Serikali inayotamba kuwa ya "masikini" yamaliza miaka miwili madarakani bila mkakati wa kuondoa umasikini

papaa musofe

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
842
1,000
Awamu ya tano inajinasibu kuwa ni serikali ya masikini na wanyonge

Japo tafsiri ya slogani hiyo pia inaleta utata katika taifa ambalo linapigana kupanda daraja kutoka taifa la watu masikini angalau tufikie ngazi ya taifa tajiri,

Kuiita serikali kuwa ni ya watu masikini na wanyonge,ni kama kuukubali umasikini kwamba ni kitu kizuri na kinatakiwa kufunikwafunikwa na masikini waishi katika hali hiyo wakiamini kwamba hata wakiwa masikini,hakuna tatizo kwa kuwa wameshaambiwa serikali hii ni yao

Mzee Mkapa alikuwa na MKUKUTA na MKURABITA

MKUKUTA ni Mpango wa kupambana na kuondoa Umasikini Tanzania,mkakati huuu ulilenga KUONDOA umasikini na kuwafanya watu wauchukie umasikini,umasikini ni kitu kibaya,unadhalilisha utu,unaua vipaji,unakosesha fursa,Mzee Mkapa alilenga kupambana nao na kuutokomeza kwa vitendo,hakuishia kuuimba majukwaani tu

Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiimba tu slogani kuwa ni serikali ya "masikini na wanyonge" umasikini hautolewi kwa kuuimba majukwaani,na umasikini si jambo la kuwafanya watu wajivunie,jitihada zote zifanyike kuhakikisha watu wanauchukia umasikini

Ninachokiona sasa jitihada zinafanyika,si kuwafanya masikini wauchukie umasikini,bali ni kuwachonganisha masikini na watu wa kipato cha kati(wakiwemo watumishi na wafanyabiashara) na matajiri wakubwa,sasa hivi kuwasumbua matajiri wakubwa eti ndio jitihada za kupambana na umasikini,na bahati mbaya watu wakiona matajiri wanahangaishwa,wao nao huridhika bila kujiuliza hiyo ina msaada gani wa moja kwa moja katika kuondoa umasikini wao.

Sasa hata waliokuwa wamepanga maghorofa wakayaachia kutokana na uchumi kuyumba,kutokana na uchonganishi kati ya masikini na watu waliowazidi kipato,utasikia masikini wakisema "wananyooshwa" bila kutafakari kwamba anayewachonganisha,chama chake ndicho kimeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50,na kilitakiwa kumjibu mtu Huyu masikini kuhusu hali yake

Masikini wanaambiwa kwamba umasikini wao,wao hawahusiki,bali hilo janga wameletewa na watumishi wa umma na wafanyabiashara,na kwamba ukipambana nao basi hao masikini watakuwa matajiri.Nadhani hapa ndipo tunapouchimbia mizizi umasikini katika jamii zetu na kuacha kuzipa muelekeo wa kuziongoza zijikomboe,

Hawa matajiri wanaohangaishwa,ukichukua utajiri wao ukagawa kwa watanzania wote, kila mtu apate chake,nadhani kila mmoja ataishia kupata elfu kumi au ishirini,baada ya kugawa,matajiri watakuwa masikini maana Mali zao zimechukuliwa,na wale waliopewa elfu ishirini za mgao watabaki kuwa masikini kwa kuwa huwezi kuwa tajiri kwa kumiliki elfu 20,

Awamu ya tano inahitaji kuandaa mkakati wa kuondoa umasikini kama kweli una nia hiyo,huwezi kupunguza bajeti ya Kilimo utarajie kuondoa umasikini katika sekta hii inayohudumia karibu asilimia 75-80 ya wananchi,na Kilimo sio kulima tu,bali hata kutafuta masoko ya mazao hayo na kuliacha soko lijitawale,

Huwezi kusema unapunguza umasikini bila mkakati wa kuongeza ajira,sasa ni kawaida kuona zimetangazwa nafasi 200 za kazi,wakaomba watu elfu hamsini

JK alikuja na programe ya Kilimo kwanza na nyingine nyingi,japo zilikuwa na shida,lakini zililenga mtu wa chini

