RC Chalamila: Daraja la Saba wanaingiza mamilioni, wa Chuo Kikuu wanalaumu mitaala haiwawezeshi kujiajiri

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,119
49,843
RC wa Dar Albert Chalamila amewashangaa watu wanaolaumu Elimu ya Chuo Kikuu Tanzania hususani graduate Kwa kulalamika na kulaumu mitaala ya Elimu na Serikali wakati Kuna mtu ana Elimu ya darasa la Saba tu anaitumia kuingiza Mamilioni Kariakoo na kwingineko.

My Take:
Naunga mkono hoja,haiwezekani mwenye Elimu ya la Saba akaitumia kupata pesa wewe mwenye Elimu ya Chuo Kikuu uwe unalaumu. Vijana wa miaka hii ni hovyo na wazembe sana.

=======

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema wakati wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu wakilalamika kwamba mitaala ya masomo yao haiwawezeshi kujiajiri, wapo watu walioishia darasa la saba wanaoingiza mamilioni ya fedha Kariakoo.

Chalamila amewataka wahitimu wa vyuo vikuu wanaokosa fursa za kuajiriwa, watafakari namna ya kuzigeuza changamoto zilizopo kwenye jamii kujiingizia kipato badala ya kubaki kulalamika.

Ameyasema hayo leo, Septemba 10, 2023 Mlimani City jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuliombea taifa amani, iliyoandaliwa na Kanisa Kuu la Bwana.

Siitetei serikali;

Ukitaka kufanikiwa hapa Tanzania, sahau kuwa una haki ya kuungwa mkono na serikali, fanya mishe zako kwa juhudi.

Tanzania tuna rasilimali na fursa nyingi sana. Ardhi ipo haina kazi, tupambaneni vijana.

Fuga, lima, fanya biashara n.k

Ukienda mpanda kuna maeneo sasa hivi tunavyoongea wanauza shilingi 250,000/= tu kwa ekari moja. Unaweza kupata eneo lako hata ekari kumi ukatumia kukupa pesa.

Nimeenda Kenya mara kadhaa, nikiri kuwa wenzetu ni wachapa kazi kuliko sisi. Vijana wa kitanzania wanawaza kula bata na ngono badala ya kazi. Matokeo yake ni kulalamikia serikali kuomba ajira hafifu za unesi, ualimu. N.k

NB. Ukishindwa kitoboa hapa Tanzania, huwezi kutoboa kwenye nchi yoyote Afrika mashariki.
 
Jadilini tu kila mmoja na mawazo mnaruhusiwa ila msifikie tu hatua ya kubeza elimu, maana watanzania kisa mtu hajasoma sana ananiingiza millioni kadhaa kwa mwezi basi anaweza akaona taaluma ni scam

Watu wapo bize na AI huko duniani, sie tupo kwenye debate lasaba na degree holder mwenye uthubutu zaidi ni nani

Nijuavyo Mimi mambo ya innovations hususani za kiTech hazitaki njaa, hazitaki stress, hazitaki kodi ya nyumba natoa wapi au mchna nitakula nini...zinataka ulale unawaza ile algorithm pale natoka vipi

Ndio maana utawaona hata kina elon mask, ni maisha safi toka wanakuwa hata kama walikuwa si mabilionea ila suala la kukiria bills halikuwa tatizo, kadhalika kina mak Wa meta

Nilitaka nitolee mfano na matajiri wetu Wa hapa ndani ila naona nimechoka kutype makala ndefu
 
RC wa Dar Albert Chalamila amewashangaa watu wanaolaumu Elimu ya Chuo Kikuu Tanzania hususani graduate Kwa kulalamika na kulaumu mitaala ya Elimu na Serikali wakati Kuna mtu ana Elimu ya darasa la Saba tu anaitumia kuingiza Mamilioni Kariakoo na kwingineko.

My Take:
Naunga mkono hoja,haiwezekani mwenye Elimu ya la Saba akaitumia kupata pesa wewe mwenye Elimu ya Chuo Kikuu uwe unalaumu. Vijana wa miaka hii ni hovyo na wazembe sana.

=======

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema wakati wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu wakilalamika kwamba mitaala ya masomo yao haiwawezeshi kujiajiri, wapo watu walioishia darasa la saba wanaoingiza mamilioni ya fedha Kariakoo.

Chalamila amewataka wahitimu wa vyuo vikuu wanaokosa fursa za kuajiriwa, watafakari namna ya kuzigeuza changamoto zilizopo kwenye jamii kujiingizia kipato badala ya kubaki kulalamika.

Ameyasema hayo leo, Septemba 10, 2023 Mlimani City jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuliombea taifa amani, iliyoandaliwa na Kanisa Kuu la Bwana.

View attachment 2745668
Aelezee kwanza,yeye alivyo tumbuliwa ukuu wa mkoa alikuwa na hari gani kifedha?
 
Mfumo wa Elimu na Jamii zilitukuza kwa kutukaza kufanya shughuli fulani kwamba ni za watu wasiokuwa na Elimu.

Mtazamo huo tumeishi nao kwa zaidi ya miaka 21 mpaka kuitwa graduates unadhani ni rahisi kuachana nao?

Ukitafuta, akapata kalaki kako, uanze kufanya hizo biashara za wasiokuwa na elimu kwasasa unakuta na mitozo, mikodi, miushuru mingi na hapo bado mgambo wa jiji hawajaanza kutukimbiza na majiko yetu vichwani.

Msioni hatutoboi, mkadhani hatujaribu!

By the way, Mwambie awache uchawa, anawatia aibu binti zake!
 
Watu wanaoishia darasa saba au kidato cha nne huwa wanaingia mtaani bila matarajio/vipaumbele vyovyote ni kuanza zero kabisa na kupambana taratibu bila pressure yoyote na inachukua miaka hadi 10 mtu kuwa sawa.Sasa kijana aliepoteza muda/ada hadi kafika chuo na kumaliza bila skill yoyote ya kumfanya apambane mtaa atakua tayari kuanza from scratch kama kijana alieishia la saba au kidato cha nne?kulikua na umuhimu gani wa kufika chuo?la msingi ni either mitaala ibadilishwe ienadane na mahitaji ya mtaa au basi vijana waishie kidato cha nne tu watafute skills nyingine zitazowawezesha kujitegemea kama ufundi magari,umeme n.k au hata bila skill yoyote kijana wa kidato cha nne anaweza kuwa na utulivu wa kuanza mdogo mdogo na kukua bila pressure yoyote kutoka kwa jamii kulingana na level ya elimu yake.
 
Ana hoja mfano yeye Chalamila alikuwa na ajira nzuri tu.kama mhadhiri wa chuo kikuu akaona hailipi.akahamia siasa

Elimu yake inamsaidia ku.move around kwenda juu

Elimu mwisho.wa siku.iingize pesa iwe kujiajiri kuajiriwa au kujitosa kwenye siasa nk
 
Back
Top Bottom