Masawe Fredrick
New Member
- May 17, 2024
- 3
- 0
UMUHIMU WA KUENEA KWA ELIMU MAALUM YA LUGHA ZA ISHARA NA ALAMA
1) Itasaidia ongezeko la wataalam ; hii ni pale tunaelimisha zaidi kuwa kila mtu ana haki ya kupata elimu. Elimu maalum kwa ajili ya wasio ona,wasio sikia, Autism, na watu wengine wenye mahitaji maalumu hawa huwa na uwezo mkubwa sana ata kwenye kufikiri na kutoa mawazo ila changamoto inakuwa ni kwenye mawasiliano hivyo serikali ikijitahidi kuongeza wataalamu wa lugha hizo itatengeneza muunganiko mzuri kati ya watu wenye mahitaji maalumu na wasio hitaji.
2) Itapunguza tatizo la Ajira, hii ni kweli kabisa pale ambapo mfano kiziwi anauwezo wa kufanya kazi ya mikono na ya kutumia mikono pia changamoto ni lugha tu ko serikali ikizingatia itasaidia sana kupunguza umaskini na tatizo la ajira.
3) Itapunguza omba omba na ajali za zisizo za lazima mitaani, omba omba wengi wana changamoto tofautitofauti ambazo zinaweza kutatulika wengine inakuta hawajui ishara ko wanashindwa namna ya kuwasiliana.