Tunaitaka awamu ya tano itengeneze mkakati wa kuondoa umasikini,na isijivunie kuungwa mkono na masikini ili iingie madarakani
 
Makambo zali

Senior Member
Sep 23, 2017
181
500
Matajiri ni washirika katika maendeleo

Wakati Manji anasota gerezani kwa kesi lukuki,watu masikini walifunga kibwebwe as if sasa mambo yatawanyookea kwa Manji kusakiziwa kesi feki,

Manji kamaliza "misala" yake ,sisi tuliokuwa tumejiandaa na kucheza,hatujaona hali zetu zikibadilika,

Nadhani serikali ijielekeze kwenye hoja za msingi

Hao matajiri wameajiri watu masikini wengi sana,ukimuangusha tajiri mmoja kwa sababu ya "visa na mikasa" ni sawa na kuangusha mti mkubwa,kishindo kitatokea

Tutafakari kwa kina tatizo la umasikini kwa kuangalia "issues" sio watu
 
stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,229
2,000
Wewe hata ukiandika maneno marefu kama gazeti la mzalendo
Ulishatumbuliwa tu
Mbona mlivokua mkila kilaini hamkulia lia?
JF mliiona kama katuni netwrk
Leo ndio mmeiona JF kama DSTV
 
mwl

JF-Expert Member
May 25, 2011
1,101
2,000
Kichaa kapewa Rungu,nchi kuongozwa na kilaza aliejificha kwenye kichaka cha PHD,
Tutakoma na bado kichaa hakijampanda vizuri,kichaa kikipanda vizuri mtahesabu namba za kirumi.
Anhaaa ndio maana mwezi unapokuwa mchanga anakuwa haeleweki, umelinotice hilo? Leo ni mwezi 17, baada ya siku 16 au 17 mchunguze uone. Ni hayo tu.
 
tongs

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
540
1,000
Tupo kwenye vita ya kiuchumi.
Hii nchi ni tajiri kwelikweli.
Msemakweli ni mpenzi wa mungu.
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
6,822
2,000
Awamu ya tano inajinasibu kuwa ni serikali ya masikini na wanyonge

Japo tafsiri ya slogani hiyo pia inaleta utata katika taifa ambalo linapigana kupanda daraja kutoka taifa la watu masikini angalau tufikie ngazi ya taifa tajiri,

Kuiita serikali kuwa ni ya watu masikini na wanyonge,ni kama kuukubali umasikini kwamba ni kitu kizuri na kinatakiwa kufunikwafunikwa na masikini waishi katika hali hiyo wakiamini kwamba hata wakiwa masikini,hakuna tatizo kwa kuwa wameshaambiwa serikali hii ni yao

Mzee Mkapa alikuwa na MKUKUTA na MKURABITA

MKUKUTA ni Mpango wa kupambana na kuondoa Umasikini Tanzania,mkakati huuu ulilenga KUONDOA umasikini na kuwafanya watu wauchukie umasikini,umasikini ni kitu kibaya,unadhalilisha utu,unaua vipaji,unakosesha fursa,Mzee Mkapa alilenga kupambana nao na kuutokomeza kwa vitendo,hakuishia kuuimba majukwaani tu

Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikiimba tu slogani kuwa ni serikali ya "masikini na wanyonge" umasikini hautolewi kwa kuuimba majukwaani,na umasikini si jambo la kuwafanya watu wajivunie,jitihada zote zifanyike kuhakikisha watu wanauchukia umasikini

Ninachokiona sasa jitihada zinafanyika,si kuwafanya masikini wauchukie umasikini,bali ni kuwachonganisha masikini na watu wa kipato cha kati(wakiwemo watumishi na wafanyabiashara) na matajiri wakubwa,sasa hivi kuwasumbua matajiri wakubwa eti ndio jitihada za kupambana na umasikini,na bahati mbaya watu wakiona matajiri wanahangaishwa,wao nao huridhika bila kujiuliza hiyo ina msaada gani wa moja kwa moja katika kuondoa umasikini wao.

