia kama wako wanamiliki wanaowataka kuvaa vinguo vifupi wawapo kazini.
 
Sema Ianze Kutoza Kodi Wavaaji
๐Ÿ˜€๐Ÿ˜๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜…๐Ÿ˜„๐Ÿ˜ƒ๐Ÿคฃ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜๐Ÿ˜€๐Ÿ˜†๐Ÿ˜‰๐Ÿ˜Š๐Ÿ˜Ž๐Ÿ˜„๐Ÿ˜…
 
Habari wadau.

Uvaaji wa nguo fupi kwenye baadhi ya mabaa na mighahawa limekuwa ni kama jambo la kawaida ingawa kwakweli halipendezi na ni udhalilishaji wa utu wa mwanamke....
Ni kweli uliyoyasema nadhani hilo linatakiwa lirudi kwetu sote hasa sisi wanaume.Tuwafanye watu wachukie tabia ya kuwaona dada/mama zetu wako nusu uchi bila ya wao kupenda.

Yaani in short wanadhalilishwa kwa ajili yetu sisi wanaume.So wanajme wote kwa kauli moja tukatae kuwa chanzo cha huu uzaliloshaji kwa kuepuka kupata huduma sehemu zenye wahudumu waliovalishwa Nusu uchi.

Hawa ni wakoloni tuu wanaangalia maslahi yao zaidi kuliko utu,hawanatofauti na wale mabosi tunaowasikia kule arabuni wanachowafanyia dada zetu.
 
Naona huwa unapinga mambo mengi ya anco magu,lakini ukweli nawe huna tofauti na unayempinga-ushamba ambao unashindwa kutofautisha kuwa sasa tupo karne ya 21.

Muda una shape mambo mengi hapa ulimwenguni usilazimishe watu waishi mambo ya karne ya 15-kama amabvyo sayansi na technology inavyokuwa mambo nayo yanatakiwa kubadilika,ndio maana sasa hivi kuna Uhuru was kuchagua uishi kwa namna gani.

Kaishi said Arabia utapata wanawake ambao hawavai nguo fupi,na huko Saudi napo kuna mambo mengi siku hizi yanabadilika.
 
Habari wadau.

Uvaaji wa nguo fupi kwenye baadhi ya mabaa na mighahawa limekuwa ni kama jambo la kawaida ingawa kwakweli halipendezi na ni udhalilishaji wa utu wa mwanamke....
Unawaza kisichowezekana. Dunia ilishatoka huko.Mbona husemi wamasai wanaotembea wakining'iniza,au macho yako yanamulika kina dada tu?
 
Cha kishangaza siku hizi hata makanisani Wengine wanavaa sawa na kwenda uchi, hata makazini Pia , kwenye maharusi!

Yani ni mmomonyoko wa maadili mema kwa kiasi kikubwa sana!

Inasikitisha!
 
Acha wivu wewe, kaa na flat screen yako ukiendelea kuangalia TBC.

Bar unafuata nini?

Unafikiri nani ataenda bar ambayo wahudumu wamevaa mabaibui?

Kila sehemu Ina taratibu zake Dada.
 
Habari wadau.

Uvaaji wa nguo fupi kwenye baadhi ya mabaa na mighahawa limekuwa ni kama jambo la kawaida ingawa kwakweli halipendezi na ni udhalilishaji wa utu wa mwanamke.

Na Kwasababu hakuna sheria inayokataza jambo hili, inaonekana pia ni sera ya baadhi ya wamiliki wa mabaa na mighahawa kawataka wahudumu wa kikee kuvaa vinguo vifupi tena sometimes vinavyopotiliza kiasi kwamba kina dada hawa inakuwa tabu hata kuinama ikitokea kaangusha sahani,chupa, n.k.

Ni wazi baadhi ya wamiliki wanakuwa na utaratibu huu kwa masilahi yao ya kibiashara wakiamini kina dada wanaovaa nguo fupi huvutia wateja wa kiume (vijana, kina baba na hata baadhi ya wazee ambao ujanja haushi)

Ukweli ni kwamba,kinachovutia wateja ni ubora wa huduma, lugha za wahudumu, eneo na mazingira ya biashara ilipo,bei, n.k na si mavazi mafupi ya wahudumu wa kike japo naamini wako baadhi ya wahudumu wasio na maadili hufurahia uvaaji huu wakiamini watapata wa kutoka nao.

Yaani kuna baadhi ya hizi sehemu inataka moyo kuambatana na mtu kama mzazi wako hasa mama wa kukuzaa ingawa hali hii siku hizi imezoeleka na kuonekana ni jambo la kawaida ingawa wewe na mzazi wako au Shanghai yako, n.k wote hulazimika kuamisha macho muhudumu wa aina hii anapopita mbele yenu(kufa na tai shingoni) kwani huu si utamaduni wetu.

Najua kuna watu watapinga wazo hili na kudai haya ni mabadiloko yanayotokana na wakati na kwamba dunia ya sasa ndio inavyokwena.Hata hivyo, watu hawa wakumbuke mavazi ya aina hii hayaruhusiwi kuvaliwa na watumishi wa umma iwapo makazini na hata vyuo vikuu vingi zikiwemo vya binafsi haviruhusu uvaaji wa aina hii katika mazingira ya chuo na wanaokiuka sheria huchukuliwa hatua.

Sasa tujiulize, kama ni kwenda na wakati, mbona ni marufuku kuvaa hivyo vyuoni, kwenye ofisi za umma au kuingia kwenye ofisi za serikali ukiwa na mavazi ya aina hiyo?

Nadhani wakati umefika uvaaji huu udhibitiwe kwa kuwataka kina dada hawa kuvaa nguo zinazofika kwenye magoti na kama ni lazima kuruhusu, basi waruhusiwe kuvaa nyakati za usiku au waruhusuwe huko kwenye club za usiku tu.

Tukumbuke tatizo la ajira linafanya watu wasichague kazi hivyo si wote wanapenda kuvaa nusu uchi na kudhalilisha milo yao hivyo tuwalinde dada zetu hawa kwa sheria maalumu na si kwa kuimba kinafiki kuhusu maadili yetu.

Katika kuandaa msaada husika,serikali inaweza kukusanya maoni ya kina dada hawa kuona kama wanaridhika na uvaaji huu na pia kama wako wanamiliki wanaowataka kuvaa vinguo vifupi wawapo kazini.
Nimeikubali hii,ni dhalilisho kwa watoto wetu wa kike
 
Back
Top Bottom