Serikali inavyochangia udhalilishaji wa elimu ya Chuo Kikuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali inavyochangia udhalilishaji wa elimu ya Chuo Kikuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pax, Aug 27, 2010.

 1. P

  Pax JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa muda mrefu elimu ya chuo kikuu imeendelea kudhalilishwa huku serikali ikifumbia macho jambo hili. Majoho tuliyozoea kuona wahitimu wa vyuo vikuu wakivaa miaka ya hivi karibuni yamekuwa mavazi ya chekechea, what a shame! haikuishia hapo, shule za msingi na sekondari nazo hazipo mbali.

  Pia siku za karibuni tumeona watu wakijipachika degree za Falsafa (PhD) za kununua serikali imeuchuna. Imeendelea viongozi wanatunukiwa PhD za heshima kiholela tu, ati wanaitwa Dr.xxxx, Dr.yyyyy na vyuo ambavyo havina hata merits. Waandishi wa habari nao bila hata aibu wanapublicize huu uozo na uzandiki.

  Serikali gani isiyoweza kusimamia elimu jamani, ikaiacha ichezewe ka uganga wa kienyeji?
  mmhhhh, ishi Tanzania uone kila aina ya vituko.
   
 2. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  For now Tanzania is indeed a lost country..she needs overhaul.
  May be someone like Dr. Slaa might bring some changes
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Mr/miss Pax, wewe uliesoma ume-make difference gani katika taifa hili? Bila shaka wewe na hao chekechea hakuna tofauti na si ajabu hao chekechea huenda wanaafadhali kuliko wewe. Jiulize tangu umegraduate umechangia nini kwenye taifa zaidi ya kuchumia tumbo lako na wanaokuzunguka tu? Ni bora hata hao chekechea wavae si ajabu wanaweza kuja ku-make wonders muda wao utakapofika. Kama unataka uheshimiwe kama graduate jitofautishe katika utendaji wako wa kila siku kwa taifa lako na si kujisifia kwa joho ambalo halina tija wala mchango wowote katika taifa zaidi ya misifa tu kwa mhusika kama wewe unavyotaka misifa.
   
 4. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Pax, kwanza naomba niongezee neno, Hominibus mbele ya jina lako.

  Pamoja na serikali kushindwa kusimamia elimu, hata vyuo vikuu vyenyewe vimeshindwa kusimamia miongozo yao. Naona kundi la wanasiasa sasa wanapata nguvu kiasi kwamba kila mtu anatafuta urafiki na kundi hili.

  Kuna watu wamejipachika, Dr ...... kwa kutumia vyeti bandia. Lakini pia kuna watu wamepewa vyeti na vyuo vyetu hapa hapa nchini bila stahili hiyo.
  Tulimjadili sana Magufuli na PhD yake. wengine walitetea, lakini ukweli utabaki pale pale kwamba hakustahili. Siyo kwa sababu hana uwezo wa kuipata! uwezo huo anao lakini hakuutumia.

  Na hapo ni UD. Ndo alipokuwa akienda siku anazotaka, akisimamiwa na rafikiye, baadaye ikapitishwa walivyotaka wao na leo ni Dr. Sijathibitisha lakini nasikia aliyemsimamia sasa hivi kazawadiwa ukurugenzi ofisi fulani huko Dar!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kinyesi..
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  Mambo mengine yanachekesha kweli
  Yani joho ndo nalo linaendana na elimu,? kwa kweli sijakuelewa, unaongelea udhalilishaji wa tamaduni ama elimu???
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Aiseeeeeeee Dr Jakaya Kikwete
   
 8. P

  Pax JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kama ambavyo mosquito net inaendana na kuzuia maambukizi ya malaria ndivyo majoho yanavyoendana na elimu ya juu, hahahah. Haihitaji ulipiwe Tuition kuelewa nilichomaanisha. Kazi kweli kwa Tanzania kuendelea kama sentensi mbili ka hizi zinakuchukua siku kuzielewa.:confused2:
   
Loading...