Sasa hata waliokuwa wamepanga maghorofa wakayaachia kutokana na uchumi kuyumba,kutokana na uchonganishi kati ya masikini na watu waliowazidi kipato,utasikia masikini wakisema "wananyooshwa" bila kutafakari kwamba anayewachonganisha,chama chake ndicho kimeongoza nchi kwa zaidi ya miaka 50,na kilitakiwa kumjibu mtu Huyu masikini kuhusu hali yake

Masikini wanaambiwa kwamba umasikini wao,wao hawahusiki,bali hilo janga wameletewa na watumishi wa umma na wafanyabiashara,na kwamba ukipambana nao basi hao masikini watakuwa matajiri.Nadhani hapa ndipo tunapouchimbia mizizi umasikini katika jamii zetu na kuacha kuzipa muelekeo wa kuziongoza zijikomboe,

Hawa matajiri wanaohangaishwa,ukichukua utajiri wao ukagawa kwa watanzania wote, kila mtu apate chake,nadhani kila mmoja ataishia kupata elfu kumi au ishirini,baada ya kugawa,matajiri watakuwa masikini maana Mali zao zimechukuliwa,na wale waliopewa elfu ishirini za mgao watabaki kuwa masikini kwa kuwa huwezi kuwa tajiri kwa kumiliki elfu 20,

Awamu ya tano inahitaji kuandaa mkakati wa kuondoa umasikini kama kweli una nia hiyo,huwezi kupunguza bajeti ya Kilimo utarajie kuondoa umasikini katika sekta hii inayohudumia karibu asilimia 75-80 ya wananchi,na Kilimo sio kulima tu,bali hata kutafuta masoko ya mazao hayo na kuliacha soko lijitawale,

Huwezi kusema unapunguza umasikini bila mkakati wa kuongeza ajira,sasa ni kawaida kuona zimetangazwa nafasi 200 za kazi,wakaomba watu elfu hamsini

JK alikuja na programe ya Kilimo kwanza na nyingine nyingi,japo zilikuwa na shida,lakini zililenga mtu wa chini

Tunaitaka awamu ya tano itengeneze mkakati wa kuondoa umasikini,na isijivunie kuungwa mkono na masikini ili iingie madarakani
No Welfare Economy Read here>>the definition of welfare economics
 
gogo la shamba

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
6,670
2,000
hivi wale waliokuwa wanautubiwa na Raisi kwenye mkutano wa ALAT na wenyewe ni miongoni mwa hao wanaoitwa masikini maana walikuwa wanakubali kila lililosemwa
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
6,822
2,000
Mhhh Jamani ni transition Period Jamaan alishasema mkuu
mmm! Hatakama Ni Transition Period isiwe Double standard Ujenzi wa Miundombinu Kasi yake ni kubwa mmno na Hiyo Miundombinu Wanao Faidi ni Hao Wa nje No Welfare For His People?
 
Gobole

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
980
1,000
Hata tuje na program ya kuwalipa maskini mshahara km TASAF bado umaskini utaendelea kuwepo...shida yetu waafrica ni umaskini wa kifikra...ukimpa mtu samaki atamla kesho atataka umpe tena,wala ht kuuliza namna ya kumvua huyo samaki na ukiendekeza kumpa msaada itafika wakati ataona ni msaada ni haki yake na atalalamika asipopewa...na zaidi tufaham kua tumeingia kwenye uchumi wa kibepari ambapo serikali hai control uchumi wa matajiri wala maskini "kila mtu apambane na hali yake"...2Pac aliwahi kuimba and i quote "They got money for war but not for the poors" akimaanisha ht USA kuna maskini na serikali haijawapa kipaumbele maskini km wanavyovipa vita vipaumbele...Tukibadilika ki fikra ht umaskini nao utapungua
 
Kweli kabisa
 
ijooo

JF-Expert Member
May 13, 2017
700
1,000
Tupo kwenye vita ya kiuchumi.
Hii nchi ni tajiri kwelikweli.
Msemakweli ni mpenzi wa mungu.
Hivi hii nnchi imeibiwa na nani ? Kwa nini? Leo wapo wapi? Wanafanya nini ? Magufuli anawajua ? Kama anawajua kachukua hatua gani? Kama hawajui anafanyaje kuwapata ? ......
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom