papaa musofe
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 842
- 1,475
Awamu ya tano inajinasibu kuwa ni serikali ya masikini na wanyonge
Japo tafsiri ya slogani hiyo pia inaleta utata katika taifa ambalo linapigana kupanda daraja kutoka taifa la watu masikini angalau tufikie ngazi ya taifa tajiri,
Kuiita serikali kuwa ni ya watu masikini na wanyonge,ni kama kuukubali umasikini kwamba ni kitu kizuri na kinatakiwa kufunikwafunikwa na masikini waishi katika hali hiyo wakiamini kwamba hata wakiwa masikini,hakuna tatizo kwa kuwa wameshaambiwa serikali hii ni yao
Mzee Mkapa alikuwa na MKUKUTA na MKURABITA
MKUKUTA ni Mpango wa kupambana na kuondoa Umasikini Tanzania,mkakati huuu ulilenga KUONDOA umasikini na kuwafanya watu wauchukie umasikini,umasikini ni kitu kibaya,unadhalilisha utu,unaua vipaji,unakosesha fursa,Mzee Mkapa alilenga kupambana nao na kuutokomeza kwa vitendo,hakuishia kuuimba majukwaani tu
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiimba tu slogani kuwa ni serikali ya "masikini na wanyonge" umasikini hautolewi kwa kuuimba majukwaani,na umasikini si jambo la kuwafanya watu wajivunie,jitihada zote zifanyike kuhakikisha watu wanauchukia umasikini
Ninachokiona sasa jitihada zinafanyika,si kuwafanya masikini wauchukie umasikini,bali ni kuwachonganisha masikini na watu wa kipato cha kati(wakiwemo watumishi na wafanyabiashara) na matajiri wakubwa,sasa hivi kuwasumbua matajiri wakubwa eti ndio jitihada za kupambana na umasikini,na bahati mbaya watu wakiona matajiri wanahangaishwa,wao nao huridhika bila kujiuliza hiyo ina msaada gani wa moja kwa moja katika kuondoa umasikini wao.
Sasa hata waliokuwa wamepanga maghorofa wakayaachia kutokana na uchumi kuyumba,kutokana na uchonganishi kati ya masikini na watu waliowazidi kipato,utasikia masikini wakisema "wananyooshwa" bila kutafakari kwamba anayewachonganisha,chama chake ndicho kimeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50,na kilitakiwa kumjibu mtu Huyu masikini kuhusu hali yake
Masikini wanaambiwa kwamba umasikini wao,wao hawahusiki,bali hilo janga wameletewa na watumishi wa umma na wafanyabiashara,na kwamba ukipambana nao basi hao masikini watakuwa matajiri.Nadhani hapa ndipo tunapouchimbia mizizi umasikini katika jamii zetu na kuacha kuzipa muelekeo wa kuziongoza zijikomboe,
Hawa matajiri wanaohangaishwa,ukichukua utajiri wao ukagawa kwa watanzania wote, kila mtu apate chake,nadhani kila mmoja ataishia kupata elfu kumi au ishirini,baada ya kugawa,matajiri watakuwa masikini maana Mali zao zimechukuliwa,na wale waliopewa elfu ishirini za mgao watabaki kuwa masikini kwa kuwa huwezi kuwa tajiri kwa kumiliki elfu 20,
Awamu ya tano inahitaji kuandaa mkakati wa kuondoa umasikini kama kweli una nia hiyo,huwezi kupunguza bajeti ya Kilimo utarajie kuondoa umasikini katika sekta hii inayohudumia karibu asilimia 75-80 ya wananchi,na Kilimo sio kulima tu,bali hata kutafuta masoko ya mazao hayo na kuliacha soko lijitawale,
Huwezi kusema unapunguza umasikini bila mkakati wa kuongeza ajira,sasa ni kawaida kuona zimetangazwa nafasi 200 za kazi,wakaomba watu elfu hamsini
JK alikuja na programe ya Kilimo kwanza na nyingine nyingi,japo zilikuwa na shida,lakini zililenga mtu wa chini
Tunaitaka awamu ya tano itengeneze mkakati wa kuondoa umasikini,na isijivunie kuungwa mkono na masikini ili iingie madarakani